KUVIMBA TUMBO: Sababu, dalili, matibabu

Maelezo ya jumla

Kuvimba tumbo mara nyngi kunatokana na gesi inayosababishwa na kula aina fulani za vyakula, lakini wakat mwingine inaweza kuwa ishara ya kuepo tatizo jingine kubwa. Kwa sababu hii, kama tatizo la kuvimba tumbo limetokea hivi karibuni, limevimba zaidi kuliko kawaida au kama dawa unazotumia hazisaidii, ni vyema kuonana na daktari ili afanye vipimo kwa ajili ya utambuzi.

Ni zipi dalili za kuvimba tumbo?

Zifuatazo ni dalili zinazoweza kuonekana kwa mtu mwenye tatizo la kuvimba tumbo:

Ni nini husababisha kuvimba tumbo?Kuvimba tumbo

Mambo yafuatayo yanaweza kuwa sababu ya kuvimba tumbo:

 • Kumeza hewa (hasa kama una woga)
 • Kufunga choo
 • Tatizo la kubeua/kucheua asidi kutoka tumboni kwenda kwenye umio -GERD
 • Kushindwa kuhimili baadhi ya vyakula – kwa mfano kujisikia vibaya baada ya kunywa maziwa au bidhaa za maziwa
 • Kula sana
 • Kuongezeka kwa bakteria katika utumbo mdogo wa chakula
 • Kuongezeka uzito wa mwili

Sababu hatari zaidi zinazoweza kusababisha kuvimba tumbo ni pamoja na:

Ni nani yuko kwenye hatari zaidi?

 • Wanawake
 • Watu wenye kiwango cha juu cha uwiano wa uzito na urefu BMI

Ni wakati gani unapaswa kutafuta matibabu?

Kama ni tatizo la kuvimba tumbo lenyewe, sio swala la kutia mashaka sana. Ni vizuri kuonana na daktari kama unaona tatizo linakusumbua sana na kama kuna dalili nyingine za ziada ambazo zinaweza kuhitaji vipimo na matibabu. Dalili ambazo zinapaswa kuangalia na daktari ni pamoja na maumivu ya tumbo, kutapika, kuharisha, kufunga choo, kupungua uzito, kuvuja damu kutoka kwenye mfumo wa chakula na kiungulia.

Baadhi ya dalili zinazopaswa kutiliwa mashaka sana ni pamoja na:

 • Kama kuvimba tumbo kunaendelea kuongezeka kadri muda unavyokwenda
 • Kama kuvimba tumbo kumetokea pamoja na dalili usiyoweza kuielezea
 • Kama tumbo linauma ukiligusa
 • Kama una homa kali
 • Kama unaharisha au unapata kinyesi chenye damu
 • Unashindwa kunywa au kula kwa zaidi ya masaa 6 – 8

Utambuzi

kuvimba tumbo

Kulingana na dalili ulizonazo, utambuzi wa sababu ya kuvimba tumbo unaweza kujumuisha yafuatayo:

 • Vipimo vya maabara – kama vile vipimo vya damu kuangalia matatizo ya mfumo wa chakula na kazi ya ini
 • Vipimo vya picha – eksirei ya tumbo na utumbo
 • Kipimo cha kutumia kamera ndogo kuangalia ndani ya utumbo na tumbo – colonoscopy, sigmoidoscopy, upper endoscopy
 • Vipimo vya kuangalia kama unaweza kuhimili maziwa – ili kuhakikisha kama tatizo la kuvimba tumbo limesababishwa na kula maziwa au bidhaa za maziwa
 • Vipimo vya kinyesi – kuangalia kama kuna damu, kiwango cha mafuta kilichomo, na kama kunavimelea wanaoitwa girdia
 • Kipimo cha mimba

Uchaguzi wa matibabu

 • Onana na daktari ili kutambua kama kuvimba tumbo hakujasababishwa na tatizo jingine kubwa kama ugonjwa wa ini au saratani ya ovari
 • Badili mlo – epuka kula maziwa au bidhaa za maziwa, na dalili zitakusaidia kufahamu vayakula unavypaswa kuepuka. Hii inaweza kuwa vyakula vya maziwa, mbogamboga, vinywaji baridi na nafaka.
 • Kwa wenye matatizo ya kufunga choo, kuongeza kiwango cha nyuzinyuzi kwenye mlo, kupunguza msongo na kutumia dawa husaidia
 • Dawa za kupunguza gesi tumboni zinaweza kusaidia, dawa kama simethicone
 • Dawa kama vile bismuth zinaweza kusaidia kama una harisha
 • Kwa wale wanaomeza hewa, ni vizuri kulitambua hilo:
  • Piga pafu ndogondogo za kinywaji cha moto
  • Epuka kunywa vinywaji baridi
  • Tafuna gum/jojo au mumunya pipi
  • Kula taratibu
  • Kunywa kwa kutumia mrija
 • Pata matibabu ya matatizo ya ini iliyokuwa nayo
 • Unapaswa kuhitajika kufanyiwa upasuaji kama sababu ya kuvimba tumbo ni kuziba kwa utumbo, ngiri, au saratani/uvimbe.
 • Unaweza kuhitajika kubakia hospitali ili kupewa dawa za antibiotiki kama kuvimba tumbo kumesababishwa na tatizo la kukua au kuongezeka kwa bakteria kunakosababisha tatizo la kuvimba kwa fumbatio – peritonitis
 • Unaweza kuhitaji kufanyiwa uchunguzi zaidi kama sababu ya kuvimba tumbo inadhaniwa kuwa tatizo la ini

Nini cha kutarajia?

Mara nyingi matokeo ni mazuri kama sababu ya kuvimba tumbo ni gesi au kushindwa kuhimili baadhi ya vyakula. Matarajio sio mazuri kama saratani ya ovari ndio sababu ya kuvimba tumbo, na matarajio hayaeleweki kulingana na hatua ya ugonjwa wa ini. Matarajio ya sababu nyingine yanategemea, yanategemea ni katika hatua gani ya ugonjwa umetambulika.

Matatizo yanayoweza kutokea?

Matatizo yanayoweza kutokea ni kidogo kama kuvimba tumbi kumesababishwa na gesi au kushindwa kuhimili aina fulani ya chakula. Baadhi yanaweza kusababisha utapiamlo – celiac sprue. Baadhi ya sababu za kuvimba tumbo zinaweza kusababisha kifo.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/003122.htm

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi