Magonjwa ya dharura

KUUMWA NA NYOKA: Dalili, cha kufanya, matibabu

kuumwa na nyoka

Niepuke vipi kuumwa na nyoka?

Unaweza kufanya yafuatayo ili kupunguza uwezekano wa kuumwa na nyoka:

  • Epuka kwenda kwenye maeneo wanapoishi nyoka. Maeno hay ani kama vile, nyasi ndefu au vichaka, maeneo yenye mawe au miamba, magogo yaliyoanguka na kulala chini, kinamasi (bwawa lenye tope nyingi na nyasi), na mashimo marefu kwenye ardhini.
  • Unapokuwa unatembea ndani ya majani marefu au uchaka, piga nyasi au ardhi iliyo mbele kwa kutumia kijiti kirefu ili kufukuza nyoka.
  • Kuwa makini na angalia unapokaa au kukanyaga unapokuwa nje
  • Vaa suruali ndefu isiyobana, viatu vizito vya ngozi au mpira.
  • Mulika njia kwa kutumia tochi unapotembea usiku
  • Usimshike nyoka, hata kama unadhani amekufa. Nyaka aliyeuwawa hivi karibuni anaweza bado kukuuma kwa sababu ya kukaza kwa misuli yake (reflex).

kuumwa na nyoka

Dalili baada ya kuumwa na nyoka?

Dalili zinatofautiana kulingana na aina ya nyoka aliyekuuma. Kama nyoka aliyekuuma hana sumu, unaweza kupata maumivu, uvimbe na wekundu tu kwenye sehemu uliyoumwa. Kama umeumwa na nyoka mwenye sumu unaweza kuwa na dalili nyingi, hii ni pamoja na:

Kwa hali kali, kama una mzio na sumu ya nyoka unaweza kuwa na dalili zilizotajwa hapo juu na dalili nyingine za nyongeza

  • Kushindwa kuongea kunakotokana na kubana kwa koo na kuvimba ulimi
  • Unaweza kukohoa sana na kukorota mfululizo

kuumwa na nyokaNifanye nini nyoka akiniuma?

  • Tulia
  • Kama umemwona nyoka, jaribu kukumbuka alikuwa anaonekanaje. Usimkaribie nyoka; usijaribu kumkamata au kumuua.
  • Vua vito vya thamani ulivyovaa (kwa mfano, bangili pete n.k) au nguo zote zinazobana eneo uliloumwa, kabla halijaanza kuvimba
  • Ili kupunguza uwezekano wa sumu kusambaa, uweke mkono au mguu ulioumia chini ya usawa wa moyo
  • Safisha eneo lenye jeraha. Hakikisha unafuta kwenye uelekeo usio na kidonda. Na lifunike kwa kitambaa safi au bandeji.
  • Kama unadhani nyoka aliyekuuma ana sumu, fika kituo cha afya haraka iwezekanavyo.
  • Usijaribu kunyonya sumu kutoka kwenye kidonda
  • Usichanje chale au kusababisha eneo liloumwa kuvuja damu
  • Usiweke barafu kwenye eneo lililoumwa na nyoka
  • Usifunge Kamba ua kitu chochote kwenye eneo lenye jeraha – kama juhudi ya kupunguza kusambaa kwa sumu. USIFUNGE.
  • Usinywe pombe
  • Usinye kahawa

kuumwa na nyoka

Matibabu baada ya kuumwa na nyoka;

Unaweza kupewa chanjo/ dawa ya kupambana/kudhibiti sumu – antivenom. Zipo dawa za kudhibiti sumu ya nyoka zinazoweza kudhibiti sumu za aina nyingi za nyoka na nyingine zinaweza kudhibiti aina moja maalumu ya nyoka. Kwa hiyo, inasaidia unapojua ni aina gani ya nyoka aliyekuuma ili kupata dawa sahihi.

Baada ya kupewa dawa ya kudhibiti sumu ya nyoka, unaweza kukaa hospitalini kwa uangalizi wa masaa 24. Utaongezewa maji kama yatapungua, dawa za maumivu kama unahisi maumivu n.k

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/imagepages/8928.htm

Leave feedback about this

  • Quality
  • Price
  • Service

PROS

+
Add Field

CONS

+
Add Field
Choose Image
Choose Video
X