Uzazi wa mpango

KUTUMIA KIBANDIKO CHENYE VICHOCHEO VIWILI KUPANGA UZAZI

Last Updated on October 13, 2023 by Dr Mniko

Kibandiko chenye vichocheo viwili ni Nini?

Kibandiko chenye vichocheo viwili ni Kiplastiki kidogo, chembamba, cha umbo la mraba kinachobandikwa mwilini.

 • Hutoa vichocheo viwili wakati wote – projestini na estrojeni, kama vilivyo vichocheo asilia vya projesteroni na estrojeni kwenye mwili wa mwanamke – moja kwa moja kupitia kwenye ngozi hadi kwenye mfumo wa damu.
 • Kibandiko kipya hubandikwa kila wiki kwa wiki 3, kisha hupitisha wiki moja bila kibandiko. Katika wiki hii ya nne mwanamke atapata hedhi.

Kimsingi hufanya kazi ya kuzuia kuruhusiwa kwa yai kutoka kwenye ovari (uovuleshaji)

Mambo Muhimu kuhusu kibandiko chenye vichocheo viwili

 • Inatakiwa kujibandika kibandiko kidogo kinachonata. Hubandikwa mwilini kila siku usiku na mchana. Kibandiko kipya hubandikwa kila wiki, kwa wiki 3, ikifuatiwa na wiki moja bila kibandiko.
 • Badili kila kibandiko kwa wakati ili kupata mafanikio makubwa zaidi.

Mabadiliko ya hedhi ni ya kawaida lakini hayana madhara. Kwa kawaida, hutokea kupata hedhi isiyotabirika kwa miezi michache ya mwanzo na kisha hedhi kidogo na kuendelea kupata hedhi ya mara kwa mara.kibandiko chenye vichocheo viwili

Kibandiko chenye vichocheo viwili kina Ufanisi Kiasi Gani?

Ufanisi hutegemea mtumiaji: Hatari ya kupata mimba ni kubwa zaidi wakati mwanamke anapochelewa kubadili kibandiko.

 • Njia ya kibandiko chenye vichocheo viwili ni mpya, na utafi ti kidogo sana umefanyika kuhusu ufanisi wake. Viwango vya ufanisi katika majaribio ya kitabibu ya kibandiko yanaonyesha kuwa kinaweza kufanya kazi kwa ufanisi zaidi kuliko Vidonge vyenye vichocheo viwili, jinsi inavyotumiwa zaidi na utumiaji mara kwa mara na kwa usahihi
 • Viwango vya mimba vinaweza kuwa vikubwa zaidi kidogo miongoni mwa wanawake wenye uzito wa 90 kg au zaidi.
 • Kupata tena uwezo wa kushika mimba baada ya kuacha kutumia kibandiko: Bila kuchelewa

Madhara, Faida Kiafya, na Hatari Kiafya

Madhara

Baadhi ya watumiaji wameripoti yafuatayo:

Kuwashwa, ngozi kuwa nyekundu, au inflamesheni ya uke

Faida na Hatari Zinazojulikana Kiafya

Tafiti za muda mrefu za kibandiko ni chache, lakini watafiti wanatarajia kuwa faida na hatari zake kiafya ni sawa na zile za Vidonge vyenye Vichocheo Viwili

Namna ya kutumia Kibandiko chenye vichocheo viwili

 • Kutoa kibandiko kutoka kwenye kifuko na kuondoa ganda
  • Unatakiwa kuchana kifuko kwa pembeni.
  • Kisha chomoa kibandiko na kuondoa ganda bila kugusa sehemu inayonata
 • Mahali na namna ya kubandika kibandiko
  • Unaweza kukibandika kwenye mkono, mgongoni, tumboni, au matakoni, popote ambapo ni safi na pakavu, lakini si kwenye matiti.
  • Gandamiza sehemu inayoganda, yenye dawa kwenye ngozi kwa sekunde 10. Apitishe kidole chake pembezoni ili kuhakikisha kinashika.
  • Kibandiko kitakaa hata wakati wa kazi, zoezi, kuogelea, na kuoga.
 • Lazima ubadili kibandiko kila wiki kwa wiki 3 mfululizo
  • Bandika kila kibandiko kipya katika siku zinazofanana za kila wiki – “siku ya kubadili kibandiko”. Kwa mfano, kama akibandika kibandiko siku ya Jumapili, vibandiko vyote vitabandikwa siku ya Jumapili.
  • Ili kuepuka kuwashwa, asiweke kibandiko kipya mahali kilipokuwa kibandiko alichokitoa.
 • Usibandike kibandiko wiki ya nne
  • Wiki hii hakika atapata hedhi
 • Baada ya wiki bila kibandiko kupita, bandike kibandiko kipya
 • Usitoke bila kubandika kibandiko kwa zaidi ya siku 7. Kufanya hivyo kunaleta hatari ya kupata mimba kibandiko chenye vichocheo viwili

Nini cha kufanya ukichelewa kuondoa au kubadili kibandiko chenye vichocheo viwili?

 • Umesahau kubandika kibandiko kipya mwanzoni mwa mzunguko wowote wa kibandiko (katika wiki ya kwanza)?
  • Bandika kibandiko kipya haraka iwezekanavyo.
  • Rekodi siku hii kama siku mpya ya kubadili kibandiko.
  • Tumia kinga kwa siku 7 za mwanzo za kutumia kibandiko.
  • Pia, kama kibandiko kipya kilichelewa kubandikwa kwa siku 3 au zaidi (kibandiko kiliachwa kwa siku 10 au zaidi mfululizo) na alifanya ngono bila kinga katika siku 5 zilizopita, fikiri kumeza vidonge vya dharura kuzuia mimba
 • Umesahau kubadili kibandiko katikati ya mzunguko wa kibandiko (katika wiki ya 2 au 3)?
  • Kama umechelewa kwa siku 1 au 2 (hadi saa 48):
   • Bandika kibandiko kipya mapema unapokumbuka
   • Endelea kubadili siku ile uliyokuwa ukibadili
   • Hakuna haja ya kutumia kinga
  • Kama umechelewa kwa zaidi ya siku 2 (zaidi ya saa 48):
   • Sitisha mzunguko huo na anza mzunguko mpya wa wiki 4 kwa kubandika kibandiko kipya mara moja.
   • Rekodi siku hii kama siku mpya ya kubadili kibandiko
   • Tumia kinga kwa siku 7 za mwanzo za kubadili kibandiko
  • Umesahau kuondoa kibandiko mwishoni mwa mzunguko wa kibandiko (wiki ya 4)?
   • Bandua kibandiko.
   • Anza mzunguko mwingine katika siku ya kawaida ya kubadili kibandiko.
   • Hakuna haja ya kutumia kinga

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/001946.htm

Leave feedback about this

 • Quality
 • Price
 • Service

PROS

+
Add Field

CONS

+
Add Field
Choose Image
Choose Video
X