KUSHUSHA KANDO/KUMWAGA NJE MBEGU KAMA NJIA YA KUPANGA UZAZI

Nini Maana ya Kushusha Kando / Kumwaga nje?

Kushusha kando au Kumwaga nje ni kitendo cha baadhi ya wanaume kuchomoa uume kutoka kwenye uke wa mwenza na kumwaga mbegu/manii nje mbali na uke wakati wa mshindo.

 • Pia inajulikana kama kukojoa nje, kumwaga nje na majina mengine.
 • Hufanya kazi kwa sababu; manii /vinyiriri humwagwa nje ya mwili wa mwanamke.

Mambo Muhimu kuhusu kushusha kando / kumwaga nje?

 • Inaweza kutumika katika kila hali. Inaweza kutumika kama njia ya msingi au na kinga.
 • Haihitaji vifaa na hakuna haja ya kwenda kliniki au kwenye duka la dawa.
 • Moja kati ya njia za kuzuia mimba zenye ufanisi kidogo. Hata hivyo, baadhi ya wanaume hutumia njia hii vizuri.
 • Hukuza ushiriki wa mwanaume na kuboresha mawasiliano kati ya wenza wawili.kumwaga nje

Kushusha kando /kumwaga nje kuna Ufanisi Kiasi Gani?

Ufanisi unategemea mtumiaji: Hatari ya kupata mimba ni kubwa zaidi kama mwanaume hatachomoa uume kutoka ukeni kabla hajamwaga manii kwa kila tendo la ngono.

 • Moja kati ya njia zenye ufanisi mdogo zaidi, kama haujaizoea.
 • Kwa kawaida, hutokea karibu mimba 27 kwa wanawake 100 ambao wenza wao hutumia njia ya kushusha kando kwa mwaka wa kwanza. Hii ina maana kuwa wanawake 73 kati ya kila 100 ambao wenzi wao hutumia njia ya kushusha kando hawatapata mimba.
 • Ikitumiwa kwa usahihi kwa kila tendo la ngono, kutakuwa na mimba 4 tu kwa wanawake 100 ambao wenza wao hutumia njia ya kushusha kando kwa mwaka wa kwanza.

Madhara, Faida Kiafya

Hakuna

Hatari za Kiafya

Haipunguzi uwezekano wa kupata magonjwa ya ngono

Nani Anaweza na Hawezi Kutumia Njia ya Kushusha Kando

Wanaume wote wanaweza kutumia njia ya kushusha kando. Hakuna hali yoyote ya kiafya inayoweza kuzuia kutumia njia hii.

kushusha kandoJinsi ya Kutumia Njia Hii

 • Mwanaume anapojisikia kuwa anakaribia kumwaga manii
 • Achomoe uume kutoka kwenye tupu ya mwanamke na kumwaga manii nje mbali na uke, ili kuhakikisha anamwaga mbegu za kiume mbali na uke.
 • Kama mwanaume amemwaga manii hivi karibuni
 • Kabla ya kufanya ngono tena, akojoe na kufuta ncha ya uume ili kuondoa manii yaliyobaki.

Ushauri Juu ya Namna ya Kutumia Njia Hii

 • Kujifunza matumizi sahihi inaweza kuchukua muda –Ni vizuri kutumia njia nyingine mpaka mwanaume atakapojisikia kuwa anaweza kutumia njia ya kushusha kando kwa usahihi kwa kila tendo la ngono.
 • Ili kupata kinga kubwa dhidi ya kupata mimba – Unashauriwa kutumia njia ya ziada au mbadala ya mpango wa uzazi,LAKINI, Wenza ambao wamekuwa wakitumia njia ya kushusha kando vizuri wasikatishwe tamaa ya kuendelea kuitumia
 • Baadhi ya wanaume wanaweza kuona ugumu kutumia njia ya kushusha kando – Wanaume ambao hawawezi kuhisi wakati wote wanapokaribia kumwaga manii AU wanaume wanaowahi kumwaga manii mapema kabla ya wakati

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/001946.htm

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi