Masikio, pua, koo

KUPASUKAPASUKA KWA MIDOMO:Sababu,matibabu..

kupasukapasuka midomo

Last Updated on October 13, 2023 by Dr Mniko

Maelezo ya jumla

Kila mmoja wetu kwa wakati fulani anapatwa na tatizo hili la kukauka na kuchanika au kupasukapasuka kwa midomo. Midomo inaathiriwa kwa urahisi na mwanga wa jua, inakauka kwa urahisi sana wakati wa baridi na hali ya hewa yenye upepo au kama unakaa kwenye vyumba vinavyopashwa joto ‘’heated’’. Tatizo hili huwa linaongezeka zaidi kama una tabia ya kulamba lamba midomo kila mara.
Mazingira ya aina hii yanaweza kusababisha ngozi na kona za midomo kupasuka, ngozi inaweza kuwa na maumivu na unaweza kujihisi kama unaungua midomo unapokuwa unafungua mdomo. Wazee wenye meno bandia au vifaa vya meno visivyotunzwa vizuri au watoto ambao wanatokwa mate mengi, wako kwenye hatari zaidi ya kupata matatizo haya. Matatizo mengine kama vile upungufu wa damu yanaweza kuchangia kuleta tatizo hili. Kama una mzio uliotokana na vipodozi unavyotumia, inaweza kusababisha midomo yako kupasuka pia

Unachoweza kufanya wewe mwenyewe

Unahitaji siku chache tu za kuwa makini na kujitunza na tatizo la kukauka, kupasuka kwa midomo na matatizo mengi yanayoambatana nayo kuondoka.kupasukapasuka kwa midomo

  • Kama midomo yako inauma au imepasuka, ipake mafuta au unaweza ukanunua ‘’lip balm’’ kutoka duka la dawa maalumu kwa ajili ya kazi hii. Kabla hujatoka nje kwenda maeneo yenye baridi na upepo, paka mafuta kuzunguka midomo yako ili kuilinda.
  • Kama unahisi kuwa dalili zako za kupasuka au kuuma kwa midomo kunatokana na kutokuendana/ mzio wa vipodozi au vifaa unavyotumia. Tupa dawa za miswaki, vipodozi na bidhaa zote unzozitumia kwenye midomo. Kisha anza kutumia aina nyingine ya dawa ya mswaki na bidhaa nyingine za kupaka au kuweka kwenye midomo, kimoja baada ya kingine ili utambue ni bidhaa gani inasababisha matatizo.
  • Epuka kutumia vyakula vyenye asidi nyingi au vyakula vyenye pilipili au vinywaji vinavyoweza kuunguza ngozi ya midomo
  • Kunywa maji ya kutosha, angalau ‘’glass’’ 6-8 za maji kwa siku, hasa wakati wa joto kali
  • Epuka kulamba lamba midomo
  • Mwone daktari wa meno kama una matatizo ya meno, kwa mfano kama meno ya bandia yahakai ‘’fit’’ vizuri

Mwone daktari kama

Panga kumwona dakatari kama:

  • Eneo la ngozi linaloizunguka midomo linaanza kuwa jekundu na linaanza kulia au kutoa majimaji au kama kuna uchafu unatoka hapo
  • Hali ya ngozi iliyopasuka inazidi kuwa mbaya au unaona hata baada ya siku 10 hakuna maendeleo mazuri
  • Kama kona za midomo Zinapasuka pasuka kila mara

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/002036.htm

Leave feedback about this

  • Quality
  • Price
  • Service

PROS

+
Add Field

CONS

+
Add Field
Choose Image
Choose Video
X