KUWASHWA

KUWASHWA

 • November 28, 2020
 • 0 Likes
 • 120 Views
 • 0 Comments

Maelezo ya jumla

Kuwashwa (itching) ni hali ya kuhisi mchonyoto unaokera kwenye ngozi anaokufanya utamani kukuna sehemu ilioathiriwa. Unaweza kuwashwa sehemu fulani ya mwili pekee au mwili mzima.

Kuwashwa husababishwa na nini?

Kuna sababu nyingi za kuwashwa, ikiwa ni pamoja na:

 • Kuzeeka kwa ngozi
 • Kuvimba kwa ngozi kunakosababishwa na mzio –atopic dermatitis
 • Kuvimba kwa ngozi kunakosababishwa na kugusa vitu vinavyosumbua na kuwasha ngozi (Kugusa sumu ya mti wa mwaloni au mwefeu)-contact dermatitis
 • Kugusa vitu vinavyoudhi au kuunguza ngozi (kama vile sabuni, kemikali, au pamba)
 • Ngozi kavu
 • Ugonjwa wa mabaka ngozini- hives
 • Kuumwa na wadudu
 • Vimelea kama vile minyoo, chawa wa mwili, chawa wa kichwa, au chawa wa mavuzi
 • Magonjwa ya ngozi kama pityriasis rosea au psoriasis
 • Upele
 • Kuunguzwa na mwanga wa jua
 • Maambukizi ya ngozi kama vile kuvimba kwa vinyweleo (folliculitis) au maambukizi yanayosababisha malengelenge (impetigo)

Kuwashwa mwili mzima kunaweza kusababishwa na:

 • Athari inayotokana na mzio (allergic reaction)
 • Maambukizi ya utotoni (kama vile tetekuwanga (chickenpox) au surua(measles))
 • Homa ya manjano (inayoashiriwa na ini kuvimba)- hepatitis
 • Upungufu wa damu (anemia) unaosababishwa na upungufu wa madini ya chuma mwilini
 • Ugonjwa wa figo
 • Ugonjwa wa ini unaosababisha manjano
 • Ujauzito
 • Matokeo mabaya ya dawa na vitu kama vile antibiotiki (penicillin, sulfonamides), dhahabu, griseofulvin, isoniazid, opiates, phenothiazines, au vitamini A

Utambuzi

Daktari au muuguzi atakuchunguza na kuuliza maswali kadhaa kuhusu historia yako ya kimatibabu na dalili.

Unaweza kuulizwa maswali yafuatayo:

 • Umekuwa ukiwashwa kwa muda gani sasa?
 • Je! Unawashwa muda wote?
 • Je, kwuwashwa kunaongezeka makali au kuenea?
 • We unadhani ni nini kinasababisha unawashwa?
 • Je! Umeshawahi kuwashwa kwa namna hii huko nyuma? Ni nini kilichosababisha uwashwe kipindi hicho?
 • Je! Umekutana na kitu chochote kinachoweza kusababisha kuwashwa ngozi hivi karibuni?
 • Je! Una mzio na kitu chochote au uko-sensitive na kitu fulani?
 • Je, unatumia dawa gani?
 • Je! Umeanza kutumia bidhaa yoyote mpya hivi karibuni? Ni ipi?
 • Je! Umetumia sabuni mpya, kitambaa , marashi, manukato, au kemikali?
 • Je! Ulikuwa karibu na wanyama?
 • Je, umekula samakigamba (shellfish) au njugu/karanga hivi karibuni?
 • Je! Umeumwa na mdudu/wadudu hivi karibuni?
 • Je, unapaka losheni kwenye ngozi yako?
 • Je, umekaa kwa muda mrefu juani hivi karibuni?
 • Je! Unawashwa sehemu gani ya mwili wako?
 • Je, Unawashwa mwili mzima?
 • Je, unawashwa eneo gani la mwili? Ni eneo lipi?
 • Je! Sehemu ya ngozi inayowasha inaonekanaje?
 • Je, kuna upele? Ikiwa ndivyo, je, kuna malengelenge, magamba au ukurutu?
 • Je, unatibiwa ugonjwa au hali nyingine yoyote?
 • Je, Una dalili nyingine zozote?

Wakati gani utafute matibabu ya haraka?

Mwone daktari au muuguzi kama unawashwa na:

 • Una dalili nyingine zisizoeleweka
 • Makali ya muwasho yanaongezeka
 • Muwasho hauishi
 • Hakuna sababu ya dhahiri ya kuwepo huo muwasho

Mara nyingi mgonjwa anaweza kutathmini na kutambua ni nini kinachosababisha muwasho bila msaada wa daktari. Jaribu kutafuta sababu inayoweza kusababisha muwasho ukiwa nyumbani.

Wakati mwingine ni rahisi sana kwa mzazi kugundua sababu ya kuwashwa mtoto. Kuangalia kwa karibu ngozi kutakusaidia kutambua kama umeumwa na mdudu, upele, ukavu wa ngozi, au  ukurutu. Mara nyingi sababu ya kuwashwa iko wazi na dhahiri, kama vile kuumwa na mbu.

Hakikisha unamwona daktari mapema iwezekanavyo kwa uchunguzi, kama haujui sababu ya muwasho na unarudi mara kwa mara , kama unawashwa mwili mzima ,au una mabaka mwilini kila mara. Kuwashwa mwili kusiko na sababu inayojulikana kunaweza kuwa dalili ya ugonjwa hatari.

Uchaguzi wa matibabu

Kama muwasho ni mkali sana au unadumu kwa muda mrefu, ni muhimu kuonana na mtoa huduma wa afya kwa ajili ya utambuzi na matibabu.

Wakati huo huo, unaweza kuchukua hatua kadhaa ili kusaidia kukabiliana na muwasho:

 • Epuka kukuna au kusugua eneo linalowasha.
 • Hakikisha kucha zako ni fupi ili kuepuka kuchuna ngozi unapojikuna.
 • Vaa nguo za kuzuia baridi au mwanga, na vaa nguo zisizobana unapolala
 • Epuka kuvaa nguo zinazokwaruza kwaruza, hasa pamba, katika eneo lenye muwasho.
 • Oga kwa kutumia maji ya vuguvugu na sabuni kidogo.
 • Jipake losheni kulainisha na kupunguza ukavu wa ngozi
 • Ukavu wa ngozi ni chanzo kikubwa cha muwasho
 • Kama eneo linawasha sana unaweza kuweka kitambaa chenye barafu au ubaridi.
 • Epuka kukaa sana karibu na moto au joto kali.
 • Fanya shughuli nyingi mchana ili usiufikirie muwasho na kukuchosha sana ili ulale vizuri usiku
 • Unaweza kujaribu kutumia dawa zinazouzwa duka la dawa kama vile antihistamines mfano diphenhydramine, lakini uwe makini na madhara yanayoweza kutokana na dawa mfano usingizi.
 • Jaribu cream ya hydrocortisone kwenye sehemu zinazowasha .

Vyanzo

http://www.nlm.nih.gov/medlineplus/ency/article/003217.htm

 • Share:

Leave Your Comment