KUWASHWA/FANGASI KWENYE PUMBU:Dalili, matibabu

Maelezo ya jumla

Ugonjwa wa kuwashwa/fangasi kwenye pumbu ni tatizo linalosababishwa na fangasi wanaoshambulia eneo la kinena.

Ni zipi dalili za kuwashwa/fangasi kwenye pumbuKuwashwa/fangasi kwenye pumbu

 • Kuwashwa kwenye kinena, kwenye mikunjo ya sehemu ya ndani ya mapaja, au mk*ndu.
 • Kunakuwepo na wekundu wa ngozi, inayobadilika kuwa kama magamba na inaweza kutengeneza malengelenge ambayo yanaweza kupasuka kutoa majimaji
 • Ngozi ya eneo lililoathirika inakuwa nyepesi kuliko kawaida na inaweza kuwa nyeusi kuliko kawaida

Ni nini sababu ya ugonjwa wa kuwashwa/fangasi kwenye pumbu?

 • Ugonjwa wa kuwashwa/fangasi kwenye pumbu husababisha na aina fulani ya fangasi anayeota na kusambaa kwenye eneo la kinena.
 • Ugonjwa wa kuwashwa/fangasi kwenye pumbu unaweza kuanza baada ya msuguano unaotokana na nguo na unyevunyevu unaokuwepo kwenye eneo la kinena, hasa baada ya kutokwa jasho.
 • Ugonjwa wa kuwashwa/fangasi kwenye pumbu unaweza kuambukiza. Unaweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja mpaka mwingine kwa kugusana ngozi kwa ngozi au kwa kuchangia nguo ambazo hazijafuliwa.

Ni nani yupo kwenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa wa kuwashwa/fangasi kwenye pumbu?

Ugonjwa wa kuwashwa/fangasi kwenye pumbu unawapata zaidi wanaume watu wazima na wavulana walio kwenye balehe. Kwa baadhi ya watu ugonjwa huu unaweza kuambatana na fangasi wa kwenye miguu na mapunye/vibarango mwilini.

Fangasi anayesababisha ugonjwa wa kuwashwa/fangasi kwenye pumbu hukua vizuri  kwenye maeneo ya joto, na yenye unyevunyevu.

Utambuzikuwashwa pumbu

Daktari anaweza kufanya utambuzi wa ugonjwa wa kuwashwa/fangasi wa pumbu kwa kuangalia mwonekano wa ngozi.

Mara nyingi vipimo sio lazima. Kama vipimo vitahitajika ili kufanya utambuzi, daktari atachukua sampuli kwa kukwangua ngozi ya mahala palipoathirika na kisha kuipeleka maabara kupimwa. Kipimo cha potassium hydroxide (KOH) kinaweza kufanyika kwenye ofisi ya daktari.

Ni wakati gani unapaswa kupata huduma ya kitabibu haraka?

Onana na daktari kama umejaribu kujihudumia mwenyewe nyumbani kwa zaidi ya wiki 2, au kama unaona una dalili nyingine.

Uchaguzi wa matibabu

Unaweza kununua dawa ya kupaka ya kudhibiti fangasi kutoka duka la dawa. Kuna aina nyingi – kwa mfano, terbinafine, clotrimazole, econazole, ketoconazole na miconazole. Dawa hizi za kisasa, zinafanya kazi vizuri kuondoa fangasi.

 • Paka dawa eneo lilioathirika na paka sentimeta 2 – 4 ya ngozi ambayo haijaathiriwa inayozunguka
 • Paka dawa kwa muda ulioelekezwa na mtaalamu. Muda wa kupaka unatofautiana kulingana na dawa ya kupka uliyopatiwa, soma maelekezo vizuri.
 • Kama ngozi iliyoathirika imevimba sana, daktari anaweza kuagiza upewe dawa ya kudhibiti fangasi iliyochanganywa na dawa ya kupunguza uvimbe. Hii kwa kawaida itapaswa kutumiwa kwa siku saba tu. Unaweza kuhitajika kuendelea kutumia dawa yenye dawa ya fangasi pekee baada ya kumaliza siku saba za dawa yenye mchanganyiko. Dawa yenye mchanganyiko wa dawa ya kudhibiti fangasi nay a kupunguza uvimbe (steroid), itasaidia kupunguza uvimbe na mwasho haraka.

Dawa za kudhibiti fangasi za kumeza zinaweza kutumika kama fangasi wamesambaa sehemu kubwa mwilini au hali inaonekana mbaya sana – kwa mfano, vidonge vya terbinafine, griseofluvin, au itraconazole.

Mambo ya kufanya wewe mwenyewe nyumbani ili kudhibiti kuwashwa/fangasi kwenye pumbu

Mambo unayoweza kufanya mwenyewe nyumbani ili kupambana na ugonjwa wa kuwashwa/fangasi kwenye pumbu ni kama ifuatavyo:

 • Osha ngozi ya kinena mara mbili mpaka mara tatu kwa siku
 • Hakikisha eneo la kinena linabakia kuwa kavu
 • Epuka kusababisha harara kwenye eneo la kinena kwa kuvaa nguo ya ndani iliyotengenezwa kwa pamba 100%
 • Epuka kutumia dawa za kufulia zilizo kali – fabric softeners, bleaches au detergents
 • Paka dawa ya kudhibiti fangasi (antifungal) kama ulivyoelekezwa katika eneo lililoathirika kila siku

Matarajio

Ugonjwa wa kuwashwa/fangasi kwenye pumbu unapona vizuri baada ya kutumia dawa. Ni ugonjwa ambao sio mkali sana ukilinganisha na aina nyingine ya maambukizi, lakini unaweza kudumu kwa muda mrefu.

Ugonjwa wa kuwashwa/fangasi kwenye pumbu unaathiri sehemu ya juu ndani ya mapaja kwenye mikunjo, na huathiri pumbu au uume. Ugonjwa huu unaweza kusambaa mpaka kwenye mk*ndu, na kusababisha kuwashwa sehemu ya haja kubwa.

Sababu nyingine zinazosababisha kuwashwa kinena ni pamoja na:

Matatizo yanayoweza kutokea

 • Mabadilko ya rangi ya ngozi yanayoweza kuwa ya kudumu kwenye eneo lililoathirika
 • Kupata maambukizi ya bakteria kwenye eneo lililoathirika
 • Unaweza kupata madhara mabaya yanayotokana na dawa zinazotumika kutibu ugonjwa huu

Kuzuia

 • Hakikisha eneo la kinena ni safi na kavu
 • Usivae nguo ambazo zinasugua au kusababisha harara kwenye eneo la kinena. Epuka kuvaa nguo zinazobana sana na zinazosugua sugua eneo la kinena
 • Vaa nguo za ndani zisizobana sana
 • Baada ya kuoga, paka dawa ya kudhibiti fangasi au powder ya kujikausha kama unapata shida hii mara kwa mara

Vyanzo

http://www.nlm.nih.gov/medlineplus/ency/article/000876.htm/

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi