KUZIBA KWA NJIA YA HEWA

KUZIBA KWA NJIA YA HEWA

 • August 19, 2020
 • 0 Likes
 • 195 Views
 • 0 Comments

Maelezo ya jumla

Kuziba kwa njia ya hewa (airway obstruction)  hutokana na uzibe kwenye njia ya hewa, uzibe huu unaweza kutokea kwenye koo (trachea) , zoloto (laryngeal), au koromeo (pharyngeal).

Je! Ni nini dalili za kiziba kwa njia ya hewa?

Dalili hutofautiana kulingana na sababu, lakini dalili zifuatazo hupatikana katika aina zote bila kujali sababu ya kuziba kwa njia ya hewa.

Hizi ni pamoja na:

 • Kupaliwa.
 • Kupata shida kupumua.
 • Kutapia hewa (gasping for air)
 • Kukorota (wheezing), kupiga mluzi, au sauti nyingine zinazoonesha mgonjwa anapata shida kupumua.
 • Rangi ya ngozi kuwa ya bluu
 • Kufadhaika au kuwa na wasiwasi mwingi.
 • Hofu
 • Kuchanganyikiwa
 • Fahamu ya mgonjwa huanza kupungua 
 • Kupoteza fahamu

Ni nini kinachosababisha kuziba kwa hewa?

Sababu za kuziba kwa njia ya hewa ni pamoja na:

 • Athari zitokanazo na mzio (allergy), ambazo husababisha koo kuvimba mpaka kuziba kabisa njia ya hewa, hii ni pamoja mzio unaotokea baada ya kuumwa na nyuki, kula njugu (peanuts) ,kutumia antibiotics kama penicillin, na dawa za kupunguza shinikizo la juu la damu (ACE inhibitors).
 • Kuunguzwa na kemikali, hasa baada ya kuvuta hewa au kunywa kemikali
 • Kifaduro (croup)
 • Kuvimba kwa kidakatonge (epiglottitis) –  husababishwa na maambukizi kwenye kidakatonge,kidakatonge hutenganisha njia ya hewa na ya chakula
 • Jeraha la moto linalotokea baada ya kupumua moshi wa moto
 • Vitu vinaweza kukwama kwenye njia ya hewa – vitu kama njugu, vipande vya chakula, vifungo,sarafu na hata vitu vidogo vya kuchezea watoto
 • Maambukizi ya virusi au bakteria
 • Jipu la tukwa/findo (peritonsillar abscess)
 • Jipu kwenye koromeo
 • Saratani ya koo
 • Jeraha
 • Matatizo ya viungo vya sauti (vocal cords)

Wakati gani utafute matibabu ya haraka?

Kikwazo chochote kwenye njia ya hewa ni dharura. Ni wazo zuri kujifunza kutoa huduma ya kwanza kwa kutumia mbinu kama Heimlich maneuver. Kuziba kwa njia ya hewa huanza taratibu kwa badhi ya magonjwa ,na hii hutoa fursa ya kumfikisha mgonjwa hospitalini. Lakini kwa magonjwa mengine hali hii hutokea ghafla, na itahitajika kumsaidia mgonjwa kabla ya kufika hospitalini.

Utambuzi

Uchunguzi wa mwili unaweza kuonesha:

 • Kupungua kwa sauti ya mapafu (decreased breath sounds)
 • Kupumua haraka haraka, kwa pumzi fupi fupi, au kupumua polepole sana.

Vipimo vifuatavyo vinaweza kufanyika, japo si kila mara:

 • Bronchoscopy – hii ni bomba nyembamba yenye kamera, inayoingizwa kwenye njia ya hewa ili kuchunguza kikoromeo (bronchi)
 • Laryngoscopy –hii ni bomba nyembamba yenye kamera, inayoingizwa kwenye njia ya hewa ili kuchunguza zoloto (larynx)
 • X-raysEksirei ya kifua inaweza kumsaidia daktari kutambua ni wapi na nini kilichoziba njia ya hewa

Uchaguzi wa matibabu

Kama njia ya hewa ya mtu imeziba kabisa na hawezi kabisa kuzungumza au kupumua, Heimlich manoeuvre inaweza kuokoa wa maisha.

Matibabu hutegemea sababu ya kuziba kwa njia ya hewa.

Vitu vilivyokwama kwenye njia ya hewa vinaweza kuondolewa kwa laryngoscope au bronchoscope. Bomba linaweza kuingizwa kwenye njia ya hewa (endotracheal tube au nasotracheal tube). Wakati mwingine upasuaji  hufanywa moja kwa moja kwenye njia ya hewa (tracheostomy au cricothyrotomy).

Nini cha kutarajia ?

Matibabu yakifanyika haraka mara nyingi hufanikiwa. Lakini, hali hii ni hatari na inaweza kutishia maisha, hata kama inatibiwa.

Matatizo yanayoweza kutokea

Kama kizuizi kwenye njia ya hewa hakitatolewa mapema kinaweza kusababisha:

 • Kuharibika kwa ubongo
 • Kushindwa kabisa kupumua
 • Kifo

Kuzuia

Kuzuia tatizo hili, hutegemea sababu ya kuziba kwa njia ya hewa. Mbinu zifuatazo zinaweza kusaidia kuzuia kuziba kwa njia ya hewa:

 • Kula chakula polepole na tafuna chakula mpaka vizuri kabla ya kumeza.
 • Usinywe pombe nyingi sana kabla au wakati wa kula.
 • Weka vitu vidogo vidogo mbali na watoto wadogo.
 • Hakikisha meno bandia (dentures) yamekaa vizuri na yanakufaa vizuri.

Vyanzo

http://www.nlm.nih.gov/medlineplus/article/000067.htm

 • Share:

Leave Your Comment