KUPIMA UZITO NA KULINGANISHA NA UMRI

Kupima uzito na kulinganisha na umri

Kupima uzito na kulinganisha na umri – Kipimo hiki hutumika kutathmini hali ya lishe kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano. Ni muhimu kumpima mtoto angalau mara moja kila mwezi ili kuweza kupata mwelekeo na kasi ya ukuaji wa mtoto, hivyo kujua hali yake ya lishe . Kipimo hiki hutumika kwenye kliniki za watoto.Kupima uzito na kulinganisha na umri

Jinsi ya kutafsiri baada ya  kupima uzito na kulinganisha na umri  

Uzito wa mtoto hulinganishwa na umri wake kwa kutumia kadi ya mtoto ya kliniki ambayo ina rangi kuu nne zinazoashiria hali ya lishe ya mtoto. Rangi nyekundu huashiria hali duni ya lishe (utapiamlo mkali), kijivu huashiria uzito pungufu kulingana na umri wake (utapiamlo wa kadiri) na ile ya kijani huashiria hali nzuri ya lishe. Endapo mtoto yuko katika rangi nyeupe ina maana uzito wake umezidi.

Ni muhimu sana kuzingatia mwelekeo wa mstari wa ukuaji kwani watoto huongezeka uzito wanapokua; endapo uzito unapungua bila kujali mtoto yupo katika rangi ipi inaashiria kuna tatizo la kiafya au ulishaji duni. Fanya uchunguzi kulibaini mapema.

Iwapo mtoto ameongezeka hata kama yuko kwenye rangi nyekundi au kijivu, ni dalili nzuri hivyo mama/mlezi ampongezwe ili kumjengea kujiamini ili aendelee kufanya vizuri.

Hatua za kuchukua kufuatana na tafsiri ya vipimo

Rangi kwenye kadi Tafsiri Hatua za kuchukua

Nyekundu

Utapiamlo mkali

 Mzazi au mlezi apewe unasihi wa lishe wa jinsi ya kuboresha ulishaji wa mtoto wake. Afuatiliwe kwa karibu kuhusu matibabu na ulishaji

Kijivu Utapiamlo wa wastani  Mzazi au mlezi apewe unasihi wa lishe wa jinsi ya kuboresha ulishaji wa mtoto wake. Afuatiliwe kwa karibu kuhusu ulaji wake na kama ana maradhi atibiwe
Kijani Uzito unaofaa  Mama au mlezi apongezwe na kutiwa moyo. Mzazi au mlezi apewe unasihi wa lishe wa jinsi ya kuendelea kumlisha mtoto wake.
Nyeupe Uzito umezidi Jadili na mama/mlezi kuhusu ulishaji wa mtoto kwani hali hii humwongezea mtoto uwezekano wa kuwa na uzito mkubwa hata atakapokuwa mtu mzima na hivyo kumuweka katika hatari zaidi ya kupata magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza. Mtoto asinyimwe chakula bali kiasi na ubora viangaliwe.

Angalizo: Zingatia mwelekeo wa mstari wa ukuaji wa mtoto

Kumbuka:

Uzito wa mwili hutegemea kiasi na aina ya chakula unachokula; pamoja na shughuli unazofanya. Mara nyingi unene hutokana na kula chakula kingi kuliko mahitaji ya mwili na kutokufanya mazoezi.

Vyanzo

https://www.tfnc.go.tz/publications/9

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi