KUTUMIA KIWAMBO/ VIWAMBO KUPANGA UZAZI

Kiwambo ni nini?

Kiwambo ni kifuniko cha mpira kinachofunika seviksi. Viwambo vya plastiki vinaweza pia kupatikana.

 • Ukingo wake una springi imara, inayonyumbulika ambayo hukifanya kiwambo kikae mahali pake.
 • Hutumiwa na krimu, jeli, au povu la dawa ya kuua mbegu za kiume ili kuongeza ufanisi.
 • Vinapatikana katika ukubwa tofauti na kwa mara ya kwanza vinatakiwa kuingizwa na mtoa huduma aliyepata mafunzo maalum ili kuchagua kukuchagulia ukubwa wa kiwambo kinachotoshea vizuri.

Hufanya kazi kwa kuzuia mbegu za kiume zisiingie kwenye seviksi; dawa za povu na jeli huua au kuzivunja nguvu mbegu za kiume. Kwa pamoja zinazuia mbegu za kiume zisikutane na yai.

Mambo Muhimu kuhusu kiwambo

 • Kiwambo huingizwa ndani ya uke kabla ya kufanya ngono. Hufunika seviksi. Dawa za povu na jeli hutoa kinga ya ziada kuzuia mimba.
 • Inatakiwa kufanya uchunguzi wa nyonga kabla ya kuanza kutumia. Mtoa huduma lazima achague kiwambo kinachomwenea vizuri.
 • Kinahitaji kutumiwa kwa usahihi kwa kila tendo la ngono ili kupata mafanikio makubwa zaidi.

Kiwambo kina Ufanisi Kiasi Gani?

Ufanisi unategemea mtumiaji: Hatari ya kupata mimba ni kubwa zaidi kama kiwambo na dawa ya povu na jeli haikutumiwa kwa kila tendo la ngono.

 • Kwa kawaida, karibu mimba 16 hutokea kwa wanawake 100 wanaotumia kiwambo na dawa ya povu na jeli kwa mwaka wa kwanza. Hii ina maana kuwa wanawake 84 kati ya kila 100 wanaotumia kiwambo hawatapata mimba.
 • Vikitumiwa kwa usahihi kwa kila tendo la ngono, karibu mimba 6 zinaweza kutokea kwa kila wanawake 100 wanaotumia kiwambo na dawa ya povu na jeli kwa mwaka wa kwanza.

Kuweza kushika mimba baada ya kuacha kutumia kiwambo: Bila kuchelewa

Kuzuia magonjwa ya ngono: Kinaweza kusaidia kuzuia baadhi ya magonjwa ya ngono lakini kisitegemewe kuzuia magonjwa haya

Madhara, Faida Kiafya, na Hatari Kiafya viwambo

Madhara

Baadhi ya watumiaji wameripoti yafuatayo:

 • Kuwashwa ndani au kuzunguka uke au uume
 • Vidonda ukeni

Faida Kiafya Zinazojulikana

Husaidia kuzuia:

Dalili za saratani na saratani ya seviksi

Kuweka Sawa Mambo Yaliyoeleweka Vibaya kuhusu kiwambo

Viwambo:

 • Haviathiri hamu ya ngono. Wanaume wachache wameripoti kugusa kiwambo wakati wa ngono, lakini wengi hawajagusa.
 • Haviwezi kupita kuvuka seviksi. Haviwezi kwenda kwenye uterasi au vinginevyo kupotelea kwenye mwili wa mwanamke
 • Havisababishi saratani ya shingo ya mlango wa kizazi

Kwanini Baadhi ya Wanawake Wanasema Wanapenda Kiwambo

 • Kinadhibitiwa na mwanamke
 • Hakina madhara ya kichocheo

Kinaweza kuwekwa mapema kabla ya wakati wa tendo na hakivurugi ngonokiwambo

Hatua 5 za Msingi za Kutumia Kiwambo

Kama ni mara yako ya kwanza kutumia kiwambo, mtaalamu wa afya atakufanyia uchunguzi na kukuchagulia kiwambo kinachoenea vizuri kufunika mlango wa kikazi. Kisha atakufundisha namna ya kutumia kiwambo.

 1. Bonyeza krimu, jeli, au povu la dawa kujaa kijiko kwenye kiwambo na kuzunguka ukingo wake
  • Safisha mikono kwa sabuni laini na maji safi , ikiwezekana.
  • Kagua kiwambo kuona kama hakina matundu, mipasuko au michaniko kwa kukielekeza kwenye mwanga.
  • Angalia tarehe ya mwisho wa kutumia dawa ya povu na jeli na epuka kutumia baada ya muda kwisha.
  • Ingiza kiwambo chini ya saa 6 kabla ya kufanya ngono.
 1. Bonyeza kingo pamoja; ingiza kwenye uke mpaka kitakapoweza kufika.
  • Chagua mkao ambao hausumbui uwekaji – kuchuchumaa, kunyanyua mguu mmoja, kukaa au kulala
 1. Gusa kiwambo ili kuhakikisha kinafunika seviksi
  • Kupitia kuba ya kiwambo, seviksi inaonekana kama ncha ya pua.

Iwapo utajisikia vibaya baada ya kuweka kiwambo, kitoe na kiingize tena

 1. Kiache ndani ya uke angalau kwa saa sita baada ya kufanya ngono.
  • Kiache kiwambo ndani ya uke kwa angalau saa 6 baada ya kufanya ngono lakini si zaidi ya saa 24.
  • Ukiacha kiwambo ndani ya uke kwa zaidi ya siku moja unaweza kuongeza hatari ya athari ya sumu. Pia kinaweza kusababisha harufu mbaya na kutoka uchafu ukeni. (Harufu mbaya na uchafu hutoka wenyewe baada ya kiwambo kutolewa).

Ukifanya ngono mara kadhaa, hakikisha kuwa kiwambo kipo mahali sahihi na pia ingiza dawa ya povu na jeli zaidi mbele ya kiwambo kabla ya kila tendo la ngonoviwambo

 1. Ili kuondoa, peleka kidole kwenye ukingo wa kiwambo ukivute na kukitoa
  • Safisha mikono kwa sabuni laini na maji safi , ikiwezekana.
  • Ingiza kidole kwenye uke mpaka uguse ukingo wa kiwambo.
  • Sogeza taratibu kidole kwenye ukingo na vuta kiwambo na kichomoe. Kuwa makini usichane kiwambo kwa kucha.
  • Safisha kiwambo kwa sabuni laini na maji safi na kikaushe kila baada kukitumia

Vidokezo kwa Watumiaji wa Dawa ya Povu na Jeli au Viwambo vyenye Dawa Povu na Jeli

 • Dawa ya povu na jeli ihifadhiwe mahali baridi na pakavu, ikiwezekana, pasipokuwa na jua. Sapozitori zinaweza kuyeyuka kwenye hali ya joto. Zikihifadhiwa na ukavu, tembe zinazotoa povu haziwezi kuyeyuka kwenye hali ya joto.
 • Kiwambo kihifadhiwe mahali pasipo na joto, pakavu, ikiwezekana.

Atahitaji kupimishwa kiwambo kipya kama amejifungua au mimba ya miezi mitatu ya pili imetoka au kuharibika.kiwambo

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/001946.htm

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi