Uzazi wa mpango

KUTUMIA KIFUNIKO CHA SEVIKSI (MLANGO WA KIZAZI) KUZUIA MIMBA

Last Updated on October 13, 2023 by Dr Mniko

Kifuniko cha Seviksi (mlango wa kizazi) ni Nini?

Kifuniko cha seviksi (mlango wa kizazi) ni kifuniko laini, kinene, cha mpira au plastiki ambacho hufunika vizuri seviksi.

  • Hupatikana katika ukubwa tofauti; Unahitaji kupimwa na mtoa huduma aliyepata mafunzo maalum ili kujua ni cha ukubwa gani kinakufaa.

Kifuniko cha shingo ya kizazi hufanya kazi kwa kuzuia mbegu za kiume zisiingie kwenye mji wa mimba; dawa za povu na jeli huua au kuzivunja nguvu mbegu za kiume. Kwa pamoja hufanya kazi ya kuzuia mbegu za kiume zisikutane na yai.kifuniko cha seviksi

Mambo Muhimu kufahamu kuhusu kifuniko cha seviksi

  • Kifuniko cha mlango wa kizazi huingizwa ukeni kabla ya ngono. Hufunika seviksi (mlango wa kizazi).
  • Inahitaji kutumiwa kwa usahihi kwa kila tendo la ngono ili kupata mafanikio makubwa zaidi.
  • Hutumiwa pamoja na dawa za povu na jeli ili kuongeza ufanisi.

Kifuniko cha mlango wa kizazi kina Ufanisi Kiasi Gani?

Ufanisi unategemea mtumiaji: Hatari ya kupata mimba ni kubwa zaidi iwapo kifuniko cha seviksi pamoja na dawa za povu na jeli hazitatumiwa kwa kila tendo la ngono.

  • Ni moja ya njia zenye ufanisi mdogo zaidi.
  • Kwa kawaida, hutokea karibu mimba 32 kwa wanawake 100 wanaotumia kifuniko cha seviksi (mlango wa kizazi) pamoja na dawa za povu na jeli kwa mwaka wa kwanza. Hii ina maana kuwa wanawake 68 kati ya kila 100 wanaotumia kifuniko cha seviksi (mlango wa kizazi) hawatapata mimba.
  • Kikitumiwa kwa usahihi kwa kila tendo la ngono, kutakuwa na karibu mimba 20 kwa wanawake 100 wanaotumia kifuniko kwa mwaka wa kwanza.

Uwezo wa kushika mimba baada ya kuacha kutumia kifuniko cha seviksi (mlango wa kizazi): Bila kuchelewa.

Kinga dhidi ya magonjwa ya ngono: Hakuna

Madhara, Faida za Kifya na Hatari Kiafya

Madhara

Baadhi ya watumiaji wameripoti yafuatayo:

  • Kuwashwa ndani au kuzunguka uke au uume
  • Vidonda ukeni

Faida Kiafya Zinazojulikana za kutumia kifuniko cha seviksi

Husaidia kuzuia:

Matumizi ya kifuniko cha seviksi (mlango wa kizazi)

Namna ya Kuingiza

  • Jaza theluthi moja ya kifuniko kwa malai, jeli, au povu la dawa.
  • Sukuma kingo za kifuniko kuzunguka mlango wa kizazi mpaka ifunikwe kabisa, kwa kusukuma taratibu kichwani ili kufanya kiweze kunyonya na kuziba.
  • Ingiza kifuniko cha seviksi wakati wowote hadi saa 42 kabla ya ngono.

Namna ya Kutoa

  • Aache kifuniko ndani kwa angalau saa 6 baada ya mwenza wake kukojoa, lakini isizidi saa 48 kutoka wakati kilipoingizwa.
  • Kuacha kifuniko kwa zaidi ya saa 48 kunaweza kusababisha madhara ya sumu na kusababisha harufu mbaya na uke kutoa uchafu.
  • Chomoa kingo za kifuniko ili kuondoa lakiri ya seviksi (mlango wa kizazi), kisha vuta kifuniko kwenda chini hadi nje ya uke

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/001946.htm

Leave feedback about this

  • Quality
  • Price
  • Service

PROS

+
Add Field

CONS

+
Add Field
Choose Image
Choose Video
X