KUSHINDWA/KUPATA SHIDA KUPUMUA:Sababu,dalili,matibabu

Maelezo ya jumla

Kushindwa/kupata shida kupumua ni hali ya kuhisi ugumu au kupata shida unapovuta pumzi au kujihisi kama vile hewa ahitoshi. Hakuna njia nzuri ya kuelezea hali ya kushidwa/kupata shida kupumua. Baadhi ya watu wanaweza kujihisi kukosa upepo baada ya kufanya mazozi kidogo tu (kwa mfano, kupanda ngazi), japo hawana tatizo lolote kiafya. Baadhi wanaweza kuwa na ugonjwa sugu wa mapafu, lakini wasipate shida yoyote wakati wa kupumua. Kukorota ni moja ya hali zinazoonesha kuwa una tatizo la kushidwa/kupata shida kupumua – unatoa sauti kali kama mluzi unapokuwa ukitoa hewa nje ya mapafu.

Ni nini husababisha tatizo la kushindwa/kupata shida kupumua?Kushindwa/kupata shida kupumua

Kushidwa/kupata shida kupumua kuna sababu nyingi:

 • Kuziba kwa njia ya hewa, puani, mdomoni au kooni kunaweza kusababisha kushidwa/kupata shida kupumua
 • Ugonjwa wa moyo unaweza sababisha kushidwa/kupata shida kupumua kama moyo unashindwa kusukuma damu ya kutosha kusambaza hewa ya oksijeni kwenye mwili. Kama ubongo, misuli, au viungi vingine vya mwili visipo pata aoksijeni ya kutosha, hali ya kushidwa/kupata shida kupumua hujitokeza.
 • Ugonjwa wa mapafu unaweza kusababisha kushidwa/kupata shida kupumua
 • Wakati mwingine, msongo wa mawazo, au hisia kali kama vile za woga zinaweza kusababisha kushidwa/kupata shida kupumua.

Matatizo yafuatayo yanaweza kusababisha kushidwa/kupata shida kupumua:

 • Matatizo ya mapafu:
  • Mabonge ya damu yaliyoziba mishipa ya ateri za mapafu – pulmonary embolism
  • Mkamba – bronchitis
  • Ugonjwa sugu unaosababishwa kuziba kwa njia ya hewa “Chronic obstructive disease”, pumu, na matatizo mengine sugu ya mapafu
  • Homa ya mapafu (nyumonia)
  • Kuongezeka kwa shinikizo la damu kwenye mishipa ya ateri za mapafu – pulmonary hypertension
 • Matatizo ya njia ya hewa:
  • Kuziba kwa njia ya hewa – kitu kimekwama na kuziba njia ya hewa
  • Kifaduro – croup
  • Kuvimba kwa kidaka tonge – epiglotitis
 • Matatizo kwenye moyo:
 • Matatizo mengine:
  • Mzio (kwa mfano fangasi, manyoya ya wanyama, au chamvua)
  • Kubanwa kifua
  • Vumbi kwenye mazingira
  • Kitambi
  • Mshtuko – panic attacks

Utambuzi wa Kushindwa/kupata shida kupumua 

Daktari atachukua historia ya kimatibabu na kufanya uchunguzi wa mwili.

Maswali uanyoweza kuulizwa

 • Je, Una tatizo la kushidwa/kupata shida kupumua?
 • Je, unatoa sauti au kukorota unapokuwa unapumua?
 • Je, unatumia nguvu nyingi ili kuvuta pumzi?
 • Je, tatizo hili limekuwepo na kuongezeka kwa wiki au miezi?
 • Je, tatizo hili limeanza hivi karibuni?
 • Je, kushidwa/kupata shida kupumua kumeanza kwa ghafla?
 • Je, kushidwa/kupata shida kupumua kumeanza taratibu?
 • Je, tatizo limeanza kidogo na linazidi kuongezeka kadri muda unavyokwenda?
 • Je, kuna mpangilio wowote wa tatizo hili? Shida inasumu kwa muda gani, na kila tukio linafanana na lililotangulia?
 • Je, kushidwa/kupata shida kupumua kumezidi zaidi hivi karibuni?
 • Je, tatizo la kushidwa/kupata shida kupumua linasababishwa uamke usiku?
 • Je, tatizo la kushidwa/kupata shida kupumua linabadilika kadri muda unavyokwenda?
 • Je, tatizo hili linatokea hata ukiwa umepumzika?
 • Je, kila tukio linadumu kwa muda gani?
 • Je, tatizo la kushidwa/kupata shida kupumua linazidi zaidi unapokuwa umelala chali?
 • Je, tatizo ni kubwa zidi unapobadilisha mkao wa mwili?
 • Je, kushidwa/kupata shida kupumua kumewahi kutokea ndani ya masaa 4 mpaka 6 baada ya kukutana na kitu ambacho unaweza kuwa na mzio nacho?
 • Je, kushidwa/kupata shida kupumua kunatokea pale tu unapokuwa unakorota?
 • Je, misuli ya kifua inaisgia ndani unapokuwa unavuta pumzi?
 • Je, ni dalili gani nyingine ulizonazo?

Uchunguzi wa mwili utajumuisha uchunguzi wa mapafu, moyo, na njia ya hewa.

Vipimo vya maabara hujumuisha vifuatavyo

 • Kuangalia kiwango cha oksijeni kwenye damu – pulse oximetry
 • Vipimo vya damu (hii ni pamoja na kipimo cha kuangalia kiwango cha gesi kwenye damu -ABG)
 • Eksirei ya kifua
 • Kipimo cha CT Scan ya kifua
 • Kipimo cha ECG
 • Kipimo cha Echocardiogram
 • Kipimo cha mazoezi
 • Kipimo cha kuangalia utendaji kazi wa mfumo wa upumuji

Uchaguzi wa matibabu wa tatizo la kushindwa/kupata shida kupumua

Kama kiwango cha oksijeni kwenye damu kiko chini zaidi ya inavyotakiwa, mgonjwa anaweza kuhitaji kuongezewa hewa. Kiwango kikubwa sana cha hewa ya oksijeni kunaweza kuleta madhara kea baadhi ya wagonjwa. Hata hivyo, sio kila mara utahitaji oksijeni kwa kila kisa.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/003075.htm

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi