MAMBO YA KUFANYA KUPUNGUZA MAUMIVU WAKATI WA HEDHI

Maelezo ya jumla

Maumivu wakati wa hedhi – wanawake wengi wanapata maumivu kwenye sehemu ya chini ya tumbo muda kidogo tu kabla au wakati hedhi inapoanza, maumivu yenyewe yanakuwa ya kunyonga. Baadhi ya wanawake pia wanapata maumivu ya kichwa, maumivu ya mgongo, kichefuchefu na hata kuhara. Msongo na wasiwasi mwingi unaweza kusababisha tatizo likawa kubwa zaidi. Maumivu wakati wa hedhi mara nyingi yanaathiri zaidi wasichana na vijana wadogo na mara nyingi yanapungua makali kadiri umri unapoongezeka au baada ya kujifungua mtoto. Mara nyingi huwa hakuna sababu ya hatari inayoyasababisha

Unapokuwa na maumivu wakati wa hedhi mwone daktari kama

 • Una maumivu sehemu ya chini ya tumbo na unatokwa damu ukeni na kuna uwezekano kuwa ulikuwa mjamzito

maumivu wakati wa hedhiUnachoweza kufanya kupunguza maumivu wakati wa hedhi

Karibu mara zote, unaweza kufanya mambo yafuatayo kujisaidia kwa njia mbalimbali nyumbani

 • Ili kupunguza maumivu ya tumbo na maumivu mengine mwilini, unaweza kutumia dawa ya ibuprofen, ibuprofen ni anti-inflammatory, na inasaidia kupunguza kunyonga kwa tumbo na kuvuja kwa damu. Kama unapata maumivu mara kwa mara, anza kutumia dawa hii mapema kabla haujaanza kutegemea kupata hedhi yako. Kama hauwezi kutumia ibuprofen kwa sababu yeyote, tumia acetaminophen
 • Unaweza pia kuchuakua maji ya moto ukayaweka kwenye chupa, kisha ukaiweka kwenye tumbo lako, itasaidia kupunguza maumivu
 • Fanya mazoezi, tembea taratibu, inaweza kuleta nafuu kwa sababu unaishtua misuli kutoa kemikali za asili ambazo zinapunguza maumivu zinazoitwa endorphins. Kama ukiendelea kufanya mazoezi kama kawaida yako ya kila siku, itasaidia kuzuia kabisa au kupunguza makali yake
 • Jaribu kuepuka msongo au shughuli ambazo unaona zinatakuelemea kimwili au kiakili
 • Ili kupunguza wasiwasi na mkazo wa misuli, jaribu kufanya mazoezi maalumu ya upumuaji na mazoezi ya kulegeza misuli (tutayaongelea haya hapo baadae)
 • Kutumia virutubisho vyenye magnesium, virutubisho hivi vinaweza kupunguza dalili hizi. Au kama mbadala, unaweza kula vyakula ambavyo vina madini haya, vyakula kama vile njugu karanga, mbegu na nafaka

Tafuta usaidizi wa daktari kama

 • Kama unapata damu yako katikati ya mzunguko wako wa damu
 • Kama maumivu yanaendelea baada ya hedhi yako kukoma au kama kuna uchafu wenye harufu mbaya unaotoka ukeni
 • Kama unapenda ku- discuss uwezekano wa kutumia dawa za kupanga uzazi, ambazo zinaweza kusaidia kupunguza maumivu yako
 • Kama njia zilizotolewa hapo juu hazikusaidii kupunguza maumivu

Kuzuia maumivu wakati wa hedhi:

 • Acha kuvuta sigara, unaweza kuzuia au kupunguza maumivu kama ukiacha kuvuta sigara. Hii ni kwa sababu uvutaji wa sigara umeonekana kuongeza muda na ukali wa maumivu ya tumbo wakati wa hedhi

Bonyeza hapa kwa maelezo zaidi

Vyanzo

https://medlineplus.gov/periodpain.html

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi