KUOMBOLEZA: Sababu, dalili, matibabu

Maelezo ya jumla

Kuomboleza ni mwitikio anaokuwa nao mtu baada ya kupoteza/kuondokewa/kuachwa. Mara nyingi ni mwitikio wa huzuni na hisia za machungu.

Dalili za kuomboleza ni nini?

kuomboleza

Kuna hatua tano wakati wa kuomboleza. Hatua hizi sio lazima zitokee kwa mpangilio wa kufuatana, na wakati mwingine zinaweza kutokea/kumpata mtu kwa wakati mmoja. Sio kila mtu anapitia hatua hizi zote.

 1. Kukataa, kutokukubali, kufa ganzi (kwa mfano “haiwezekani jambo hili liwe hivi”
 2. Hasira, kuwalaumu wengine (kwa mfano “kama isingekuwa mama yangu nisinge…)
 3. Kuanza mazungumzo (kwa mfano “kama nikipona kansa hii, sitavuta tena sigara”)
 4. Hisia za huzuni, sonona, na kulia
 5. Kukubaliana, kuwa tayari na kinachokuja (kwa mfano ” kila mtu ana wakati wake, nadhani huu ndio mwisho wangu”)

Watu wanaoomboleza wanaweza kushtuka na kuanza kulia, wanaweza kupata shida kulala, na inaweza kuwa ngumu kufanya kazi

Ni nini husababisha kuomboleza?

Kuomboleza kunaweza kusababishwa na kifo cha mtu unayempenda. Watu wanaweza pia kuomboleza kama kuna mtu kwenye familia mwenye ugonjwa ambao hauna tiba, au ugonjwa sugu ambao unavuruga mfumo wao wa maisha. Mwisho au kukoma kwa mahusiano ya karibu kunaweza pia kusababisha mchakato wa kuomboleza.

Kila mtu anaomboleza kwa namna yake. Hata hivyo, kuna hatua zinazofanana tunazopitia sisi sote. Huanza kwa kutambua kwamba umepoteza/kuachwa/kuondokewa na kuendelea mpaka pale utakapokubalina hali hiyo. Mwitikio wakati wa kuomboleza unaweza kuwa tofauti kwa kila mtu, kulingana na mazingira ya kifo.

Kwa mfano, mtu ambaye amekufa kwa sababu ya ugonjwa sugu, kifo kinawezakuwa kimetarajiwa. Na kifo cha mtu aliyekuwa anaumwa ugonjwa mbaya linaweza pia kuwa jambo la kheri/kupumzisha. Kama kifo kilitokana na ajali au ugomvi, kufikia hatua ya kukubaliana na kifo inachukua muda mrefu zaidi.

Ni wakati gani unapaswa kutafuta usaidizi wa kitabibu?

Onana na daktari kama:

 • Kama unashindwa kudhibiti hisia za kuomboleza
 • Kama unatumia dawa nyingi zaidi au pombe nyingi zaidi wakati wa kuomboleza
 • Umekuwa na huzuni mwingi sana
 • Umekuwa na huzuni mwingi mpaka umeanza kuathiri utendaji kazi na maisha yako ya kila siku

Utambuzi

 • Daktari atafanya uchunguzi wa mwili na kukuuliza kuhusu dalili ulizo nazo, hii ni pamoja na usingizi na hamu ya kula.
 • Dalili zinazodumu kwa muda mrefu zinaweza kusababisha ugonjwa wa sonona

Uchaguzi wa matibabu|Kuomboleza

 • Wanafamilia wanaweza kutoa mchango wa kukutegemeza kihisia katika kipindi cha maombolezo.
 • Wakati mwingine mambo kadhaa yanaweza kuathiri mchakato wa kuomboleza, watu wanaweza kuhitaji msaada kutoka kwa:
  • Kanisani/msikitini/hekaluni
  • Mtaalamu wa afya ya akili
  • Makundi ya msaada binafsi
  • Ustawi wa jamii
 • Kipindi cha kikali cha maombolezo kwa kawaida kinadumu kwa miezi 2. Dalili nyepesi za kuomboleza zinaweza kudumu kwa mwaka mzima au zaidi.
 • Ushauri wa kisaikolojia unaweza kumsaidia mtu ambaye anashindwa kukubaliana na hali, au mwenye ugonjwa wa sonona.

Matarajio

Inaweza kuchukua mpaka mwaka au zaidi kushinda hisia kali za kuomboleza, na kukubaliana na hali.

Matatizo yanayoweza kutokea wakati wa kuomboleza

 • Kuomboleza kunaweza kuathiri afya yako kwa ujumla. Kunaweza kusababisha ugonjwa wa sonona au kujikuta unakuwa mlevi wa pombe au kutumia dawa za kulevya
 • Kuomboleza kunakodumu kwa zaidi ya miezi miwili na kunasababisha ushindwe kufanya kazi zako za kila siku, inaweza kuwa dalili ya ugonjwa wa sonona
 • Kutumia dawa kunaweza kusaidia.

Kuzuia

Kuomboleza  hakupaswi kuzuiwa kwa sababu ni mchakato mzuri kiafya wa kushughulika na kupoteza/kuachwa/kuondokewa. Mchakato huu unapaswa kuheshimiwa. Watu wanaoomboleza wanapaswa kutegemezwa wakati wanapopitia mchakato huu mgumu wa kuomboleza.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/bereavement.html

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi