Magonjwa ya akili

TATIZO LA KUTAPIKA WAKATI WA SAFARI

kutapika wakati wa safari

Last Updated on October 13, 2023 by Dr Mniko

Maelezo ya jumla

Kama una tatizo la kutapika wakati wa safari, utahisi kizunguzungu, kichefuchefu na wakati mwingine maumivu ya kichwa unapokuwa umekaa ndani ya gari, meli, garimoshi au ndege. Kama motokaa itaendele kutembea, hali inaweza kuzidi kuwa mbaya zaidi, na unaweza kuanza kutokwa jasho, kupumua haraka haraka na mwishoni unatapika. Tatizo la kutapika safarini linatokea kunapokuwepo na mkanganyiko wa taarifa zinazofika kwenye ubongo kutoka kwenye viungo vilivyo ndani ya sikio na taarifa kutoka kwenye macho. Viungo vingine vya mwili vinahisi umekaa, lakini macho yanaona unatembea, taarifa hizi mbili za uwiano zinauchanganya ubongo na kusababisha ujisikie vibaya. Baadhi ya watu wapo kwenye hatari kubwa zaidi ya kuwa na shida hii, wasiwasi kwa sehemu kubwa unachangia. Kwa ujumla watoto wanapatwa zaidi na tatizo hili kuliko  watu wazima

Unachoweza kufanya wewe mwenyewe kutapika wakati wa safari

Kuna baadhi ya mambo unayoweza kufanya ii kuzuia au kupunguza uwzekano wa kutapika wakati wa safari. Jipange kwa kutumia mbinu hizi kabla haujaanza safari

 • Kabla haujasafiri kula chakula chepesi. Usinywe pombe na kunywa vinywaji vyenye kaboni kama vile soda muda mfupi au wakati wa safari.
 • Unaweza kutumia dawa za kudhibiti kutapika wakati wa safari. Dawa hizi zina ‘’antihistamines’’ kama vile ‘’meclizine’’ au dimehydrinate’’, ambazo husaidia kupunguza dalili. Tumia dawa hizi muda mfupi kabla ya kuanza safari. Zinaweza kukufanya ukawa unasinziasinzia, kwa hiyo usiendeshe baada ya kuzitumia. Zinaweza pia kusababisha pombe kuongezeka au kukaa mwilini kwa muda mrefu, kwa hiyo usinywe pombe baada ya kuzitumia
 • Ukiwa ndani ya gari, ndege au garimoshi, chagula sehemu ya kuketi ambayo haina mitikisiko sana. Kama ni kwenye ndege kaa eneo la katikati ya ndege, kwenye dirisha ukiyaangalia mabawa ya ndege. Kwenye meli, kaa katikati au kaa sehemu ya wazi ya ndege ‘’on deck’’ kama unaweza. Kama uko sehemu ya chini au ndani ya chumba ‘’enclosed cabin’’, jaribu kulala kadri unavyoweza. Kwenye gari moshi ‘’train’’, kaa karibu na dirisha ukiangalia kule unakoelekea, usikae ukiangalia nyuma. Ndani ya gari, kaa kwenye kiti cha mbele.
 • Hakikisha unapata hewa safi. Epuka kukaa karibu na harufu kali au moshi wa sigara
 • Ndani au kwenye garimoshi, ukikaa uwe unaangalia anga au yaweke macho yawe yanaangalia ‘’focus’’ kitu kilicho mbali kwenye uelekeo wa safari yako. Epuka kusoma, kuandika au kuangalia chini.
 • Kula tangawizi ‘’ginger’’ itasaidia kupunguza kichefuchefu. Tangawizi inaweza kupunguza dalili za tatizo hili kwa baadhi ya watu. Kuwa na kipande cha tangawizi, tafuna kidogokidogo wakati wa safari au unaweza kunywa ‘’juice’’ ambayo umeiwekea nusu mpaka kijiko kimoja cha unga wa tangawizi. Watoto wapendelea kitafunwa ambacho kimewekewa tangawizi ‘’coockie’’
 • Kwa baadhi ya watu, wakisafiri usiku inasaidia kupunguza kutapika wakati wa safari, hasa kama msafiri atakuwa amelala kabisa
 • Kama wasiwasi unachangia kupata tatizo hili, unaweza kujaribu mazoezi ya upumuaji ambayo yanasaidia kupunguza wasiwasi. BONYEZA HAPA KUJIFUNZA MBINU HIZI
 • Kama mwanao anapata shida ya kutapika au kujihisi kuumwa wakati wa safari, unaweza kuongeza urefu wa kiti anachokaa ili aweze kuona nje kupitia dirishani. Jaribu kumsahaulisha mtoto kuwa yuko safarini, mwekee mziki anaopenda, mwekee kanda yenye hadithi anazopenda au fanya nae michezo ambayo inahusisha yeye kuangalia vitu vilivyo mbele kabla hamjavifikia.

Mwone daktari kama

Panga kumwona daktari kama:

Vyanzo

https://medlineplus.gov/motionsickness.html

Leave feedback about this

 • Quality
 • Price
 • Service

PROS

+
Add Field

CONS

+
Add Field
Choose Image
Choose Video
X