KUUMIA JICHO AU JERAHA LA JICHO :Dalili …..

Maelezo ya jumla

Ni rahisi sana kupata jeraha la jicho yanayotokana na kupigwa. Macho yanaweza kupata majeraha pia yanayosababishwa na vitu vyenye ncha kali kama vile vipande vya kioo, au uchafu au vumbi inayoingia machoni. Kemikali zinaweza pia kurukia machoni na bidhaa nyingi za kusafishia nyumba zinaweza kusumbua jicho zikiingia. Kuna maumivu makali baada ya kuumia jicho, na jicho lililoumia hutokwa na machozi na kuvimba na kuwa jekundu. Jeraha lolote la jicho ni hatari na linapaswa kutiliwa maanani kwa sababu kuna uwezekano wa uwezo wa kuona kuathirika.

Mwone daktari ukiwa na jeraha la jicho na:

Mwone dakatari haraka sana

  • Kama jeraha kwenye jicho limesababisha unashindwa kuona vizuri au unaona ukungu
  • Kama kuna kitu kimekwamia au kinashinda kutoka jichoni
  • Kama kuna kemikali imekurukia jichoni
  • Kama mtoto ana jeraha jichoni

Mambo unayoweza kufanya wewe mwenyewe ukiwa na jerala la jicho

Namna ya kutibu jeraha la jicho

Unapaswa kuomba msaada wa kitabibu baada ya kupata jeraha lolote la jicho, isipokuwa jeraha dogo sana ambalo halikupi wasiwasi. Lengo lako kuu ni kumtuliza mgonjwa, kufunika jeraha kwa kitambaa safi na kumsaidia afike kituo cha afya kwa matibabu.

  1. Chunguza jicho kwa umakini. Kama kuna damu iliyovia chini ya ngozi ya jicho na una uhakika jeraha sio kubwa, unaweza kulitibu. Kama kuna uchafu au vumbi unaweza kuitoa, hasa kama iko kwenye eneo jeupe la jicho.

          ANGALIZO: Usijaribu kuondoa uchafu au kitu chochote kilichong’ang’ania kwenye eneo jeusi la jicho.

  1. Kama jicho limeumia sana, msaidie mgonjwa alale. Mshauri ajaribu kuyatuliza macho yake. Funika jicho lililoumia kwa kitambaa safi na kisha muombe mgonjwa aishikilie. Msaidie kufika kituo cha afya.

Namna ya kutibu jicho lililoingiliwa na kemikali (Jeraha la jicho)

Inabidi uwahi kuosha na kuondoa kemikali machoni. Jilinde na uhakikishe kuwa maji yenye kemikali yaliyotoka kwenye jicho lako yanatupwa vizuri.

  1. Vaa glavu kama zipo. Weka jicho lako chini ya mfereji wa macho yanayotiririka kwa dakika 10, weka kichwa kwa namna ambayo itaruhusu maji kumwagika bila kumwagikia jicho la pili au uso. Suuza jicho na nyusi zako vizuri. Kama macho yote yameathirika geuza kichwa ili uweka jicho la pili kwenye mfereji.
  2. Baada ya maumivu kupungua, mpatie mgonjwa kitambaa safi ili kufunika jicho vizuri. Funga vizuri kwa kutumia ‘’bandage’’ au kamba na kisha mpeleke mgonjwa hospitali. Kama unaweza jitahidi kujua ni aina gani ya kemikali ili kuwaambia madaktari.

Vyanzo

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi