Last Updated on October 12, 2023 by Dr Mniko
Maelezo ya jumla
Kuota matiti kwa wanaume (Gynecomastia) ni tatizo la kuongezeka ukubwa wa matiti kwa wanaume. Kuongezeka kwa ukubwa wa matiti kunasababishwa na kuongezeka kwa kiwango cha homoni ya estrojeni (homoni ya kike) kuliko homoni ya testosteroni (homoni ya kiume) kwa wanaume. Hali hii mara nyingi inawapata zaidi watoto wachanga, kipindi cha balehe na wakati wa utu uzima na huwa tatizo hili linaisha jenyewe. Kuota matiti kwa wanaume mara nyingi hakuhitaji vipimo, lakini kiwango cha homoni katika damu, kipimo cha picha za ultrasound au mammogram kinaweza kufanyika kwa nyakati fulani ili kuhakikisha hakuna ugonjwa mwingine.
Ni nini dalili za kuota matiti kwa wanaume?
- Kuongezeka ukubwa wa matiti
- Maumivu ya matiti
Ni nini sababu za kuota matiti kwa wanaume?
- Wanaume wote na homoni za kiume na kike kwa kiwango fulani. Homoni za kiume zinasababisha mtu kuwa na tabia za kiume, kama vile kuta nywele mwilini, ukubwa misuli, na kuwa na sauti nzito. Homoni ya kike ya estrojeni husababisha tabia za kike.
- Mabadiliko katika kiwango cha homoni hizi, au mabadiliko kwa namna mwili unavyozitumia homoni hizi kunaweza kupelekea kuota matiti kwa wanaume.
Sababu za kawaida zaidi ni pamoja na:
- Mtoto mchanga
- Wakati wa balehe
- Kuzeeka
- Ugonjwa sugu wa ini
- Mtumizi ya dawa aina ya steroids kwa wajenga misuli
- Matumizi ya dawa zenye homoni ya estrojeni (homoni ya kike)
- Kushindwa kwa figo na kuchujwa damu kwa mashine – dialysis
- Kupungua kwa kiwango cha homoni ya testosteroni (homoni ya kiume)
- Matumizi ya bhangi
- Matumizi ya homoni kutibu saratani ya tezi dume
- Matumizi ya tibamionzi kutibu korodani
- Madhara mabaya yanayotokana na baadhi ya dawa (ketoconazole, spironolactone, cimetidine e.t.c)
- Tezi dundumio inayofanya kazi sana kuliko kawaida
Sababu nadra ni kama zifuatazo:
- Matatizo ya kijenetiki
- Uvimbe/kansa
Ishara zinazoashiria kuwa ni saratani ya matiti ni pamoja na
- Titi la upande mmoja pekee ndio huongezeka ukubwa
- Uvimbe wa titi unakuwa mgumu na unaweza kuwa umejishikiza kwenye tishu zinazouzunguka
- Kunakuwa na maumivu kwenye ngozi inayoufunika uvimbe
- Kunaweza kuwepo na damu inavuja kutoka kwenye chuchu
Ni wakati gani unapaswa kutafuta usaidizi wa kitabibu?
Ongea na daktari kama:
- Una uvimbe ulioanza hivi karibuni, unauma, au unazidi kuongezeka ukubwa kwenye titi moja au yote
- Kuna majimaji yenye rangi nzito au yenye dmu yanatoka kwenye chuchu
- Ngozi inayofunika uvimbe inauma au imetengeneza kidonda
- Uvimbe unaonekana mgumu ukiubonyeza
Uchaguzi wa matibabu ya tatizo la kuota matiti kwa wanaume
Kujihudumia nyumbani
- Weka kitambaa kilichochovywa kwenye maji ya barafu au tumia dawa za kupunguza maumivu kama ulivyoagizwa na daktari kama titi limevimba na linauma
- Acha kutumia dawa, kama vile bhangi.
- Acha kutumia virutubisho vyoyote unavyotumia au dawa zozote unazotumia bila maelekezo ya daktari
Nini cha kutegemea utakapokwenda kumwona daktari?
- Daktari atachukua historia ya kimatibabu na kufanya uchinguzi wa mwili
- Baadhi ya maswali utakayoulizwa ni pamoja na:
- Je, ni titi moja au yote mawili?
- Je, una umri gani?
- Je, unatumia dawa gani?
- Je, kuota matiti kwa wanaume kumekuwepo kwa muda gani?
- Je, matiti yaliyoota, yanaongezeka ukubwa, yanapungua au yamebaki vilevile?
- Je, kuna dalili nyingine zozote?
- Kufanya vipimo kunaweza kusiwe lazima, lakini vipimo vifuatavyo vinaweza kufanyika ili kutambua magonjwa kadhaa:
- Vipimo vya kiwango cha homoni kwenye damu
- Kipimo cha picha ya ultrasound ya matiti
- Kipimo cha kupima ufanyaji kazi wa figo na ini
Nini cha kufanya
- Kama kuna tatizo lililosababisha tatizo la kuota matiti kwa wnaume, linapaswa kutibiwa. Daktari atapaswa kuangalia dawa zote unazotumia kama zinaweza kuwa sababu ya shida hii. Kuota matiti kwa wanaume wakati balehe na wakati mtoto akiwa mchanga kunaisha kwenyewe baada ya muda.
- Matiti yanapoongezeka ukubwa na kuwa makubwa sana, yasiyolingana,na hayaishi yanaweza kumtia aibu kijana.
- Matibabu yanayoweza kutumika katika hali fulani ni pamoja na:
- Matibabu ya homoni zinazozuia kazi ya estrojeni
- Upasuaji wa kupunguza ukubwa wa matiti
Leave feedback about this