Njia ya Kunyonyesha Maziwa ya Mama ni Nini?
Njia ya kunyonyesha maziwa ya mama ni njia ya muda ya uzazi wa mpango inayotegemea athari za asili za kunyonyesha maziwa ya mama kuzuia mimba.
- Njia ya Kuzuia Mimba kwa Kunyonyesha Maziwa ya Mama inahitaji masharti matatu. Masharti yote matatu lazima yatimizwe:
-
- Mama bado hajaanza kupata hedhi.
- Mtoto ananyonyeshwa maziwa wakati wote au karibu wakati wote na ananyonyeshwa mara kwa mara, mchana na usiku.
- Mtoto ana umri chini ya miezi sita.
- “Kunyonyesha wakati wote” ni pamoja na kunyonyesha maziwa ya mama tu (kichanga hakipati aina nyingine ya maji au chakula, hapati hata maji, zaidi ya maziwa ya mama) na kunyonyesha karibu maziwa ya mama tu (mtoto anapata vitamini, maji, maji ya matunda, au virutubisho vingine mara moja wakati fulani kwa kujazia maziwa ya mama).
- “Kunyonyesha karibu wakati wote” ina maana kuwa mtoto anapata maji au chakula zaidi ya maziwa ya mama, lakini sehemu kubwa ya chakula (zaidi ya mara tatu au nne ya chakula chote) ni maziwa ya mama.
Hufanya kazi kimsingi kwa kuzuia yai kupevuka na kuondoka kwenye ovari (uovuleshaji).
Mambo Muhimu kuhusu njia ya kunyonyesha
- Njia ya mpango wa uzazi inayotegemea kunyonyesha. Huzuia mimba kwa mama na kutoa lishe bora kwa mtoto.
- Inaweza kufanya kazi vizuri hadi miezi sita baada ya kujifungua, alimradi iwe hajaanza kupata hedhi na mwanamke ananyonyesha wakati wote au karibu wakati wote.
- Inahitaji kunyonyesha mara kwa mara, mchana na usiku. Karibu mlo wote wa mtoto uwe maziwa ya mama.
- Hutoa fursa ya kumpatia mwanamke njia endelevu ambayo anaweza kuendelea kutumia baada ya miezi 6.
Njia ya kunyonyesha ina Ufanisi Kiasi Gani?
Ufanisi unategemea mtumiaji: Hatari ya mimba ni kubwa zaidi wakati mwanamke akiwa hawezi kumnyonyesha wakati wote au karibu wakati wote mtoto wake.
- Kama ilivyo, hutokea karibu mimba 2 kwa wanawake 100 wanaotumia njia ya kunyonyesha katika miezi sita baada ya kujifungua. Hii ina maana kuwa wanawake 98 katika kila 100 wanaotegemea njia hii hawatapata mimba.
- Ikitumiwa kwa usahihi, kutakuwa na chini ya mimba 1 kwa wanawake 100 wanaotumia njia hii katika miezi 6 ya mwanzo baada ya kujifungua.
Kuweza kushika mimba baada ya kuacha kunyonyesha: Inategemea mwanamke ameendelea kwa muda gani kunyonyesha.
Madhara, Faida Kiafya, na Hatari Kiafya
Madhara
Hakuna: Matatizo yote yanalingana na ya wanawake wengine wanaonyonyesha
Faida Kiafya Zinazojulikana
Husaidia kuzuia: Hatari ya kupata mimba
Hatari za Kiafya Zinazojulikana
Hakuna
Kwanini Baadhi ya Wanawake Wanasema Wanapenda Njia ya Kunyonyesha
- Ni njia ya asili ya uzazi wa mpango
- Inasaidia kunyonyesha maziwa kwa wingi, inaleta faida kiafya kwa mtoto na mama
- Haina gharama za moja kwa moja za mpango wa uzazi au kumlisha mtoto
Njia ya Kunyonyesha kwa Wanawake Wenye VVU
- Wanawake ambao wameambukizwa VVU au ambao wana UKIMWI wanaweza kutumia njia ya kunyonyesha. Kunyonyesha maziwa ya mama hakutafanya hali yao iwe mbaya. Hata hivyo, kuna uwezekano wa mama mwenye VVU kumwambukiza mtoto wake VVU kupitia kunyonyesha maziwa ya mama. Kwa kuwa kwa ujumla watu wengi hunyonyesha, watoto 10 hadi 20 kati ya kila 100 wanaonyonya maziwa ya mama wataambukizwa VVU kupitia maziwa ya mama kujazia wale walioambukizwa wakati wa mimba na wakati wa kuzaliwa. Maambukizi ya VVU kupitia maziwa ya mama yanawezekana kwa kinamama waliozidiwa na ugonjwa au walioambukizwa karibuni.
- Wanawake wanaomeza dawa za kupunguza makali ya UKIMWI wanaweza kutumia njia ya kunyonyesha. Ukweli, dawa ya kupunguza makali ya UKIMWI katika wiki za mwanzo za kunyonyesha maziwa ya mama zinaweza kupunguza hatari ya maambukizo ya VVU kupitia maziwa ya mama.
- Kumpatia mtoto lishe mbadala hakuna hatari ya maambukizi ya VVU. Kama tu chakula mbadala kitafaa, kinapatikana, nafuu, endelevu, na salama, kinapendekezwa kwa miezi 6 ya mwanzo baada ya mtoto kuzaliwa. Iwapo chakula mbadala kilichopo hakiwezi kukidhi vigezo hivi 5, kumnyonyesha maziwa ya mama pekee kwa miezi 6 ya mwanzo ndiyo njia salama zaidi ya kumlisha mtoto, na inaendana na njia ya kunyonyesha.
- Mkakati mmoja wa kufanya unyonyeshaji maziwa ya mama uwe salama ni kukamua maziwa ya mama na kuyapasha moto. Kwa wanawake wanaotegemea kunyonyesha kuzuia mimba, kukamua maziwa kunaweza kupunguza ufanisi wa kuzuia mimba kuliko kunyonyesha.
Wahimize wanawake wenye VVU watumie kondomu pamoja na njia ya kunyonyesha. Zikitumiwa wakati wote na kwa usahihi, kondomu husaidia kuzuia maambukizi ya VVU na magonjwa mengine ya ngono.
Aanze Lini Kuitumia njia ya kunyonyesha
Hali ya mwanamke | Uanze lini kutumia |
Ndani ya miezi 6 baada ya kujifungua | Anza kunyonyesha mara moja (ndani ya saa moja) au mapema iwezekanavyo baada ya kujifungua. Katika siku chache za mwanzo baada ya kujifungua, majimaji ya manjano yanayozalishwa na matiti ya mama (colostrum) yana virutubisho muhimu kwa afya ya mtoto. |
Wakati wowote kama amekuwa akimnyonyesha mtoto wake maziwa ya mama tu au karibu amekuwa akimnyonyesha maziwa ya mama na hajaanza kupata hedhi. |
Mwanamke Anaweza Kutumia Njia ya Kunyonyesha Wakati Gani?
Mwanamke anayenyonyesha anaweza kutumia njia ya kunyonyesha ili kutenganisha uzazi wake na kama njia ya mpito kuelekea kwenye njia nyingine ya kuzuia mimba. Anaweza kuanza kutumia njia ya kunyonyesha wakati wowote kama anatimiza vigezo 3 vinavyotakiwa kwa ajili ya kutumia njia hii
- Je umeanza kupata hedhi?
- Je mara kwa mara unampatia mwanao vyakula vingine mbali na maziwa ya mama au kuacha muda mrefu bila kumnyonyesha, ama mchana au usiku?
- Mwanao ana umri zaidi ya miezi 6?
Kama jibu la maswali yote ni hapana… …anaweza kutumia Njia ya kunyonyesha kuzuia mimba. Kuna uwezekano wa 2% tu kupata mimba wakati huu. Mwanamke anaweza kuchagua njia nyingine ya uzazi wa mpango wakati wowote – lakini isiwe njia ya vichocheo vya estrojeni wakati mtoto akiwa na umri chini ya miezi 6. Njia zenye estrojeni zinajumuisha Vidonge vyenye vichocheo viwili, sindano za kila mwezi, vibandiko vyenye vichocheo viwili, na pete ya kuzuia mimba
Lakini, jibu la swali lolote kati ya haya likiwa ndiyo… …uwezekano wake wa kushika mimba unaongezeka. Mshauri aanze kutumia njia nyingine ya uzazi wa mpango na aendelee kunyonyesh maziwa ya mama kwa ajili ya afya ya mtoto
Namna ya kutumia njia ya kunyonyesha maziwa ya mama
- Kunyonyesha mara kwa mara
- Utaratibu unaofaa ni kumnyonyesha anapohitaji (ina maana, wakati wowote mtoto atakapotaka kunyonya) na angalau mara 10 hadi 12 kwa siku katika wiki chache za mwanzo baada ya kujifungua na baadaye mara 8 hadi 10 kwa siku, pamoja na angalau mara moja usiku katika miezi ya mwanzo.
- Unyonyeshaji wa wakati wa mchana usipishane zaidi ya saa 4, na unyonyeshaji wa usiku usipishane zaidi ya saa 6.
- Baadhi ya watoto hawataki kunyonya maziwa ya mama mara 8 hadi 10 kwa siku na wanaweza kutaka kulala usiku kucha. Watoto hawa wanaweza kuhitaji kutiliwa mkazo kwa kunyonyeshwa mara kwa mara
- Anza kumlisha vyakula vingine akiwa na miezi 6
- Anza kumlisha vyakula vingine kujazia maziwa ya mama mtoto anapofi kisha umri wa miezi 6. Katika umri huu, maziwa ya mama hayawezi kutosha kumpatia lishe ya kutosha mtoto anayekua.
- Panga kwenda kliniki
- Panga siku ya kurudi kliniki wakati vigezo vya kunyonyesha kuzuia mimba bado vikiwa vinatumika, ili aweze kuchagua njia nyingine na kuendelea kuzuia mimba
Ikiwezekana, chukuc kondomu au vidonge vyenye kichocheo kimoja kwa sasa. Unaweza kuanza kuzitumia kama mtoto hategemei maziwa kama chakula kikuu au ananyonya kidogo, kama ameanza kupata hedhi, au mtoto amefikisha umri wa miezi 6 kabla ya kuanza kutumia njia nyingine.
Kurekebisha imani potofu zilizopo kuhusu njia ya kunyonyesha
Njia ya kunyonyesha:
- Inafanya kazi sana kama mwanamke atatekeleza vigezo vyote vitatu vya njia hii.
- Inafanya kazi vizuri kwa wanawake wanene na wembamba.
- Inaweza kutumiwa na wanawake wanaotumia lishe ya kawaida. Havihitajiki vyakula maalum.
- Inaweza kutumiwa kwa miezi sita kamili bila kuhitaji chakula cha ziada. Maziwa ya mama pekee yanaweza kumstawisha mtoto kikamilifu kwa miezi 6 ya mwanzo wa maisha. Ukweli, ni chakula kinachofaa wakati huu kwa maisha ya mtoto.
- Inaweza kutumiwa kwa miezi 6 bila kuogopa kuwa mwanamke ataishiwa maziwa. Maziwa yataendelea kuzalishwa kwa miezi 6 na zaidi kulingana na unyonyaji wa mtoto au kukamua maziwa ya mama
Leave feedback about this