Macho

TATIZO LA UKAVU WA MACHO | KUPUNGUA KWA MACHOZI

Last Updated on October 13, 2023 by Dr Mniko

Maelezo ya jumla

Tatizo la ukavu wa macho / kupungua kwa machozi – macho yanaweza kuwa makavu unapokuwa hautengenezi machozi ya kutosha au kama machozi unayotengeneza hayalowanishi macho vizuri. Ukiwa na tatizo la kupungua kwa machozi unaweza kuhisi macho yanakwaruza, kunata na kama yana mchanga ndani. Mtu wa umri wowote anaweza kupatwa na hili tatizo, lakini watu wazima, hasa wanawake ambao damu imekata ”menopause” wanapatwa zaidi na tatizo hili. Mara nyingi hali hii inakuwa mbaya zaidi kama kuna upepo au kama hali ya hewa ni kavu sana, lakini pia kuogelea kwenye mabwawa yenye” chlorine” , kutumia kiyoyozi ”air conditioner” au kama unapasha joto nyumba hasa maeneo yanye baridi kali sana. Kisukari na baadhi ya madawa kama vile ”antihistamines”, zinaweza kusababisha kupungua kwa machozi na macho kuvimba

Kupungua kwa machozi – mwone daktari kama

Ukiwa na tatizo la kupungua kwa machozi, panga kumwona daktari ili aweze kutambua nini sababu ya tatizo lako

Unachoweza kufanya wewe mwenyewe

Unaweza kufuata hatua zifuatazo ili kupata nafuu

  • Fumba na kufumbua macho mara kwa mara. Hasa wakati ambao unaangalia au kushughulika na kazi aina fulani kwa muda mrefu. Pumzika mara kwa mara kama unatumia kompyuta kufanya kazi.
  • Unaweza kutumia machozi ya bandia kama hali hii haikutokei mara kwa mara ili kulowanisha macho. Machozi ya kutengenezwa ni matone au gel ambayo ina ”hydroxypropyl methylcellulose” ambayo inalowanisha macho na kupunguza usumbufu uliopo. Usivae ”Contact lens” unapotumia bidhaa hizi.

Kupungua kwa machozi

  • Unaweza kutumia mafuta maalumu ya kununua yanayotia utelezi kwenye macho (lubricating oitments) ili kulinda macho wakati wa usiku ukiwa umelala. Haya mafuta ya kulainisha unayaweka kabla ya kulala na yanalinda macho usiku mzima. Mafuta haya hayapendelewi sana mchana kwa sababu yanaweza kusababisha ikawa ngumu kuona vizuri. Ni vizuri kuongea na mfamasia apendekeze bidhaa inayofaa zaidi
  • Kwa wale wanaishi ndani ya vyumba vinavyopashwa, unaweza kuongeza unyevunyevu ndani kwa kutumia ”humidifier” au unaweza kuweka bakuli lenye maji karibu na ”radiator” ili kuongeza unyevu ndani ya nyumba
  • Kunywa maji angalau glasi 6-8 za maji. Ni vizuri kupunguza kiasi cha kahawa, chai na cola unachotumia, kwa sababu vinywaji hivi vyote vina ”caffeine” ambayo inasababisha maji mwilini kupungua
  • Vaa miwani ya kukinga macho unapokuwa unaogelea (swimming googles)
  • Epuka kukaa maeneo yenye moshi au maeneo yenye uchafuzi mkubwa wa hewa, inaweza kusumbua macho zaidi
  • Unaweza kuongeza viwambo maalumu kwenye miwani yako ili kukinga upepo kuingilia pembeni (glass side shields) hasa wakati wa upepo mkali

Jinsi ya kuweka dawa ndani ya jicho

Kama unatatizo la kupungua kwa machozi na unataka kuweka dawa ndani ya jicho, iweke kwenye sehemu ya ndani ya kope ya chini. Hakikisha kuwa sehemu ya mdomo wa chupa ya dawa haugusi jicho ili ibakie kuwa safi

Kupungua kwa machozi – tafuta usaidizi kama

Kama una tatizo la kupungua kwa machozi, panga kuonana na daktari kama:

  • Kama unashida ya macho kukaukakauka sana na unahisi karaha machoni
  • Kama unaona unazo dalili nyingine za nyongeza

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/000426.htm

Leave feedback about this

  • Quality
  • Price
  • Service

PROS

+
Add Field

CONS

+
Add Field
Choose Image
Choose Video
X