KUSHINDWA/KUPATA SHIDA KUMEZA:Sababu, dalili, matibabu

Maelezo ya jumla

Kushindwa/kupata shida kumeza ni hali ya kuhisi kama chakula kinakwama kwenye koo au eneo lolote kabla hakijafika tumboni. Kumeza kunahusisha kutafuna chakula na kukirudisha kwenye sehemu ya nyuma ya mdomo ili kukisafirisha kwenda kwenye umio. Umio ni bomba linalosafirisha chakula kwenda kwenye tumbo.

Ni zipi dalili za tatizo la Kushindwa/kupata shida kumeza?Kushindwa/kupata shida kumeza

Maumivu ya kifua, kujihisi kama chakula kinakwama kwenye koo, au kuhisi uzito au mkandamizo kwenye shingo au juu au chini kidogo mwa kifua, lakini pia:

Unaweza kupata tatizo la Kushidwa/kupata shida kumeza chakula au kinywaji, au aina fulani tu ya vyakula au vinywaji. Kupata shida kumeza vyakula vya moto au vya baridi, vikavu au mkate, nyama, au kuku inaweza kuwa dalili za mwoanz za matatizo ya Kushindwa/kupata shida kumeza.

Ni nini husababisha tatizo la Kushindwa/kupata shida kumeza?

Kumeza ni mchakato unaohusiha mambo mengi. Neva nyingi za mfumo wa fahamu hufanya kazi kwa pamoja kudhibiti misuli ya mdomo, koo na umio ili mchakato huu kufanikiwa. Kazi kubwa ya mchakato wa kumeza inafanyika bila wewe kufahamu.

Tatizo la ubongo au mfumo wa fahamu linaweza kuharibu mchakato huu wa udhibiti wa misuli ya mdomo na koo.

 • Tatizo kwenye ubongo linaweza kusababishwa na ugonjwa wa Parkinson, multiple sclerosis au kiharusi
 • Tatizo la mishipa ya fahamu linaweza kusababisha na majeraha ya uti wa mgongo, amyotrophic lateral sclerosis au myasthenia gravis

Msongo wa mawazo au woga uliopitiliza unaweza kusababisha baadhi ya watu kuhisi mkazo kwenye shingo au kuhisi kamakuna kitu kimeziba kooni.

Matatizo yanayoathiri umio yanaweza pia kusababisha tatizo la Kushindwa/kupata shida kumeza, hii ni pamoja na:

 • Kutengenezeka kwa mviringo “ring” karibu na umio linapokutana na tumbo – schatziki ring
 • Kukaza na kulegea kwa misuli ya umio
 • Saratani ya koo/ umio
 • Kuharibika au kushindwa kulegea kwa misuli ya ukanda unaofungia chakula kwenye tumbo baada ya kutoka kwenye umio – ukanda huu ukikaza unazuia chakula kutoka kwenye umio kwenda kwenye tumbo – achalasia
 • Kovu kwenye umio linalopunguza kipenyo. Kovu linaweza kutokana na mionzi, kemikali, dawa, kuvimba, vidonda au maambukizi
 • Kama kuna kitu kimekwama kwenye umio, kama vile kipande cha chakula
 • Uvimbe kwenye kifua unaobana umio

Utambuzi wa tatizo la kushindwa/kupata shida kumeza

Daktari anaweza kuagiza vipimo ili kutambua sababu ni nini, kama vile:

 • Kitu kinachoziba au kusababisha kipenyo cha umio kupungua
 • Matatizo ya misuli ya umio
 • Mabadiliko ya utando ute unaofunika sehemu ya ndani ya umio

Kipimo kinachoitwa “upper endoscopy”  mara nyingi hufanyika

 • Kamera ndogo iliyowekwa kwenye ukanda unaoweza kujikunja hutumika kumulika ndani ya umio ili daktari aweze kufanya uchunguzi mpaka kwenye tumbo
 • Utapewa dawa ya suingizi ili usihisi maumivu wakati wa kipimo hiki.

Vipimo vingine ni pamoja na:

 • Kipimo kinahohusisha kumeza tonge lililochovywa kwenye barium “barum swallow” – aina hii ya kipimo hufanyika ili kukagua kipenyo cha umio kwa kutumia eksirei.
 • Eksirei ya kifua
 • Kipimo cha kupima shinikizo la umio – esophageal manometry
 • Eksirei ya shingo

Vipimo vya damu vinaweza kuhitajika ili kutambua baadhi ya matatizo

yanaweza kusababisha tatizo la Kushidw a/kupata shida kumeza.

Ukiwa na tatizo la kushindwa/kupata shida kumeza, ni wakati gani unapaswa kumwona daktari?

Onana na daktar kama tatizo la kushindwa kuemza haliishi baada ya siku chache, au kama linakuja na kuondoka. Ongea na daktari haraka sana kama:

 • Una homa au unapata shida kupumua
 • Unapungua uzito wa mwili
 • Tatizo la Kushidwa/kupata shida kumeza linazidi kuwa baya zaidi
 • Unakohoa au kutapika damu
 • Una pumu inayozidi kuwa mbaya
 • Unahisi kama unapaliwa wakati au baada ya kula au kunywa

Uchaguzi wa matibabu ya tatizo la kushindwa/kupata shida kumeza

Matibabu ya tatizo la Kushidwa/kupata shida kumeza yanategemea sababu.

Ni muhimu kujifunza kula na  kunywa kwa usalama. Kukosea kumeza kunaweza kusababisha ukapaliwa au kuvuta chakula au kinywaji kwenda kwenye njia ya hewa. Hii inaweza kusababisha nyumonia (homa ya mapafu)

Kushughulikia tatizo la Kushidwa/kupata shida kumeza nyumbani ni hatua muhimu, lakini kama tatizo haliiishi

 • Daktari anaweza kukupatia mapendekezo ya kubadili mlo. Anaweza pia kukupatia kimiminika maalumu cha mlo ili kukuweka mwenye afya.
 • Unaweza kuhitaji kujifunza namna nzuri ya kutafuna na kumeza chakula

Dawa zinazoweza kutumika zinategemea sababu ya tatizo la kushindwa kumea, na zinaweza kujumuisha:

 • Dawa zinazosaidia kulegeza misuli ya umio. Hizi ni pamoja na “nitrate”, dawa hii inatumika kutibu shinikizo la juu la damu, na “dicyclomide”.
 • Sindazo za sumu ya botulinum “botox”
 • Dawa za kutibu kiungulia na kucheua/kubeua kwa asidi (GERD)
 • Dawa za kutibu matatizo ya woga na hofu iliozidi, kama ipo

Baadhi ya taratibu na njia za upasuaji zinazoweza kusaidia ni pamoja na:

 • Kwa kutumia kamera ndogo “upper endosopy”, dakatari anaweza kutambua na kupanua sehemu za umio zilizopungua kipenyo. Kwa baadhi ya watu, hii inapaswa kufanywa, na mara nyingi inafanyika mara kadhaa.
 • Saratani inaweza kutibiwa kwa upasuaji au mionzi. Kulegea kwa misuli au kukaza kwa misuli ya umio kunaweza kutibiwa kwa upasuaji
 • Kama dalili zako ni kali sana na unashindwa kabisa kula au kunywa, au kama unapaliwa au unapata homa ya mapafu (nyumonia), unaweza kuwekewa mrija wa kulishiwa.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/007543.htm

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi