Maeleozo ya jumla
Kila mmoja wetu anapatwa na kwikwi mara moja moja- unajikuta unavuta hewa kwa haraka na kwa mshtuo, kunakosababishwa na kuvutika kwa kiwambo kinachosaidia upumuaji (diaphragm). Japo mara nyingi kwikwi inatokea bila sababu yoyote, baadhi ya sababu za kawaida ni pamoja na kula chakula kuzidi kiasi au kula haraka haraka sana, kula chakula chenye pilipili au viungo vingi sana, kula chakula cha moto sana au cha baridi sana, kunywa vinywaji vya viwandani vyenye carbon, au kunywa pombe. Kuvuta sigara au mambo ya kihisia kama vile mshtuko au woga ulipitiliza unaweza kusababisha kwikwi, lakini pia mabadiliko ya ghafla ya joto yanaweza kusababisha pia. Kwikwi mara nyingi inadumu kwa dakika kadhaa tu. Kama kwikwi itaendelea kwa siku kadhaa inaweza kuwa dalili kuwa una ugonjwa mwingine na inaweza kusababish ukapata shida kulalana hata kupungua uzito wa mwili
Unachoweza kufanya ukiwa na kwikwi
Kwikwi huwa inaisha tu yenyewe lakini kama unataka iishe mapema. Unaweza kujaribu kufanya moja ya mambo yafuatayo:
- Jaribu kushikilia pumzi yako kwa kadri unavyowezaau toa na kuvuta pumzi haraka haraka. Au unaweza kupumua ndani ya mfuko. Chukua mfuko liotengenezwa kwa karatasi (usiwe wa plastic), weka kuzunguka mdomo wako na pua, na kisha vuta pumzi ndani na kutoa nje kama mara kumi hivi. Pumzi ambayo inakuwa imetolewa huwa na kiwango kikubwa cha kabonidioksidi kuliko kawaida, na kuivuta ndani tena kutoka kwenye mfuko inasaidia kiwambo kinachosaidia upumuaji ku-relax na kuzuia kwikwi.
- Piga pafu maji ya barafu au tafuna kipande cha barafu na mumunya barafu iliyopondwa, kwa dakika 10-15.
- Kula kipande kikavu cha makate
- Weka sukari kwenye sehemu ya nyuma ya ulimi kwa kutumia kijiko na kisha imumunye taratibu
- Kama kuna kipande cha limao kimumunye au unaweza piga pafu kiwango kidogo cha siki (vinegar)
- Vuta kwa nguvu ulimi wako au jaribu kugusa sehemu ya nyuma ya ulimi wako kwa kutumia kidole
- Kaa kwenye kiti au kwenye saafu na kisha vuta miguu yako kuelekea kwenye kifua chako huku ukiegemea mbelec(lean forward)
- Unaweza ukamwambia mtu mwingine akakushtua (startle). Hii pekee mara chache inaweza kuondoa kabisa kwikwi
Ukiwa na kwikwi tafuta msaada wa daktari kama:
- Kama unapata kwikwi ambayo imedumu kwa muda wa zaidi ya masaa 24
- Kama unapata kwikwi mara kwa mara
Leave feedback about this