KUTOKWA | KUVUJA DAMU KUTOKA PUANI

KUTOKWA | KUVUJA DAMU KUTOKA PUANI

 • January 21, 2021
 • 1 Like
 • 57 Views
 • 0 Comments

Maelezo ya jumla

Kuvuja damu kutoka puani (Nosebleed) ni jambo la kawaida sana kwa watoto, lakini watu wazima pia wanapatwa na hii hali mara chache pia. Sababu za kawaida ni pamoja na kuchokonoa pua na kupuliza kwa nguvu pua hasa wakati wa kutoa makamasi, lakini mara nyingi kuvuja damu puani huwa kunaokea bila sababu ya msingi au inayoeleweka. Pua yako iko kwenye hatari zaidi ya kuvuja damu kama utando mwembamba unaofunika sehemu ya ndani ya pua utapata harara kwa sababu ya baridi au mzio., au kama umekuwa mkavu na kuanza kupasuka kwa sababu ya hali ya hewa iliyo kavu sana. Japo sehemu kubwa ya matukio ya kuvuja damu huleta karaha ya muda mfupi, lakini  kwa mara chache inaweza kuwa dalili ya tatizo kubwa lililojificho

Alama za hatari

Omba msaada wa daktari kama:

 • Kama unavuja damu saana
 • Kama umeumia kichwa au shingo
 • Kama unatapika damu ambayo ulikuwa umeimeza
 • Kama unatumia madawa kama Aspirin au madawa mengine yanasababisha damu yako kuwa nyepesi

Unachoweza kufanya kuzuia damu kutoka

Kuvuja da mu puani kunaweza kukutisha lakini ukweli ni kwamba ni rahisi sana kuzizuia zisiendelee kutoka na kuzuia pia zisijirudie. Kwa wazee, kuvuja damu kutoka puani kunaweza kuwa kugumu kidogo kudhibiti. Jaribu njia zifuatazo

Kudhibiti damu isiendelee kutoka

 • Kuwa mtulivu. Kama unamsaidia mtu mwingine, mhakikishie kuwa hali itakuwa shari.
 • Fuata hatua hizi ili kuzuia damu kuvuja . Njia hii itazuia damu kutoka baada ya kuitumia kwa dakika 5 – 10
 • Egemea kwenda mbele kidogo. Kama unajihisi kizunguzungu au kuzimia kaa chini na kisha egemea kwenda mbele
 • Finya sehemu laini ya mbele ya pua kwa dakika 5 mpaka 10. Pumua kupitia mdomoni
 • Kama kuvuja damu kutaendelea baada ya dakika 10. Finya tena kwa dakika 5 mpaka 10, kama bado haitasimama kutoka tafuta usaidizi wa kidaktari.

Baada ya damu kuacha kutoka

 • Jitahidi usipulize pua zako kwa agalau masaa 24 baada ya damu kuacha kuvuja. Jitahidi pia usichokonoe pua zako
 • Kama unatahisi unataka kupiga chafya fanya hivyo ukiwa umefungua mdomo
 • Epuka kunywa vinywaji vya moto au pombe au kuvuta sigara
 • Lala kichwa chako kikiwa kimenyanyuliwa kwa angalau mito 2 au 3
 • Epuka mazoezi magumu kwa agaau masaa 24 baada ya damu kuvuja kutoka puani
 • Kama unaishi kwenye chumba kinachopashwa, kwa wale wanoishi maeneo ya baridi, nasi tumia humidifier (vifaa vya kuongeza unyevu chumbani) au weka bakuli lenye maji karibu na radiator
 • Kama unavuja damu puani mara kwa mara kwa sababu ya kukauka na kuchanika kwa sehemu ya ndani ya pua yako, jaribu kupaka mafuta ndani ya pua (petrolium jelly) mara kadhaa kwa siku ili kulainisha na kukinga kiwambo laini kinachofunika pua yako. Au unaweza kutumia matone ya saline (saline nose drops) ili kuongeza unyevu ndani ya pua. Saline zinapatikana kwenye maduka ya dawa na ni salama kuyatumia hata kwa watoto. Kama pua zinakauka yatumie mara kadahaa kwa siku

Tafuta msaada wa daktari kama

 • Kama unavuja damu kutoka puani mara kwa mara
 • Kama unajihisi vibaya au hauko vizuri kwa ujumla
 • Kama unakuwa rahisi damu kuvia chini ya ngozi yako (bruise)

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/003106.htm

 • Share:

Leave Your Comment