KUONGEZEWA DAMU

KUONGEZEWA DAMU

 • January 19, 2021
 • 0 Likes
 • 18 Views
 • 0 Comments

Maelezo ya jumla

Kuongezewa damu (blood transfusion) ni utaratibu wa kimatibabu wa kuwaongezea wahitaji damu iliyochangishwa toka kwa wadhamini wa kujitolea. Damu hii huingizwa mwilini kupitia kwenye mshipa wa mkono.

Utaratibu huu unaweza kuokoa maisha ya mtu aliyepoteza damu kwa sababu ya upasuaji au ajali. Kuongezewa damu kunaweza kusaidia pia kwa mgonjwa mwenye ugonjwa unaopunguza uzalishaji wa damu mwilini.

Mara nyingi hakuna matatizo yoyote yanayotokana na kuongezewa damu. Matatizo yanapotokea huwa ni ya kawaida tu yanayoweza kudhibitiwa.

Kwa nini uongezewe damu

Watu huongezewa damu kwa sababu mbalimbali, kama vile upasuaji, ajali, magonjwa au matatizo yanayosababisha kuvuja damu.

Damu imegawanyika katika sehemu kadhaa, hii ni pamoja na:

 • Seli nyekundu hubeba oksijeni na husaidia kuondoa taka mwilini
 • Seli nyeupe husaidia mwili wako kupambana/kudhibiti maambukizi
 • Plazima ni kimiminika au majimaji yanayounda damu
 • Chembe sahani husaidia damu kuganda vizuri

Kuongezewa damu hufanyika ili kukidhi mahitaji ya mwili wako. Daktari anaweza kuchagua kukuongezea sehemu moja tu ya damu unayoihitaji, mfano-seli nyekundu za damu au akachagua kukuongezea damu nzima yenye sehemu zote.

Kwa sasa watafiti wanajitahidi kutengeneza damu bandia ili kuwa mbadala wa damu lakini hilo halijawezekana bado.

Je, ni hatari?

Kuongezewa damu ni utaratibu salama, lakini kuna uwezekano wa matatizo kutokea. Matatizo yasiyo makali na kwa mara chache matatizo makubwa na hatari yanaweza kutokea wakati wa kupewa damu au siku kadhaa au zaidi baada ya kupewa damu.

Matatizo yanayoonekana zaidi ni pamoja na mzio unaoweza kusababisha vipele na kujikuna na homa.

Maambukizi ya damu

Benki za damu huchunguza na kufanyia vipimo damu zote za wafadhili kabla ya kutumika, kwa hiyo maambukizi kama Virusi vya ukimwi, homa ya ini B na C ni NADRA SANA.

Matatizo mengine hatari

Matatizo haya pia ni nadra sana, ni pamoja na:

 • Acute immune haemolytic reaction. Mfumo wako wa mwili hushambulia na kuharibu seli zote nyekundu ulizoongezewa kwa sababu damu yako na damu uliyoongezewa hazifanani. Seli hizi zilizoharika hutoa sumu fulani inayoweza kuharibu figo zako.
 • Delayed haemolytic reaction: Hii hufanana na acute haemolytic reaction lakini hutokea polepole zaidi. Inaweza kuchukua wiki moja mpaka 4 kugundua upungufu wa seli nyekundu mwilini. Uharibifu wa seli hufanyika taratibu
 • Graft-versus-host disease: Katika hali hii, seli nyeupe zilizo kwenye damu uliyoongezewa huanza kushambulia na kuharibu uboho wa mifupa yako. Hali hii mara nyingi husababisha kifo, na kwa mara nyingi huwapata watu wenye kinga hafifu ya mwili, kama vile wanaotibiwa saratani ya damu au lymphoma

Matayarisho kabla ya kuongezewa damu

Damu yako itapimwa kabla ya kuingiziwa damu ili kutambua kundi lako la damu A, B, AB au O na kama damu yako ni Rh Chanya (+) au Rh (-). Damu utakayoongezewa inapaswa kuendana na kundi la damu yako.

Mwambie mtumishi wa afya kama umewahi kupata tatizo lolote au mjibizo mbaya baada ya kuongezewa damu hapo zamani.

Utegemee nini

Utaratibu wa kuongezewa damu mara nyingi hufanyka hospitalini, kliniki au kwenye ofisi ya daktari. Utaratibuu kwa kawaida huchukua saa 1 mpaka masaa 4, kutegea na kiwango cha damu unapaswa kupewa.

Kabla ya kuongezewa damu

Kwa hali fulani unaweza kutoa damu yako ikatunzwa na baadae kuongezewa wakati wa upasuaji uliopangwa, lakini sehemu kubwa ya damu hupatikana kutoka kwa wadhamini.

Wakati wa kuongezewa damu

Sindano itaingizwa kwenye moja ya mishipa yako. Damu iliyochangishwa toka kwa wafadhili na kutunzwa kwenye mfuko maalumu huingizwa kwenye mishipa kupitia mrija maalumu ulioungwa kwenye sindano. Utakua umekaa au umelala wakati wa utaratibu huu, inaweza kuchukua saa 1 mpaka 4 hivi.

Muuguzi atafuatilia hali yako wakti wote wa utaratibu huu na atakupima shinikizo la damu, joto la mwili na mapigo ya moyo. MWAMBIE MUUGUZI KAMA:

Baada ya kuongezewa damu

Sindano na mrija wake itaondolewa. Damu inaweza kuvia eneo ulilochomwa sindano, lakini itaondoka baada ya siku kadhaa.

Mwone mtoa huduma ya kiafya kama unapata shida kupumua au maumivu ya kifua au mgongo baada tu au siku kadhaa baada ya kupewa damu.

Matokeo ya kuongezewa damu

Unaweza kuhitajika kufanya vipimo zaidi ili kuangalia jinsi mwili wako unavyoikubali damu uliyoongezewa na kuangalia kama kiasi kimeongezeka.

Hali fulani huhitaji mtu kuongezewa damu chupa zaidi ya moja ya damu

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/patientinstructions/000431.htm

 • Share:

Leave Your Comment