Kupungua kwa uwezo wa kuona na upofu ni nini?
Kupungua kwa uwezo wa kuona ni neno linalotumiwa kuwakilisha watu wenye tatizo la kupungua uoni au upofu. Watu wenye tatizo la kupungua kwa uwezo wa kuona ni wale ambao hawawezi kuona vizuri na hivyo kushindwa kufanya shughuli zao za kila siku.
Watu wenye upofu ni wale ambao uoni wao ni 20/200. Hii inamaanisha wanaona vitu vilivyo umbali wa futi 20 kama viko futi 200. Watu wenye tatizo la kupungua kwa uwezo wa kuona wanahitaji vifaa maalum ili kuwasaidia kufanya shughuli zao za kila siku. Kama tatizo lililosababisha uwezo wa kuona kupungua lisipotibiwa – upofu unaweza kutokea.
Ni nini husababisha tatizo la kupungua kwa uwezo wa kuona au upofu?
Baadhi ya mabadiliko katika uwezo wa kuona ni ya kawaida kama sehemu ya uzee, kama vile – kushindwa kuona vizuri vitu vilivyo karibu. Sababu nyingine za kawaida zinazoweza kusababisha tatizo la kupungua kwa uwezo wa kuona au upofu ni majeraha, maambukizi na mabadiliko kwenye jicho yanayotokana na magonjwa mengine. Sababu kubwa za kupungua kwa uwezo wa kuona na upofu kwa watu wenye umri wa miaka 40 na zaidi ni kama vile:
- Macular degeneration – mabadiliko yanayotokea kwenye sehemu ya nyuma ya jicho
- Glaukoma /presha ya jicho – kuongezeka kwa shinikizo / presha ndani ya majimaji ya jicho
- Mtoto wa jicho – huu ni ukungu unaotokea ndani ya lenzi ya jicho
- Uharibifu wa jicho unaotokana na ugonjwa wa kisukari – hii hutokea kunapokuwepo na mabadiliko kwenye sehemu ya nyuma ya jicho kunakosababishwa na kiwango kikubwa cha sukari
Nitajuaje kama uwezo wangu wa kuona unapungua?
Unaweza kujua kuwa una matatizo ya kupungua kwa uwezo wa kuona au upofu kama unapata shida kufanya shughuli zako za kila siku, kama vile kusoma, kuangalia television, kutia saini ya jina lako, kuandika, au kutembea unapopanda na kushuka ngazi. Unaweza kuanza kupata shida kuwatambua watu.
Ninaweza kufanya nini kama nina tatizo la kupungua kwa uwezo wa kuona au upofu
Unapaswa kumwona daktari kama unaona kupungua kwa uwezo wa kuona unakuzuia kufanya kazi za kila siku. Daktari atajaribu kutibu sababu inayosababisha uwezo wa kuona kupungua. Daktari anaweza pia kupendekeza daktari bingwa wa macho anayeweza kukuhudumia zaidi. Kwa wagonjwa wengi, watahitajika wataalamu kadhaa ili kudhibiti hali hii. Baadhi ya madaktari bingwa wanaoweza kuhusika kukutibu ni pamoja na:
- Daktari bingwa wa macho – ophthalmologist – atahusika kutibu matatizo na magonjwa mbalimbali ya macho yanayosababisha tatizo lako
- Daktari bibgwa wa uoni – optometrist – atahusika kuhakikisha uwezo wako wa kuona unaendelea kuwepo – anaweza pia kupendekea miwani itakayokufaa au vifaa vingine kama utavihitaji – vifaa kama vile vya kukuzia vitu, telescopes n.k
- Daktari bingwa wa mazoezi ya mwili – atasaidia kuweka sawa balance ya mwili na uwezo wa kutembea, na atakufundisha namna ya kutumia fimbo kama utaihitaji
- Daktari bingwa wa ukarabati wa shughuli kazi – occupational therapist – atakusaidia kuanza kufanya shughuli za kila siku na kukufundisha namna ya kutumia vifaa mbalimbali kwa msaada
- Mfanyakazi wa ustawi wa jamii – social worker – atasaidia kuhakikisha unadhibiti hisia zako baada ya kupoteza uwezo wako wa kuona
Angalizo
- Taarifa zilizotolewa katika ukurasa huu zimetoa muhtasari na zinaweza zisimfae kila mtu. Ongea na daktari ili kung’amua kama taarifa hizi zinakufaa na wewe au jaribu kutafuta habari zaidi kuhusu shida hii.
Leave feedback about this