KUVIMBIWA NA KUJAMBA:Dalili,sababu,matibabu

Maelezo ya jumla

Kuvimbiwa na kujamba ni tatizo la kawaida linalosababishwa na kujaa kwa hewa ndani ya mfumo wa umeng’enyaji wa chakula. Unaweza pia kuhisi maumivu makali au kusikia sauti za kuunguruma ndani ya tumbo. Matukio mengi ya kuvimbewa na kujamba yanatokana na chakula, baadhi ya vyakula kama maharage na kabeji vinatoa kiasi kikubwa cha hewa wakati kinameng’enywa. Kula haraka haraka pia kunaweza kusababisha gesi tumboni. Baadhi ya watu mfumo wao wa kumeng’enya chakula hauwezi kuhimili maziwa, baadhi ya viungo au unga wa ngano, na kwa sababu hiyo wanapata shida hii. Kwa baadhi ya nyakati, kuvimbiwa na kujamba kunaweza kutokana na matatizo ya utumbo kama vile ‘’irritable bowel syndrome’’.

Kuvimbiwa na kujamba – mwone daktari

Panga kumwona daktari kama una dalili nyingine za mfumo wa umeng’enyaji, kama vile kufunga choo, kuhara, damu kwenye kinyesi, kichefuchefu, kutapika au maumivu ya tumbo ya muda mrefu au yanayojirudia rudia.

Unachoweza kufanya wewe mwenyewe

Jaribu kufanya mambo yafuatayo ili kupunguza kujaa kwa gesi au kutibu kuvimbiwa na kujamba

  • Jaribu kutambua ni vyakula gani ambavyo ukila vinasababisha tatizo hili. Mara nyingi kabeji, vitunguu maji, vitungu swamu, maharage, na viungo vingine vinasababisha shida hii.
  • Unaweza ukapata gesi tumboni kama umeongeza kwenye vyakula vyenye kiwango kikubwa cha nyuzinyuzi kwenye mlo haraka sana. Vyakula vyenye nyuzinyuzi ni vigumu kumeng’enya, mwili unahitaji muda kuvizoea. Punguza, na kisha anza kuongea taratibu, ndani ya wiki 2-3
  • Kunywa na kula taratibu, tafuna chakula vizuri na kikamilifu. Inaweza kusaidia ukila milo midogo midogo kwa siku badala ya kula mlo mmoja au miwili mikubwa
  • Punguza kunywa pombe na vinywaji vya viwandani vyenye kaboni kama vile soda. Punguza kuvuta sigara na kutafuna ‘’gum’’. Vitu vyote hivi vinaweza kujaza gesi tumboni na kusababisha kujamba
  • Jaribu kunywa chai, ukitumia majani ya chai ya kienyeji itapendeza zaidi, inaweza kusaidia kupunguza dalili
  • Unaweza kutumia mchanganyiko wa ‘’simethicone’’ ili kutibu gesi tumboni. Inasaidia kutawanya gesi tumboni. Mara nyingi huwa inatumika pamoja na dawa za kudhibiti asidi tumboni ‘’antiacid’’ ili kuboresha mmeng’enyo wa chakula. Kama unatumia madawa mengine, usitumie dawa za kudhibiti aside bila ushauri wa daktari, dawa hizi zinaweza kupunguza uwezo wa kufyonzwa kwa dawa unazotumia.

Kuvimbiwa na kujamba – mwone daktari

Panga kumwona daktari kama una tatizo la kuvimbiwa na kujamba lililodumu kwa muda wa wiki 2 au kama unaona kuna dalili nyingine mpya

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/003124.htm

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi