Last Updated on October 13, 2023 by Dr Mniko
Maelezo ya jumla
Kukosa usingizi ni tatizo kubwa kwa watu wengi, wegine wanashindwa kulala kabisa usiku au wanashtuka kutoka usingizini mapema sana na wanashindwa tena kupata usingizi. Watu wazima wanahitaji angalau masaa 7-8 ya usingizi kwa wastani, lakini ukweli ni kwamba kadri umri unavyoongezeka na uhitaji wa kulala unapungua, wazee huwa wanahitaji si zaidi ya masaa 5-6 ya usingizi. Kwa mara kadhaa, kutokulala hakutokusababishia matatizo, lakini unaweza kujihisi mchovu siku inayofuata.
Kutolala mara nyingi husababishwa na msongo wa mawazo, woga uliopitiliza au sonona na kunaweza kukuacha ukiwa mchovu, mgovi na hata ukashindwa ku-concentrate au kufikiria vizuri mambo. Unaweza kuanza kujihisi maumivu, kupata shida kupumua na hata kuhisi mwili unapata joto.
Kuna baadhi ya madawa pia yanasababisha hili tatizo
Kukosa usingizi -mwone daktari kama
- Unahisi kuwa una sonona au kushuka moyo
- Kama unadalili zozote mwilini zinazo kusababishia usilale
Mambo unayoweza kufanya kama unashindwa kulala/ kukosa usingizi
Kuna mambo kadhaa unayoweza kufanya kama una tatizo la kukosa usingizi ili iwe rahisi kwako kupata usingizi usiku
- Jaribu kuweka ratiba vizuri ili uweze kulala muda mmoja kila siku. Hata kama umechoka ni vizuri usilale mchana
- Usile chakula chochote kizito masaa 3 kabla ya kulala. Epuka kunywa kahawa, chai, vinywaji vya cola, pombe na kuvuta sigara.
- Kama una njaa, kula kitu chepesi, kula cookies au ndizi. Kunywa glass ya maziwa nusu saa kabla ya kulala
Unaweza pia kujaribu kufanya mambo yafuatayo
- Funga kazi zako/ acha kufanya kazi angalau saa 1 kabla ya muda wa kulala, soma kitabu au sikiliza mziki laini. Chumba chako jitahidi kisiwe na makelele, kiwe na giza na kisiwe na joto au baridi sana
- Kama haujaweza kusinzia baada ya dakika 30, amka, nenda chumba kingine na usome kitabu. Usiangalie TV
- Kama kichwa chako kinafikiria mambo mengi ambayo unatakiwa kuyafanya hapo kesho ukiamka, weka notepad karibu na kitanda chako na uyarekodi
Zipo tiba za asili ambazo unaweza kuzijaribu, zinaongeza uwezekano wa kupata usingizi kama una tatizo la kukosa usingizi
- Unaweza kutumia majani ya mrujuani (lavender), majani yake huwa yana harufu nzuri na ukiweka kidogo ndani ya mto wako wa kulalia itakusaidia kulala vizuri. Yapo pia mafuta ya mrujuani (lavender oil), ukiyanunua unaweza kuyanysa tu au ukayaweka kidogo kwenye maji ukayaoga kabla ya kulala
- Kama unajihisi umekakamaa na kazi zimekuzidi, fanya mazoezi ya ku-relax (nitayaongelea hivi karibu, endelea kuwa nasi), yafanye muda mfupi kabla ya muda wa kulala
- Unaweza pia kutumia dawa zinazoleta usingizi zinazopatikana kwenye maduka ya madawa (antihistamine i.e. diphenhydramine), madawa haya huwa yanaumika kukusaidia kulala kwa muda mfupi tu, si suluhisho la kudumu, kwa hiyo usizitegemee sana
Ni vizuri kuongea na daktari kama baada ua kujaibu njia hizi nilizozizungumza hapa na hazikukusaidia
Leave feedback about this