Last Updated on October 13, 2023 by Dr Mniko
Maelezo ya jumla
Wanaume wengi huwa wanapata shida hii ya kushindwa kusimamisha uume kwa wakati fulani au wengine wanaweza kusimamisha ila baada ya muda uume unalala na hausimami tena. Sababu kubwa huwa ni msongo, uchovu, matumizi ya pombe kupita kiasi au ugonjwa wa hivi karibuni. Kama ukiamka asubuhi unakuta uume umesimama, basi kushindwa kusimamisha kwa siku moja sio swala linalopaswa kukutia wasiwasi. Tatizo la kudumu la kushindwa kusimamisha uume linaweza kusababishwa na ugonjwa kama vile kisukari na magonjwa mengine yanayoathiri mfumo wa kuzungusha damu mwilini au madawa, kama vile madawa ya kudhibiti shinikizo la juu la damu au madawa ya kudhibiti sonona. Tatizo hili pia linaweza kusababishwa na wasiwasi uliozidi kipimo au matatizo kwenye mahusiano. Kadri unavyoendelea kuzeeka, inaweza kuchukua muda mrefu zaidi uume kusimama na ukishasimama unakuwa hauna nguvu sana.
Ukiwa na tatizo la kushindwa kusimamisha uume mwone daktari kama
Panga kumwona daktari kama:
- Unashindwa kusimamisha uume mara kwa mara au kama unatumia madawa ambayo unadhani yanachangia kutokea kwa tatizo hili
Unachoweza kufanya wewe mwenyewe ukiwa na tatizo la kushindwa kusimamisha uume
Kuna baadhi ya mambo unayoweza kuyafanya yakakusaidia kuondokana na tatizo la kushindwa kusimamisha ambalo sio la kudumu
- Usijilaumu sana. Kama una msongo mkubwa wa mawazo au uchovu, kwa mfano, kwa sababu ya maswala ya pesa, kazi au ugonjwa, shughulika na matatizo yako kwanza.
- Kama upo kwenye mahusiano kwa muda mrefu ongea na mwenzi wako. Mwambie wasiwasi ulionao na kisha msaidiane kushughulika na tatizo kwa pamoja. Itasaidia kukupunguzia shinikizo linaloletwa na matarajio ya kufanya vizuri ukiwa kitandani. Kama wasiwasi wa kushindwa kusimamisha unakuelemea na unashinda kabisa kushughulika, jaribu njia zifuatazo ili kukusaidia kupunguza wasiwasi wakati wa tendo la ngono
- Unapokuwa na wasiwasi mwingi na ukawa unawaza kama utaweza kusimamisha uume wakati wa ngono, mawazo haya ya uoga yanaweza kusababisha ukashindwa kusimamisha japo hauna tatizo lolote. Moja ya njia nzuri za kupunguza wasiwasi ni kufanya mambo taratibu bila haraka.
- Punguza shinikizo kwa kufanya mambo taratibu. Wewe na mwenzio mnaweza kutomasana mwili taratibu, kila mtu kwa zamu yake. Mnapaswa kukubaliana kuwa kwa wakati huu, hakuna kugusa matiti au sehemu za siri. Hii itawasaidia wote wawili kujiachia.
- Baada ya kufanya mzunguko huo mara kadhaa, mnaweza kuruhusu kutomasa matiti na sehemu za siri pia, lakini mjizuie kuanza kufanya ngono kwanza.
- Endelea kutomasana mpaka mtakapoanza kuona uume umeanza kusimama tena na wote mpo tayari kwa ajili ya kushiriki ngono.
- Ili kupunguza wasiwasi, unaweza kujaribu kufanya mazoezi ya upumuaji ‘’deep breath exercise’’ na mbinu za kulegeza misuli ‘’muscle relaxation technique’’. KAMA UNAPENDA KUJIFUNZA KUHUSU NJIA HIZI BONYEZA HAPA
- Punguza kiwango cha pombe unachokunywa; au acha kabisa kunywa. Kunywa pombe kwa wingi kunaweza kusababisha kushindwa kusimamisha; Madawa ya kulevywa pia yanaweza kusababisha tatizo hili.
- Acha kuvuta sigara au punguza kuvuta sigara. Vijana wanaovuta sigara wanaongeza hatari mara 2 ya kupata matatizo ya kudumu ya kushindwa kusimamisha uume maishani.
Ukiwa na tatizo la kushindwa kusimamisha uume mwone daktari kama
Panga kumwona daktari kama:
- Njia hizi hazikusaidii, au kama unadhani kushindwa kusimamisha uume kumesababishwa na jeraha au ugonjwa
Leave feedback about this