KUONDOA SUGU KWENYE MIGUU AU MIKONO

KUONDOA SUGU KWENYE MIGUU AU MIKONO

 • January 21, 2021
 • 0 Likes
 • 159 Views
 • 0 Comments

Maelezo ya jumla

Kama kuna msuguano wa muda mrefu unaosababiswa na mgandamizo kwenye mikono au miguu kunatokea sugu ambayo inasababisha ngozi ya mahali hapo kuwa ngumu (calluses). Sugu zinaweza kutokea kwenye miguu kama unavaa viatu vinavyobana miguu au ambayo sole yake hailingani unapotembea na kwenye mikono kama unafanya kazi ngumu au kama unapiga kifaa cha mziki. Sugu huwa inatengenezeka ili kulinda ngozi laini ya ndani, kwa hiyo unaweza usihitaji kuzitoa kama haziumi.

Unapaswa kumwona daktari kama

Unapaswa kumwona daktari kama una sugu kwenye miguu au mikono na una ugonjwa wa kisukari au magonjwa mengine yanayopunguza mzunguko wa damu kwenda kwenye miguu

Unachoweza kufanya kuondoa sugu kwenye miguu au mikono

Corn pads

Kwanza unapaswa kutafuta nini sababu ya sugu, kwa sababu itakuwa rahisi kuzitibu kama kisababishi kitaondolewa. Unaweza kufanya mambo yafuatayo kupunguza sababu

 • Unaweza kutumia vifaa maalumu ambavyo vitasaidia kupunguza mkandamizo kwenye vidole, tumia corn pads (hivi ni vi-sponge vidogo kama ring) ambavyo vinapunguza mkandamizo kwenye sugu. Tumia corn and blister bandages ambazo huwa na kiwamboa ambacho kinakusanya unyevunyevu unatoka kwenye ngozi. Unyevu huu unatengeneza geli ambayo inapunguza mgandamizo lakini pia ina lainisha ngozi ya mahali penye sugu, ili iwe rahisi kuziondoa
 • Unaweza kuloweka sugu kwenye maji ya uvuguvugu, yenye sabuni kwa dakika 10 kila siku na kisha unaweza kutumia jiwe la kuogea kusugua taratibu ngozi ngumu itoke
 • Epuka kukata au kukwanyua sugu yako mwenyewe. Ila, unaweza kupaka salicylic acid ambayo inakuwa kwenye gel, lotion au mafuta ya kawaida, inasaidia kulainisha sugu na kuzifanya kuwa rahisi kuondolewa. Kuna baadhi ya bidhaa za salicylic ambazo zinaweza kuunguza ngozi inayozunguka kwa hyo kuwa makini na fuata maelekezo unapoipaka.

Kujikinga na sugu kwenye miguu au mikono

Unaweza kufanya mambo yafuatayo na yakapunguza makandamizo na msuguano kwenye miguu au mikono yako

 • Vaa viatu vinavyokutosha. Epuka viatu vyenye kisigino kirefu (heals) au viatu ambavyo vimechongoka. Hakikisha kuwa viatua ambavyo vimeharibika au kuisha, vimerekebishwa vizuri na haraka
 • Kama unyayo wako unapata sugu mara kwa mara, jaribu kutumia corn & blister bandages au unaweza kutumia sponge maalumu ili kupunguza mkandamizo ndani ya kiatu

  Corn babdage
 • Unaweza kutumia moisturizer mara kwa mara ili kulainisha ngozi, jipake water based creams au mafuta kwenye mikono na miguu baada ya shughuli
 • Vaa gloves nzito unapokuwa ukitumia mashine au kufanya kazi ngumu ya mikono
 • Kama unapiga kifaa cha mziki huwa inasaidia kufunga adhesive bandages kwenye vidole vyako, itakukinga

Mwone daktari kama

 • Kama haziondoki baada ya kujaribu mwenyewe kuziondoa
 • Kama ngozi inaanza kuwa na maumivu, nyekundu, iliovimba na inayotoa majimaji au kutengeneza kidonda

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/001232.htm

 • Share:

Leave Your Comment