KUONGEZEKA UZITO: Sababu na nini cha kufanya?

Maelezo ya jumla

Kuongezeka uzito ni hali ya kuongezeka uzito bila kuamua mwenyewe kufanya hivyo. Wakati wa ujauzito uzito wa mwili unaendelea kuongezeka, lakini pia unaweza kuongezeka uzito kipndi cha hedhi. Kuongezeka uzito haraka sana kunaweza kaushiria kuwa mwili unashidwa kutoa maji kutoka mwilini.

Ni nini husababisha kuongezeka uzito?upasuaji wa kupunguza uzito

Kuongezeka uzito kunaweza kusababishwa na sababu nyingi tofauti.

Kadri unavyoendelea kuongezeka umri, mchakato wa kimetaboliki unapungua kasi. Hii inaweza kusababisha uongezeke uzito kama unakula sana, unakula vyakula visivyo afya, au kama haupati mazozi ya kutosha.

Matatizo ya kitabibu au matumizi ya baadhi ya dawa yanaweza kusababisha kuongezeka uzito.

Dawa zinazoweza kusababisha kuongezeka uzito wa mwili ni pamoja na  “corticosteroids” na dawa zinazotumiwa kutibu magonjwa ya akili kama vile “bipolar disorder”, “schizophrenia”, na sonona.

Mabadiliko ya homoni yanaweza kutokea mwilini na kusababisha kuongezeka uzito. Mabadiliko haya yanaweza kusababishwa na:

 • Ugonjwa wa Cushing – cushing syndrome
 • Ugonjwa unatokana na kushindwa kwa tezi dundumio kutengeneza homoni zake – hypothyroidism
 • Ukomo wa hedhi

Kuvimba mwili kunakotokana na kujaa maji kwenye tishu za mwili kunaweza kusababisha kuongezeka uzito. Hii inaweza kutokea pamoja na hedhi, matatizo ya moyo, matatizo ya figo, kifafa cha mimba, au baadhi ya dawa.

Kama umeacha kuvuta sigara, unaweza kuongezeka uzito wa mwili. Watu wengi wanaoacha kuvuta sigara wanaongezeka kati ya kilo 2 – 4.5 ndani ya miezi 6 ya mwanzo baada ya kuacha. Baadhi wanaongezeka mpaka kilo 11 – 14. Ongezeko hili la uzito wa mwili halitokani tu na kula sana.

Ni wakati gani utafute msaada wa kitabibu?

Ni vizuri kuongea na daktari kama una dalili zifuatazo na uzito wa mwili unaongezeka:

 • Kufunga choo
 • Kuongezeka uzito wa mwili kulikopitiliza bila sababu ya msingi
 • Kupoteza/kupukutika/kuchomoka kwa nywele
 • Kuhisi baridi sana/ hauwezi kuhimili baridi
 • Kuvimba kwa miguu na unapata shida kupumua
 • Unahisi njaa kali inayoambatana na mapigo ya moyo kwenda mbio, kutetemeka kwa mikono na kutokwa jasho jingi
 • KUbadilika kwa uwezo wa kuona

Uchaguzi wa matibabu ya tatizo la kuongezeka uzitoKuongezeka uzito

Chakua hatua kwa kuanza kula mlo sahihi na mpango wa mzoezi ya mwili. Unaweza kuhitaji ushauri namna ya kufanya yote haya mawili. Weka malengo yaliyo na uhalisia yanayoweza kukusaidia kudhibiti ongezeko la uzito. Ongea na daktari anaweza kupendekeza baadhi ya maeneo ya kuboresha.

Matarajio

Daktari atafanya uchunguzi wa mwili, atakupima urefu na uzito wa mwili ili kupiga hesabu kujua uwiano wa uzito na urefu (Body mass index), na atakuuliza maswali kuhusu uzito wako wa mwili, kama vile:

 • Una wasiwasi, woga, au msongo mkubwa wa mawazo?
 • Je, uzito wa mwili umeongezeka haraka au taratibu?
 • Je, una historia ya kupata ugonjwa wa sonona?
 • Je, unatumia pmbe au dawa za kulevya?
 • Je, tatizo la kuongezeka uzito linakuwazisha sana?
 • Je, umepunguza kushiriki katika kazi za kijamii?
 • Je, uwezo wako wa kushughulisha mwili umepungua baada ya kupata ugonjwa au jeraha?
 • Je, kumekuwepo na mabadiliko katika mlo unaokula?
 • Umeongezeka uzito kiasi gani?
 • Unatumia dawa gani?
 • Je, una dali gani nyingine?
 • Je, kuongezeka uzito kumeanza lini?

Baadhi ya vipimo unavyoweza kufanya ni pamoja na:

 • Vipimo vya damu
 • Vipimo vya viwango vya homoni

Kuongezeka uzito kulikosababishwa na matatizo ya kihisia yanaweza kuhitaji kupewa ushauri nasaha. Ongea na daktari kuhusu mlo sahihi na mpango wa mazoezi wenye malengo halisia yanayoweza kukusaidia kupunguza uzito. Kama kuongezeka uzito kumesababishwa na ugonjwa, matibabu ya ugonjwa yatatolewa.

Kama kuongezeka uzito kutaendelea japokuwa unakula mlo sahihi na kufanya mazoezi, ongea na daktari kuhusu njia nyingine za kupunguza uzito, hii ni pamoja na dawa na upasuaji.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/003084.htm

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi