KUZAMA KWENYE MAJI: Nini cha kufanya

Maelezo ya jumla

Kuzama kwenye maji humaanisha kuwa mtu karibia afie ndani ya maji kwa sababu ya kushindwa kupumua ndani ya maji. Kama mtu ameokolewa baada ya tukio la kuzama kwenye maji, anahitaji huduma ya kwanza haraka na matibabu.

Ni zipi dalili za kuzama kwenye maji?Kuzama kwenye maji

Dalili za kuzama kwenye maji ni pamoja na:

 • Kuvimba au kujaa tumbo
 • Kubadilika kwa rangi ya uso, hasa midomo kuwa ya bluu
 • Maumivu ya kifua
 • Ngozi kuwa ya baridi na iliyofifia
 • Kuchanganyikiwa
 • Kukohoa makohozi yenye rangi ya pink
 • Kutokutulia
 • Uchovu
 • Kushindwa kupumua
 • Kupumua kwa kutapatapa
 • Kupoteza fahamu
 • Kutapika

Ni nini husaabisha mtu kuzama kwenye maji?

Zifuatazo ni baadhi ya sababu zinazoweza kusababisha mtu kuzama kwenye maji;

 • Kujaribu kujiua
 • Kupigwa, kupata jeraha au degedege ukiwa ndani ya maji
 • Kunywa pombe/ kulewa ukiwa ndani ya mtumbwi au ukiwa unaogelea
 • Kudumbukiwa kwenye maji, hasa kama umesimama juu ya barafu iliyoganda juu ya maji
 • Kushidwa kuogelea au kushtuka wakati wa kuogelea
 • Kuwaacha watoto wadogo bila uangalizi wanapokuwa karibu na maji au bwawa la maji

Ni wakati gani unahitaji kuomba msaada wa kitabibu?

Kuzama kwenye maji
Kumpulizia pumzi

Kama huwezi kumuokoa mtu anayezama kwenye maji bila kujiweka hatarini, omba msaada haraka sana. Kama umefunzwa na unaweza kumuokoa mtu anayezama, jaribu kumuokoa.

Wagonjwa wote walio zama kwenye maji wanapaswa kuonana na daktari. Hata kama mtu huyo ameamka haraka au baada ya kutolewa kwenye maji na anajisikia vizuri, matatizo ya mapafu yanaweza kutokea baadae. Uwiano wa maji na madini yaliyopo mwilini unaweza kuwa umevurugika, na majeraha mengine yanaweza kuwepo.

Uchaguzi wa matibabu

Mtu anapokuwa anazama kwenye maji;

 • Usijiweke kwenye hatari. Usiingie kwenye maji au kutembea kwenye barafu nyepesi iliyoganda juu ya maji, mpaka umehakikisha kuwa ni salama
 • Tumia mti mrefu au kichana cha mti ili mtu huyo akishike au mtupia Kamba ambayo imefunga kwenye kitu kinachoelea, kama vile mviringo wa kuokolea watu “life ring” au “life jacket”.
 • Kama umepata mafunzo ya uokoaji, fanya hivyo haraka kama unadhani kuwa haitakusababishia madhara yoyote
 • Kumbuka kuwa, watu waliodumbukia kwenye maji ya barafu wanaweza kushindwa kushikilia vitu vilivyo karibu yao wanapokuwa wakivutwa kwenda sehemu salama.

Kama upumuaji wa mtu huyo umesimama, unaweza kumpulizia pumzi haraka iwezekanavyo. Hii huwa inamaanisha unaweza kuanza kumpa pumzi kabla haujamtoa kabisa ndani ya maji.

Endelea kupulizia pumzi mtu huyu kila baada ya sekunde kadhaa huku ukimpeleka sehemu iliyo kavu. Baada ya kufika nchi kavu, anza kubonyeza kifua chake na kufnaya CPR. Kwa usaidizi wa kujifunza kuhusu CPR, Jifunze hapa. (Makala hii bado inaandaliwa)

Kuzama kwenye maji
CPR

Wakati wote, kuwa makini unapomhamisha mtu baada ya kuzama kwenye maji. Fikiria kuwa mtu huyu anaweza kuwa na jeraha kwenye shingo au ut wa mgongo, na epuka kuzungusha au kukunjwa shingo yake. Weka kichwa na shingo vitulie kabisa wakati wa CPR na unapomuhamisha mgonjwa. Unaweza kukifunga kichwa kwa kutumia tape wenye machela ngumu au unaweza kuweka taulo zilizokujwa vizuri pembeni mwa kichwa.

FUATA HATUA ZIFUATAZO

 • Toa huduma ya kwanza kwa majeraha mengine hatari aliyonayo
 • Jaribu kumtuliza mgonjwa. Omba msaada wa kitabibu haraka
 • Mvue nguo zote za baridi na mfunike kwa nguo ili kumtia joto
 • Mtu huyu anaweza kukohoa au kupata shida kupumua baada ya upumuaji kurejea

Mviringo wa kuokolea

USIFANYE YAFUATAYO

 • USIJARIBU kuogelea na kwenda kumuokoa mwenyewe ,isipokuwa kama umepata mafunzo ya uokoaji.
 • USIJARIU kuingia kwenye bahari au maji yaliyochafuka yanayoweza kukuweka hatarini
 • USIJARIBU kwenda kumuokoa mtu kwenye barafu kama unaweza kumfikia kwa mkono au kwa kumpatia kitu akashika
 • Kumminya kifua kutoka nyuma “Heimlich maneuver” sio sehemu ya utaratibu wa kuokoa mtu aliyezama kwenye maji. USIJARIBU kufanya Heimlich maneuver isipokuwa baada ya kujaribu kupulizia pumzi mara kadhaa na unadhani kuwa kuna kitu kinaziba njia yake ya hewa. Kufanya Heimlich maneuver kunaongeza uwezekano wa mtu kutapika , na matapishi yanaweza kumpalia na kuingia kwney njia ya hewa.

Kuzuia kuzama kwenye maji

Kufanya mambo yafuatayo kunapunguza uwezekano wa kuzama kwenye maji:

 • Epuka kunywa pombe unapokuwa unaogelea au kukiwa ndani ya mtumbwi
 • Kuzama kwenye maji kunaweza kutokea kwenye chombo chochote chenye maji. Usiache maji kwenye vyombo (kwenye mabeseni, ndoo, sehemu za kuogea, vyombo vya maji). Funika matundu ya vyoo ili kulinda usalama wa watoto.
 • Weka uzio kuzunguka mabwawa ya kuogelea “pools” na weka mlango unaweza kufungwa kwa nje.
 • Kama mtoto wako haonekani, kagua bwawa la kuogelea haraka
 • Kamwe usiruhusu watoto kuogelea bila uangalizi, hata kama wanaweza kuogelea vizuri.
 • Kamwe usiruhusu watoto, hata kwa sekunde moja kuwa sehemu usipowaona wanapokuwa karibu na bawawa la kuogelea au mto, ziwa au bahari. Kuzama kwenye maji kumetokea mara nyingi kwa sababu mzazi aliondoka kwa dakika moja tu kwenda kupkea simu au kufungua mlango

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/patientinstructions/000387.htm

 

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi