KUNYONYESHA MTOTO: Taratibu, faida, madhara, imani potofu

Taratibu za unyonyeshaji zinazopendekezwakunyonyesha mtoto

Shirika la Afya Duniani linapendekeza kufuata taratibu sahihi za kunyonyesha mtoto. Taratibu hizo ni;

 • Mwili wa mama ugusane na mwili wa mtoto ngozi kwa ngozi mara tu baada ya kujifungua
  • Hii husaidia kujenga mahusiano ya upendo kati ya mama na mtoto
  • Pia husaidia kuchochea utengenezaji wa maziwa hususani ya mwanzo yenye rangi ya njano
 • Kuanza kumnyonyesha mtoto ndani ya saa moja baada ya kujifungua
  • Hakikisha mtoto amewekwa vizuri kwenye titi
  • Mpe mtoto maziwa ya mwanzo yenye rangi ya njano ambayo yana viini vingi vya kingamwili
 • Mtoto apewe maziwa ya mama ya mwanzo. Haya ni maziwa yanayotoka siku chache za mwanzo (Siku 2 hadi 3) baada ya mama kujifungua. Maziwa haya yana wanga, protini na kingamwili nyingii zinazoingia mwilini mwa mtoto.
 • Kunyonyesha maziwa ya mama pekee kuanzia mtoto anapozaliwa hadi anapotimiza umri wa miezi 6
  • Mpe mtoto maziwa ya mama pekee katika miezi 6 ya mwanzo
  • Usimpe chakula au kinywaji kingine chochote, hata maji, katika miezi sita ya mwanzo isipokuwa dawa kwa maelekezo ya daktari.
 • Kunyonyesha mtoto mara kwa mara wakati wote usiku na mchana
  • Endapo mama yupo mbali na mtoto akamue maziwa yake
  • Kunyonyesha mara kwa mara husaidia utengenezaji wa maziwa
 • Kuyonyesha mtoto kila wakati kadiri anavyohitaji
  • Kulia ni dalili ya mwisho ya njaa kwa mtoto
  • Dalili za awali za mtoto anayetaka kunyonya ni:
   • Kukosa utulivu
   • Kufungua kinywa na kugeuza geuza kichwa
   • Kutoa ulimi nje ya mdomo
   • Kunyonya vidole na ngumi
 • Acha mtoto anyonye na kumaliza maziwa yote kwenye titi moja na aachie mwenyewe kabla ya kumhamishia kwenye titi lingine.
  • Kumhamishia mtoto kwenye titi lingine kabla la kwanza halijaisha maziwa humzuia asipate maziwa yanayotoka mwisho yenye nishati lishe kwa wingi.
  • Maziwa yanayotoka mwanzo: Yana maji kwa wingi yanayosaidia kukata kiu ya mtoto
  • Maziwa yanayotoka mwisho: Yana mafuta kwa wingi yanayosaidia kumshibisha mtoto
 • Mpakate na kumweka mtoto vizuri kwenye titi Dalili za mtoto aliyepakatwa vizuri ni:
  • Mwili wa mtoto umenyooka, uso unaangalia titi
   • Tumbo la mtoto limegusana na tumbo la mama
   • Kichwa cha mtoto, mabega na miguu vimenyooka
   • Mama ameshika mwili wa mtoto (Kichwa cha mtoto kiwe kwenye kiwiko cha
   • mama na kiganja cha mama kishike makalio ya mtoto)
  • Dalili za mtoto aliyewekwa vizuri kwenye titi:
   • Mdomo wa mtoto umeachama vizuri
   • Kidevu cha mtoto kinagusa titi
   • Sehemu kubwa ya eneo jeusi inayozunguka titi inaonekana juu na siyo chini ya mdomo
   • Mdomo wa chini umebinuka kwa nje
   • Mtoto hasababishi maumivu kwa mama wakati anaponyonya

Faida za Unyonyeshaji

Unyonyeshaji unatoa faida kwa wote – mtoto na mama.

Faida kwa mtoto

 • Kupungua kwa uwezekano wa kupata tatizo la manjano
 • Kuboresha ukuaji na hali ya lishe ya mtoto
 • Kupungua kwa vifo vya watoto
 • Kuimarisha kingamwili ya mtoto
 • kupungua kwa maambukizi
 • Kupungua kwa magonjwa ya ngozi
 • kupungua kwa magonjwa ya mfumo wa njia ya chakula
 • Kupungua kwa magonjwa ya kuharisha
 • Kupungua kwa magonjwa ya mfumo wa njia ya hewa
 • Kuboresha mahusiano baina ya mama na mtoto
 • Kupungua kwa uwezekano wa magonjwa sugu (kisukari, magonjwa ya moyo, pumu na baadhi ya saratani)
 • Kupunguza uwezekano wa kuwa na uzito uliozidi au kiribatumbo
 • Kuboresha ukuaji wa kiakili na misuli

Faida kwa mama

Madhara ya ulishaji mbadala kwa watoto

Ulishaji Mbadala maana yake ni kumlisha mtoto vyakula au vinywaji vingine badala ya maziwa ya mama. Katika kipindi cha miezi 6 ya mwanzo ulishaji mbadala unaweza kusababisha athari nyingi za kifiziolojia na kisaikolojia kwa mama na mtoto.

Athari kwa mtoto ni:

Athari kwa mama

Kukabiliana na Imani Potofu na Changamoto za Unyonyeshaji

Baadhi ya imani potofu na changamoto za unyonyeshaji nipamoja na:

 • “Maziwa ya mama hayatoshi katika siku tatu za mwanzo baada ya kujifungua, na hata kidogo yanayotoka hayafai kumpa mtoto, inafaa kumpa mtoto asali, maji yenye sukari, au maziwa mbadala katika kipindi hiki.”
 • Wingi wa maziwa ya mama unategemea chakula na tabia za ulaji za mama, pia vyakula vingi huathiri afya ya mtoto. Kama mama anakula vyakula vya moto mtoto atapata tatizo la kuhara na kama mama atakula vyakula vya baridi, mtoto atapata tatizo la kukohoa.”
 • “Wakati anaponyonyeshwa, mtoto anahitaji maji ya nyongeza hususani hali ya hewa inapokuwa ya joto.”
 • “Kama mama ana matiti madogo, atatengeneza kiasi kidogo cha maziwa.”
 • “Kama mama amejifungua kwa njia ya upasuaji hatakiwi kumnyonyesha mtoto.”
 • “Mtoto anayeharisha asinyonyeshwe maziwa ya mama.”
 • “Mtoto mwenye umri wa miezi 3 anaweza kuachishwa kunyonya na kuanzishiwa vyakula mbadala ili mama yake arudi kazini.”

Vyanzo

https://www.tfnc.go.tz/publications/9

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi