KUWASHWA SEHEMU YA KUTOLEA HAJA KUBWA

KUWASHWA SEHEMU YA KUTOLEA HAJA KUBWA

 • February 21, 2021
 • 0 Likes
 • 169 Views
 • 0 Comments

Maelezo ya jumla

Kuwashwa sehemu ya kutolea haja kubwa (mkundu), ni hali inayoleta karaha sana na inaweza kuaibisha kwa sababu unapata hamu kubwa ya kutaka kujikuna. Ngozi inayozunguka mkundu inaweza kuwa nyekundu na inayouma, na inaweza kuvuja damu na hata kupata maambukizi kama utapakuna sana. Kuwashwa mara nyingi huwa kunazidi baada ya kujisaidia na usiku. Mtu anaweza kuwashwa mkundu kwa sababu ya harara inayotokana na bidhaa za kujitawadhia au marashi anayotumia, jasho, unyevu unyezi au vipande vya mavi vinavyobakia kwenye ngozi kuzunguka eneo la kutolea haja kubwa. Watu ambao wana uzito mkubwa, wanaotokwa jasho jingi sana au wanaovaa chupi zinazobana sana wako kwenye hatari zaidi ya kuwashwa. Wakati mwingine aina fulani za vyakula, zinaweza kuchangia tatizo hili. Bawasiri na minyoo inayoitwa ‘’pinworm’’ ni sababu pia za tatizo hili.

Mwone daktari kama

Panga kumwona daktari kama:

 • Unatokwa na damu kwenye eneo linalozunguka sehemu ya kutolea haja au kama kuna vitu kama kamasikamasi vinatoka huko
 • Una maumivu na/ au uvimbe mk*nduni au au eneo linalozuunguka mkundu

Unachoweza kufanya wewe mwenyewe

Tatizo la kuwashwa sehemu ya kutolea haja kubwa, kwa kawaida linaweza kudhibitiwa kwa matibabu kadhaa nyumbani, matibabu haya yanaweza pia kuzuia tatizo hili lisijirudie

 • Jitahidi na epuka kujikuna. Kata kucha ziwe fupi na ukiweza vaa glavu wakati wa usiku ili usijikwaruze utakapojikuna ukiwa usingizini
 • Unaweza kutumia madawa yenye ‘’antihistamine’’ ili kupunguza kuwashwa na kukupatia usingizi. Madawa haya yanapatikana kama kidonge au dawa ya kunywa, zitumie ili zikusaidie ulale.
 • Safisha eneo la mkundu asubuhi na jioni kwa kutumia maji ya kawaida na kisha pakaushe vizuri. Hakikisha kuwa eneo limekausha vizuri. Unaweza kutumia ‘’hair dryer’’ kupakausha’
 • Unaweza kupaka mchanganyiko unaotumika kudhibiti bawasiri ‘’hemorrhoid preparation’’ ili kupunguza kuwashwa. Madawa haya yana ‘’phenylephrine’’ ambayo inasaidia kupunguza uvimbena mwasho unaosababishwa na bawasiri na ‘’hydrocortisone’’ ambayo inapunguza uvimbe. Usitumie madawa haya kwa zaidi ya siku 5-6.
 • Jisafishe vizuri kila baada ya kujisaidia. Kama kujisafisha haiwezekani kwa wakati huo, tumia kitambaa kilicholoweshwa au karatasi laini za chooni zilizolowanishwa kujisafisha. Tumia ‘’toilet paper’’ kujikausha vizuri ili kuondoa unyevu nyevu baada ya kukojoa.
 • Vaa kufuli/chupi zisizo bana zilizotengenezwa kwa pamba, na badili kila siku na ikibidi mara kadhaa kwa siku. Euka kuvaa suruali zinazobana au ‘’panyhose. Ukiweka upindo wa kitambaa au tishu laini karibu na sehemu ya kutolea njia ya haja kubwa itanyonya na kuondoa unyevunyevu wote.
 • Jaribu kutafuta na kutambua aina za vyakula au vinywaji ambavyo vinaweza kuwa vinachangia kukusababishia tatizo hili la kuwashwa sehemu ya kutolea haja kubwa. Vinywaji na vyakula kama vile bia, kahawa, nyanya na vyakula vyenye pilipili nyingi.

Mwone daktari kama

Panga kumwona daktari kama:

 • Kuwashwa hakujapungua baada ya wiki moja ya kufuata mbinu zilizoelekezwa hapo juu
 • Unaona kuna dalili nyingine zinaanza kujitokeza kwako au kama mwanafamilia mwingine amenza kupata shida kama yako

Vyanzo

https://www.healthline.com/health/itchy-anus

 • Share:

Leave Your Comment