KUWAHI KUFIKA KILELENI

KUWAHI KUFIKA KILELENI

 • February 23, 2021
 • 0 Likes
 • 92 Views
 • 2 Comments

Maelezo ya jumla

Kuwahi kufika kileleni, ni pale mwanaume anapomwaga manii muda mfupi tu baada ya msisimuo wa kingono, kabla tu au muda mfupi tu baada ya kuingiza uume kwenye uke. hili ni tatizo linalowapata wanaume wengi, hasa vijana wadogo wanaoanza ngono. Tatizo hili mara nyingi linasababishwa na hamu au mshawasha na/au wasiwasi ambao mara nyingi unakuwepo wakati wa mahusiano mapya, lakini tatizo linaisha kadri muda unavyokwenda na wapenzi kuzoeana. Lakini, kama tatizo la kuwahi kufika kileleni litakuwa la kudumu, linaweza kukera sana kimwili, kihisia na hata kusababisha mahusiano ya wapenzi kutatizika. Msongo wa mawazo na sonona husababisha hali kuwa mbaya zaidi; baadhi ya wanaume wanakuwa na wasiwasi mwingi sana kiasi kwamba wanashindwa kabisa kusimamisha uume. Kwa mara chache, tatizo hili linaweza kusababishwa na shida kwenye tezi dume au mfumo wa mishipa ya fahamu.

Unachoweza kufanya wewe mwenyewe ukiwa na tatizo la kuwahi kufika kileleni

Kwa sababu wasiwasi unachangia kwa kiasi kikubwa kuwahi kufika kileleni, kuzungumza kuhusu tatizo hili na mwenzi kutasaidia kulipunguza. Lakini pia kuna mbinu kadhaa unazoweza kuzijaribu

 • Kama upo kwenye mahusiano ya muda mrefu, zungumza na mwenzi wako. Ongea na mwenzio kwa utaratibu bila haraka mkiwa mmetulia, usizungumze nae wakati wa ngono, au baada tu ya ngono. Usijilaumu au kuhisi hatia.
 • Kwa baadhi ya wanaume wakivaa kondomu inasaidia kupunguza msisimko na kwa sababu hiyo wanachelewa kufika angalau.
 • Jaribu kutumia mbinu ya kuminya uume ili kusaidia kudhibiti kufikia kileleni
  • Njia hii ya kusaidia kuzuia kufika kileleni mapema inaweza kufanywa na mwanaume mwenyewe au mwenzi wake
  • Ukianza kuhisi kuwa unataka kumwaga manii, chomoa uume na tumia kidole gumba na vidole viwili vya mwanzo, kuminya uume sehemu ya kwenye kichwa kwa chini (kama ilivyooneshwa pichani). Kutumia mbinu hii kunasaidia kupoteza hamu ya kutaka kumwaga manii kwa muda, na unaweza kuendelea na tendo.
  • Ukiendelea kutumia njia hii mara kwa mara, itakusaidia kudhibiti ni wakati gani wa kumwaga manii, na hili litakuongezea kujiamini zaidi. Mwishowe, hautahitaji tena kutumia njia hii.
 • Wakati wa kuandaana / kutomasana kabla ya ngono, fikiria zaidi jinsi ya kumpa raha mwenzio kuliko wewe, na chelewesha kuanza kufanya ngono kadri unavyoweza. Kama mwenzi wako atakuwa yuko karibu kufika kileleni au amefika kileleni kabla haujamwingilia, itawapunguzia wote wasiwasi kuhusu kuwahi kufika.
 • Jaribu kufanya utafiti na jaribu mikao mbalimbali ya ngono, kuona upi unawahi na upi unachelewa. Kwa mfano, ukimuweka mwenzi wako kwa juu, inapunguza msuguano na kusaidia kuchelewa kumwaga.
 • Wakati wa tendo la ngono unaweza kujisahaulisha ‘distract’’ kwa kufiria kitu kingine ambacho hakihusiani na ngono; kwa mfano unaweza kuwa unahesabu kimoyomoyo kurudi nyuma au unaweza kufikiria kuhusu kazi

Kama una tatizo la kuwahi kufika kileleni mwone daktari kama

Panga kumwona daktari kama:

 • Unaendelea kupata tatizo hili la kuwahi kufika kileleni japo umejaribu njia zote zilizoelekezwa hapo juu

 Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/001524.htm

 • Share:

2 Comments

 •  4 siku ago

  Shukran Sana ndugu kwa elimu unayo endelea kutupati Mungu Akubariki uendelee kua na moyo wa busra nguvumu za kijana na hekma kama mZee

  •  4 siku ago

   Asante kwa mrejesho , nikefurahi kusikia kutoka kwako. Endelea kuwa balozi wetu, tufuatilie, penda na sambaza makala zetu.

Leave Your Comment