Last Updated on October 13, 2023 by Dr Mniko
Maelezo ya jumla
Kuvimba kwa vifundo vya miguu ‘’swollen ankles’’ kunaweza kutokea baada ya kukaa kwa muda mrefu bila kufanya lolote, kwa mfano; wakati wa safari ndefu ya gari au ndege au kama unatumia muda mrefu ukiwa umesimama, hasa katika mazingira ya joto kali. Kuvimba kwa vifundo vya miguu hutokana na kutwama kwa majimaji miguuni kwa sababu ya mzunguko hafifu wa damu. Kwa kawaida hakutakuwa na maumivu kwenye vifundo vya miguu, ila unaweza kuhisi kama ngozi imebana na karaha kiasi.
Tatizo hili linaweza kutokea sambamba na kuvimba kwa vena za miguu ‘’varicose veins’’, na baadhi ya wanawake wako kwenye hatari zaidi ya kuvimba vifundo vya miguu wakati wa ujauzito. Baadhi ya madawa pia yanaweza kuchangia tatizo la kuvimba vifundo vya miguu, na tatizo hili mara kadhaa huwa ni dalili inayoonesha kuwa unaweza kuwa na matatizo kwenye moyo, figi au ini.
Mwone daktari kama
Panga kumwona daktari
- Kama una maumivu kwenye ndama ya mguu wako
- Kama mguu mmoja tu ndio umevimba na hakuna sababu ya wazi
- Kama unatumia madawa ambayo yanaweza kuwa yanasababisha kuvimba kwa vifundo vya miguu
Kuvimba kwa vifundo vya miguu-unachoweza kufanya mwenyewe
Jaribu kufanya mambo yafuatayo ili kupunguza au kuzuia kuvimba kwa vifundo vya miguu
- Ili kupunguza uvimbe wa vifundo vyako vya miguu, lala chini kisha inua miguu 15-30cm kutoka usawa wa moyo wako. Usiweke kitu chochote chini au nyuma ya magoti
- Kama utasimama kwa muda mrefu, jaribu kunyoosha ndama za miguu yako kila baada ya dakika kadhaa au chezesha vidole vyako vya miguu mara kwa mara
- Kama uko kwenye hatari ya vifundo kuvimba, vaa ‘’support stockings’’. Zivae asubuhi na mapema kabla miguu haijaanza kuvimba
- Kama unasafiri kwa muda mrefu, simamisha gari mara kwa mara ili upate kupumzika na kunyoosha miguu.
- Wakati wa safari ya ndege au ya gari ya muda mrefu, fanya mazoezi haya kila baada ya dakika 30 ili kuboresha mzunguko wa damu miguuni. Yatasaidia pia kuzuia kupata tatizo hatari la kuganda damu miguuni linaloitwa ‘’deep vein thrombosis’’.
- Anza miguu yako ikiwa imelala kabisa sakafuni, visigino vikibakia sakafuni, jaribu kuinua juu vidole vya miguu kadri unavyoweza
- Sasa nyanyua visigino vyako juu huku vifundo vya vidole vikiwa vimekanyaga chini. Jaribu kuinua na kushusha visigino kwa angalau sekunde 30.
- Nyoosha mguu mmoja mbele ya mwingine na kisha jaribu kuuzungusha kwa angalau mara 8 kila mwelekeo. Badili na kurudia utaratibu huu kwenye mguu mwingine
- Kunywa maji angalau glass 6-8 kwa siku ili kuepuka upungufu wa maji mwilini. Mwili utaondoa maji ambayo hauyataji.
- Vaa viatu visivyo na visigino virefu. Viatu vyenye visigino virefu vinasababisha misuli ya ndama ya miguu kufanya kazi zaidi na kupunguza mzunguko wa damu. Viatu vyenye visigino vya kawaida huongeza mzunguko wa damu
- Epuka kuvaa ‘’girdles’’, control-top underwear’’ au ‘’pantyhose’’ na socks zinazobana. Vyote hivi vinabana sehemu ya juu ya miguu, hivyo kupunguza mzunguko wa damu
Kuvimba kwa vifundo vya miguu -mwone daktari kama
Panga kumwona daktari
- Kama kuvimba kwa vifundo vya miguu hakupungui baada ya kufanya mambo yaliyoelezwa hapo juu
Leave feedback about this