KUWASHWA AU MAUMIVU YA KOO

Maelezo ya jumla

Kuwashwa au maumivu ya koo ni tatizo la kwaida sana. Pamoja na koo kuuma, unaweza kuwa unapata shida kumeza, ukawa na ka-kikohozi kepesi, sauti inaweza kuwa inakwaruza kwaruza, homa, maumivu ya kichwa na kuvimba kwa tezi zilizo kwenye shingo. Kwa kawaida unakuta hii hali ya kuwasha au kuuma kwa koo inazidi kuwa mbaya ndani ya siku 2-3 na baada ya hapo inaondoka. Kwa kawaida hali hii huwa inasababishwa na maambukiz ya virusi, na mara nyingi inatokea sambamba na mafua. Sababu nyingine inayoweza kusababisha hali hii ni ugonjwa wa mafindofindo ‘’tonsilitis’’. Kama una mafindofindo kuna uwezekano kuwa utakuwa na homa kali zaidi na unaweza kujisikia kuumwa zaidi. Tezi zako za koo zitakuwa zimevimba , zitakuwa na usaha na hautajisikia vizuri utakapojaribu kula au kunywa.

Kuwashwa au maumivu ya koo na unachoweza kufanya mwenyewe

Unaweza kufanya mambo yafuatayo ili kupunguza karaha unapojisikia kuwashwa au maumivu ya koo

 • Kunywa maji angalau glass 8 kwa siku, hata kama unahisi maumivu wakati wa kunywa maji, kwa sababu koo lako litakuwa na hali mbaya zaidi kama litakuwa limekauka au kama umepungukiwa maji mwilini. Unaweza kutumia maji ya uvuguvugu ambayo yamewekewa limao na asali. Epuka ‘’juice’’ za matunda jamii ya machungwa ambayo haijawekewa maji ya kutosha, yana asili ya tindikali ‘’acid’’ ambayo inaweza kusumbua koo zaidi
 • Kula vyakula laini, vyakula vilivyopondwa kama vile wali boko na yogurt kama una tatizo la kuwashwa au maumivu ya koo. Ice cream ni nzuri, inapooza koo na inawafaa kuwapa shime watoto kula
 • Tumia dawa za kupunguza maumivu, dawa kama ‘’acetaminophen’’ au ibuprofen zinaweza kutumika pia na watoto, zipo za maji ambazo wanaweza kunywa. Kwa watu wazima wanaweza kuloweka Aspirini kidonge 1 au 2 kisha waka gogomoa ‘’gargle’’ huo mchanganyiko ili ufike kabisa kooni. Unaweza kufanya hivi mara 3-4 kwa siku kama unavyohitaji. TAHADHARI: Watoto na vijana walio kwenye balehe wasitumie Aspirin bila ushauri wa daktari kwa sababu kunakuwepo na hatari ugonjwa mkali unaoitwa ‘’Reye’s syndrome
 • Unaweza pia kugogomoa ‘’gargle’’ kwa kutumia mchanganyiko wa chumvi na maji. Chukua chumvi nusu kijiko na uiloweke kwenye maji ya uvuguvugu kwenye glass, na kisha gogomoa kwa sekunde 30, kisha tena.

  Kuwashwa au maumivu ya koo
  Kugogomoa
 • Usitumie madawa ya kusukutua mdomo ‘’mouthwashes’’ ambazo zina pombe ‘’alcohol’’ ndani yake, hizi huwa zinakausha mdomo na ulimi na kusababisha shida zaidi
 • Pumzisha koo lako. Epuka kuonea saana au kuongea kwa nguvu sana
 • Kama unakaa kwenye nyumba inayopashwa, hasa watu wanaokaa maeneo ya baridi. Hakikisha chumba chako kina unyevu wa kutosha ‘’humidified’’, unaweza kuweka bakuli lenye maji karibu na ‘’radiator’’ ili kuongeza unyevu chumbani
 • Epuka kukaa maeneo yenye moshi au uchafuzi mkubwa wa mazingira, maana itasababisha hali yako kuwa mbaya zaidi. Kama unavuta sigara, jaribu kuacha kuvuta au jaribu angalau kupunguza wakati huu unapokuwa na shida hii.

Kuwashwa au maumivu ya koo – mwone daktari kama

Ni vizuri kupanga kumwona daktari kama:

 • Kama Kuwashwa au maumivu ya koo yanazidi kuongezeka au hayapungui baada ya siku 5
 • Kama unaona unapata shida saana kumeza
 • Kama unaona kuna dalili nyingine zinaanza kujitokeza, kama vile maumivu ya viungo ua kuvimba kwenye makwapa au kwenye kinena

Vyanzo

https://medlineplus.gov/sorethroat.html

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi