KUTUMIA PETE YA MPIRA YENYE VICHOCHEO VIWILI KUPANGA UZAZI

Pete ya Mpira Yenye Vichocheo Viwili Ni Nini?

Pete ya mpira yenye vichocheo viwili ni pete laini inayowekwa ukeni.

 • Hutoa vichocheo wakati wote – projestini na estrojeni, kama vilivyo vichocheo asilia vya projesteroni na estrojeni kwenye mwili wa mwanamke – kutoka ndani ya mpira wa pete. Vichocheo hufyonzwa kupitia ukuta wa uke moja kwa moja na kuingia kwenye mfumo wa damu.
 • Pete ya Mpira huwekwa na kubaki ndani kwa wiki 3, kisha huondolewa wiki ya nne. Wakati wa wiki hii ya nne mwanamke atapata hedhi.

Kimsingi hufanya kazi kwa kuzuia kutoka kwa yai kutoka kwenye ovari (uovuleshaji)

Mambo Muhimu kuhusu pete ya mpira yenye vichocheo viwili

 • Inatakiwa kuweka pete ya mpira laini ukeni. Huachwa ndani wakati wote, usiku na mchana kwa wiki 3, ikifuatiwa na wiki bila kuwa na pete.
 • Anza kuweka pete mpya ya mpira mapema ili kupata ufanisi mkubwa.

Ni kawaida kupata mabadiliko ya hedhi lakini hayana madhara.

Pete ya mpira ina Ufanisi Kiasi Gani?

Ufanisi unategemea mtumiaji: Hatari ya kupata mimba ni kubwa zaidi kama mwanamke atachelewa kuanza kutumia pete mpya

 • Pete ya mpira yenye vichocheo viwili ni njia mpya, na utafi ti juu ya ufanisi uliofanyika ni kidogo. Viwango vya ufanisi katika majaribio ya kitabibu ya mpira wa pete vinaonyesha kuwa unaweza kuwa na ufanisi zaidi kuliko Vidonge vyenye vichocheo viwili, kwa jinsi unavyotumika zaidi na unavyotumika wakati wote na kwa usahihi

Kurudi kuwa na uwezo wa kupata mimba: Bila kuchelewa

Madhara, Faida Kiafya, na Hatari Kiafya

Madhara

Baadhi ya watumiaji wameripoti yafuatayo:

 • Mabadiliko ya hedhi pamoja na: – hedhi ya matone matone na hutoka kwa siku chache – hedhi isiyotabirika – hedhi kuendelea kwa muda mrefu – kukosa hedhi
 • Maumivu ya kichwa
 • Kichefuchefu
 • Kuwashwa, ngozi kuwa nyekundu, au inflamesheni ya uke (vaginitis)
 • Kutokwa ute mweupe ukeni

Faida na Hatari Zinazojulikana Kiafya

Tafiti za muda mrefu kuhusu pete ni chache, lakini watafi ti wanatarajia kuwa faida na hatari zake kiafya ni sawa na zile za Vidonge vyenye Vichocheo Viwili

Kutoa na kuweka Pete za Mpira Zenye Vichocheo Viwili

 • Jinsi ya kuingiza pete ya mpira yenye vichocheo viwili
  • Unaweza kuchagua mkao unaomfaa – kwa mfano, kusimama kwa mguu mmoja, kuchuchumaa, au kulala.
  • Bana pete pande mbili zikutane na kuingiza sehemu iliyokunjika iingie ndani ya uke.
  • Mahali kamili si muhimu, lakini kuiingiza ndani kunasaidia kuifanya ikae isitoke, na hawezi kuihisi. Misuli ya uke kwa kawaida huifanya pete ikae mahali pake.
 • Pete lazima iendelee kuwepo ndani ya uke kwa wiki tatu
  • Acha pete iwepo ndani ya uke wakati wote, kila siku usiku na mchana kwa wiki tatu.
  • Unaweza kutoa pete mwishoni mwa wiki ya tatu na kuitupa kwenye chombo cha kutupa taka
 • Toa pete wiki ya nne
  • Ili kutoa pete, aingize kidole chake cha shahada ndani ya uke na kuishika, au kuibana pete kwa kidole cha shahada na cha kati, na kuivuta kuitoa nje.
  • Wiki hii atapata hedhi.
  • Kama atasahau na kuiacha pete wiki ya nne, hahitaji kuchukua hatua yoyote.
 • Pete isitolewe nje kwa zaidi ya saa 3 mpaka wiki ya nne ifike
  • Pete inaweza kutolewa kwa ajili ya kufanya ngono, usafi, au sababu nyingine, ingawa hakuna umuhimu wa kuitoa.

Iwapo pete itachomoka, aisuuze kwa maji safi na aiingize haraka.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/001946.htm

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi