KUVIMBA KWA MISHIPA YA VENA MIGUUNI

Maelezo ya jumla

Kuvimba kwa mishipa ya vena miguuni ‘’varicose veins’’, ni tatizo la vena za miguu, linalosababisha mishipa ya damu kugeuka rangi na kuwa za bluu, kuvimba na kujikunja kunja chini ya ngozi. Mara nyingi utazikuta sehemu ya ndani ya mguu, kwenye ndama ya mguu au kwenye kifundo cha mguu. Mguu uliathirika unakuwa mzito, kifundo cha mguu kinavimba, na ngozi iliyofunika vena hizi inakuwa imekauka kabisa na inaweza kuwa inawasha. Tatizo hili linawapata zaidi wanawake na mara nyingi huwa ni la kurithi. Ujauzito, kufunga choo, kuwa na uzito mkubwa au kusimama muda mrefu huongeza hatari ya kupata tatizo hili.

Kuvimba kwa mishipa ya vena miguuni -unachoweza kufanya mwenyewe

Ukweli ni kuwa, njia tunazojifunza hapa hazitaondoa kabisa tatizo hili la kuvimba kwa mishipa ya vena miguuni, ila zitasaidia kupunguza karaha na kuzuia tatizo lisizidi kuendelea, kwa kuborehsa mzunguko wa damu na mkazo wa misuli

 • Epuka kusimama kwa muda mrefu. Kama unaona haiwezekani kutokusimama kwa muda mrefu, jitahidi kunyoosha misuli ya ndama ya miguu na chezesha vidole vya miguu mara kwa mara. Kama unakaa kwa muda mrefu, simama angalau kila baada ya dakika 30 na utembee tembee.
 • Usikunje miguu unapokua umekaa, kwa sababu ukifanya hivi unapunguza mzunguko wa damu kwenye miguu
 • Kama umekaa kwenye kiti cha ofisini ‘’armchair’’, nyanyua miguu kwa kuiweka juu ya ‘’stool’’ au rundo la vitabu ili kuboresha mzunguko wa amu. Kuwa makini usiweke chochote chini ya magoti.
 • Vaa viatu visivyo na visigino virefu; viatu vyenye visigino virefu vinasababisha misuli ya ndama ya mguu kufanya kazi zaidi unapokua unatembea
 • Usivae ‘’girdles’’, ‘’control top underware’’ au ‘’pantyhose’’ zinazobana kiuno au nyonga na kupunguza mzunguko wa damu kupita kwenye sehemu ya juu ya miguu. Epuka kuvaa ‘’socks’’ au ‘’knee-highs’’ zinazobana kwa juu.

Kuvimba kwa mishipa ya vena miguuni

Kuvimba kwa mishipa ya vena miguuni

 • Unaweza kutumia ‘’moisturizing creams’’ kama ngozi inakauka na kuwasha sana baada ya kuvimba kwa mishipa ya vena miguuni. Unaweza kupaka taratibu juu ya vena zilizoathirika ili kuounguza ukavu na kuwasha.
 • Kuwa makini usigonge au kuumiza ngozi inayofunika mishipa ya neva iliyovimba, ni rahisi sana kuitoboa na kusababisha kuvuja damu nyingi
 • Acha kuvuta sigara; Kuvuta sigara kuongeza hatari ya kuvimba kwa mishipa ya vena za miguu

Kuzuia kuvimba kwa mishipa ya vena miguuni

Mabadiliko kadhaa ya mfumo wa maisha yanaweza kusaidia kupunguza hatari ya kuvimba kwa mishipa ya vena miguuni au kusaidia kuzuia isiendelee kuvimba zaidi

 • Punguza uzito kama uzito wako ni mkubwa. Hii itasaida kuipunguzia shinikizo mishipa ya naeva na kuzuia mingine isivimbe
 • Fanya mazoezi mara kwa mara, kama vile kutembea, kuendesha baiskeli na kuogelea ili kuboresha mzunguko wako wa damu.
 • Kuzuia kufunga choo, kunywa maji angalau 6-8 kwa siku. Ongeza kwenye mlo vyakula vyenye nyuzinyuzi kwa wingi kamavile mkate usiokobolewa, nafaka; mchele wa usiokobolewa, mbogamboga, viazi, maharage na matunda
 • Vaa ‘’support stockings’’ au ‘’pantyhoe’’ mara kwa mara kama una ujauzito au kama kazi yako inakubidi usimame kwa muda mefu

Mwone daktari kama

Panga kumwona daktari:

 • Kama unaona kuvimba kwa mishipa ya vena miguuni kunaongezeka au kama unaona mishipa mingine inaanza kuvimba
 • Kama mshipa wa vena unaanza kuwa mwekundua au unakuwa wa moto
 • Kama ngozi inayofunika vena zilioathirika inaanza kubadilika rangi, inaanza kuuma au inaanza kuvuja majimaji

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/001109.htm

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi