Masikio, pua, koo

KUTOBOKA/KUPASUKA KWA NGOMA YA SIKIO

kutoboka kwa ngoma ya sikio

Last Updated on October 12, 2023 by Dr Mniko

Maelezo ya jumla

Kutoboka/kupasuka kwa ngoma ya sikio ni kutokea kwa upenyo au tobo kwenye ngoma ya sikio, ngoma ya sikio hutenganisha sehemu ya nje na ya ndani ya sikio. Ngoma ya sikio inapoharibika uwezo wa kusikia unaweza kupungua.

Ni zipi dalili za Kutoboka/kupasuka kwa ngoma ya sikio?kutoboka kwa ngoma ya sikio

Maumivu ya sikio yanaweza kupungua mara tu baada ya Kutoboka/kupasuka kwa ngoma ya sikio. Baada ya Kutoboka/kupasuka kwa ngoma ya sikio unaweza kuwa na dalili zifuatazo:

  • Majimaji yanaweza kutoka kwenye sikio (majimaji yanaweza kama maji, usaha, au damu)
  • Kusikia kelele kwenye sikio – buzzzz
  • Maumivu ya sikio au kujisikia vibaya kwenye sikio
  • Uwezo wa kusikia unaweza kupungua kwenye sikio lililoathirika
  • Unaweza kupooza uso, au kuhisi kizunguzungu (kwa visa vyenye hali kali sana)

Ni nini sababu ya Kutoboka/kupasuka kwa ngoma ya sikio?

Maambukizi ya sikio yanaweza kusababisha Kutoboka/kupasuka kwa ngoma ya sikio, hasa kwa watoto. Maambukizi yanasababisha usaha au majimaji kujikusanya nyuma ya ngoma ya sikio. Kadri shinikizo linavyoongezeka, ngoma ya sikio inaweza kuchanika.

Kuharibika kwa ngoma ya sikio kunaweza kusababishwa na:

  • Kelele kali sana karibu na sikio, kama vile kupiga risasi karibu na sikio.
  • Mabadiliko ya ghafla ya shinikizo la hewa kwenye sikio, hii hutokea wakati wa kusafiri kwa ndege, unapozama kwenye kina kirefu cha maji, au unapoendesha gari milimani
  • Kuwepo kwa vitu vigeni kwenye sikio
  • Jeraha kwenye sikio (kwa mfano kupigwa kofi sikioni au mlipuko)
  • Kuingiza vidunde vya kusafishia masikio au kuingiza vitu masikioni

Utambuzi wa tatizo la kutoboka/kupasuka kwa ngoma ya sikioKutoboka/kupasuka kwa ngoma ya sikio

Daktari ataangalia ndani ya sikio kwa kutumia kifaa kinachoitwa otoscope. Kama kuna Kutoboka/kupasuka kwa ngoma ya sikio, daktari ataona tobo au upenyo, na anaweza kuona vimfupa vidogo vinavyatikana kwenye sehemu ya ndani ya sikio. Wakati mwingine, inaweza kuwa ngumu kwa daktari kuona ngoma ya sikio kwa sababu ya majimaji yanayotoka (usaha) kwenye sikio. Kipimo kinaweza kufanyika ili kuangalia ni kwa kiasi gani uwezo wa kusikia umepungua – audiology testing.

Ni wakati gani unapaswa kutafuta usaidizi wa kitabibu kama una tatizo la kutoboka/kupasuka kwa ngoma ya sikio?

Kama ukiona maumivu ya sikio yamepungua baada ya Kutoboka/kupasuka kwa ngoma ya sikio, unaweza kusubiri mpaka siku inayofuata kuonana na daktari.

Onana na daktari haraka sana kama baada ya Kutoboka/kupasuka kwa ngoma ya sikio:

  • Unasikia kizunguzungu
  • Una homa, unajihisi kuumwa, au unaona uwezo wa kusikia umepungua
  • Una maumivu makali sana au unasikia kelele kubwa sana kwenye masikio
  • Una kitu kwenye sikio ambacho kinashindwa kutoka
  • Una dalili zinazodumu kwa zaidi ya miezi 2 baada ya matibabu

Uchaguzi wa matibabu ya tatizo la kutoboka/kupasuka kwa ngoma ya sikio

Matibabu ya kitabibu

  • Kuweka kitu cha moto karibu na sikio husaidia kupunguza maumivu
  • Dawa za maumivu kama vile “ibuprofen” au “acetaminophen” husaidia kupunguza maumivu
  • Dawa za antibiotiki (dawa za kunywa au za kuweka kwenye sikio) hutumika kuzuia au kutibu maambukizi.
  • Weka sikio katika hali ya usafi na kavu wakati unapoendelea kupona
  • Weka pamba iliyoviringwa vizuri na kupaka mafuta kwenye sikio ili kuzuia maji kuingia wakati unaoga. Epuka kuogelea au kuweka kichwa ndani ya maji.
  • Wakati mwingine, daktari anaweza kuweka kiwambo juu ya ngoma ya sikio ili kuharakisha mchakato wa kupona

Upasuaji

  • Upasuaji wa kurekebisha ngoma ya sikio “tympanoplasty” unaweza kuhitajika, kama ngoma ya sikio isipoweza kupona yenyewe.

Kuzuia kutoboka/kupasuka kwa ngoma ya sikioKutoboka/kupasuka kwa ngoma ya sikio

Usiweke vitu kwenye sikio, hata kama unataka kulisafisha. Vitu vilivyoingia ndani ya sikio vinapaswa kuondolewa na daktari. Hakikisha unatibu maambukizi ya sikio mapema.

Matarajio

Tobo kwenye ngoma ya sikio mara nyingi hupona ndani ya miezi 2. Kupungua kwa uwezo wa kusikia huwa ni wa muda tu. Kwa nadra, matatizo mengine yanaweza kutokea, kama vile:

  • Ukiziwi wa kudumu
  • Kusambaa kwa maambukzi kwenda kwenye mfupa ulio nyuma ya sikio – mastoditis
  • Kupata tatizo la vertigo – tatizo hili husababisha kujisikia kizunguzungu na kukosa balance

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/001038.htm

Leave feedback about this

  • Quality
  • Price
  • Service

PROS

+
Add Field

CONS

+
Add Field
Choose Image
Choose Video
X