Last Updated on October 13, 2023 by Dr Mniko
Maelezo ya jumla
Kuota nywele nyingi kuliko kawaida (hirsutism) ni tatizo ambalo linaweza kuwapata watu wa jinsi zote mbili, lakini huwa linawaathiri zaidi wanawake. Baadhi ya wanawake kwa asili yao, wana nywele nyingi mwilini kuliko wengine na wanaweza kuwa na nywele ambazo hawazipendi au hawazitaki hasa usoni au wanaweza kuota nywele nyingi na nzito kwenye mikono, sehemu za siri, tumboni au kwenye mapaja. Kuota nywele nyingi kuliko kawaida pia kunaweza kutokea wakati wa ujauzito au baada ya damu ya hedhi kukata.
Kwa mara chache, unaweza kukuta tatizo hili limesababishwa na ugonjwa au dawa fulani alizotumia. Baadhi ya nywele zinaweza kuota kwenda ndani ya ngozi; unywele wakati wa kukua unajikunja na kuota kwenda ndani ya ngozi na kuvimba, mara nyingi shida hii huwa inatokea baada ya kukata vibaya au kutia vibaya unywele
Mwone daktari
Unapaswa kupanga kumwona daktari:
- Kama umegundua kuwa ghafla tu, hivi karibuni, wingi wa nywele zako za usoni au mwilini zimeanza kuongezeka sana na/au kama una dalili nyingine kama vile mzunguko wa damu ya hedhi unayobadilika badilika au kama unakosa kabisa damu ya hedhi, kama unaanza kuona sauti yako inaanza kuwa nzito (base) na uzito wako unaongezeka
- Kama unadhani kuwa ongezeko la nywele zako ni matokea ya dawa ambayo umeandikiwa na daktari
Unachoweza kufanya wewe mwenyewe baada ya kuota nywele
Kama ongezeko la nywele mwilini lina kukera, unaweza kujaribu njia zifuatazo ili kurejesha urembo ili ujisikie vizuri
- Kwa watu wenye ngozi nyeupe au ambayo sio nyeusi sana, wanaweza kutumia bidhaa za kubadili rangi ya nywele ili kuzifanya zisionekane sana (hair bleaches). Madawa ya kubadili rangi nywele yanaweza kuzifanya nywele zikafifia kidogo kufanana na ngozi, lakini kwa watu wenye ngozi yenye rangi nzito zinaweza zisisaidie.
- Kama unaota nywele ndani ya pua au kwenye kidevu unaweza kuzing’oa kwa kutumia tweezers, kuzing’oa kunasababisha zisiwahi kuota.
- Ni bora kunyoa, hasa kwenye maeneo makubwa kama vile miguu. Unaweza kutumia kifaa cha umeme kunyoa au kwa kutumia wembe na maji, wembe na maji hukatatia chini zaidi nywele. Utapaswa kunyoa nywele kila siku ili kuepuka vile vinywele vigumu vinavyotokea kama mtu hajanyoa kwa muda mrefu. Tofauti na imani za watu, kunyoa nywele hakusababishi ziote nyingi zaidi, kwa hiyo nyoa tu.
- Kama mbadala unaweza kutumia madawa yanayotumika kuondoa nywele (hair removal products). Yapo madawa ya kupaka kwenye sehemu yenye nywele yanaziyeyusha na inakuwa rahisi kuziondoa
- Njia nyingine ni Waxing, kutumia waxing ni njia madhubuti kabisa kama utaiweza. Ukitumia njia ya ku-wax unang’oa unywele mpaka mzizi wake, kwa hiyo inachukua mpaka wiki 4 kwa nywele kuota tena. Ila kama unaona ni ngumu kufanya waxing mwenyewe ni bora kuomba msaada wa mtaalamu wa urembo akusaidie. Ila kama utaweza kuhimili fuata njia zifuatazo:
- Kabla haujaanza ku-wax, nywele zinapaswa kuwa angalau 5mm kwa urefu na ngozi iwe safi, kavu na isiwe imepakwa ”cream” au mafuta yoyote.
- Kama wax inahitaji kupaswa (heated wax), angalia usiipashe sana, ikiwa ya moto sana itaunguza ngozi.
- Anza kwa kupaka wax taratibu kwenye eneo dogo lenye nywele linalopaswa kuondolewa nywele, paka kuelekea uelekeo wa nywele zinavyokua mf: kwenye mguu nywele zinakua kuelekea chini
- Baada ya kupaka, weka fabric stip (kitambaa cha waxing) juu ya eneo ulilopaka na kinyooshe kwenda chini. Kisha kivute kwa haraka (kwa mshtuo) huku ukiwa umeshikilia ngozi kwa kuikaza. Unapokuwa unavuta, vuta ukikinzana na uelekeo wa nywele mf: kwa nywele za miguu, vuta kuelekea juu kwa kushtua
- Endelea kupaka wax, kuweka kitambaa na kubandua haraka mpaka utakapoondoa nywele zote, kwenye maeneo korofi rudia mara nyingi zaidi.
- Baada ya nywele kuisha, epuka kuoga au kuogelea mpaka utakapoona wekundu wa ngozi umeisha
- Kwa unywele uliojikunja na kuota kwenda ndani ya ngozi, mara nyingi huwa unachomoka wenyewe kama ukiuacha ukue. Ila kama sivyo, unaweza kuchukua sindano ukajaribu kuuinua na kuuchomoa kutoka ndani. Kumbuka kusafisha sindano kwa kuiweka juu ya moto kabla ya kuitumia. Usinyoe nywele kabla uvimbe uliosababishwa na unywele uliojikunja kuisha.
Kama una shida ya kuota nywele, mwone daktari kama
Unapaswa kupanga kumwona daktari kama:
- Kama umegundua kuwa ghafla tu, kwa muda mfupi tu, wingi wa nywele za usoni au mwilini zimeanza kuongezeka sana na/au kama una dalili nyingine kama vile mzunguko wa damu ya hedhi unayobadilika badilika au kama unakosa kabisa damu ya hedhi, kama unaanza kuona sauti inaanza kuwa nzito ”base” na uzito unaongezeka
- Kama unadhani kuwa ongezeko la nywele zako ni matokea ya dawa ambayo umeandikiwa na daktari
Leave feedback about this