Last Updated on October 12, 2023 by Dr Mniko
Moyo
Moyo ni pump ndogo inayolingana na ngumi inayosukuma damu mwilini
Mfumo wa kuzungusha damu mwilini umeundwa na mishipa ya damu inayotoa na kupeleka damu kwenye moyo.
Mishipa ya ateri hubeba damu kutoka kwenye moyo na mishipa ya vena hurudisha damu kwenye moyo.
Damu inayozunguka mwilini hupeleka oksijeni kwenye seli zote mwilini na kuondoa hewa chafu ya carbondioxide mwilini.
Oksijeni inafyonzwa na kuingia kwenye damu kupitia vifuko vidogo vya hewa vinavyopatikana kwenye mapafu vinayoitwa alveoli
Wakati oksijeni inapoingia ndani, kabonidioksaidi inapenya na kutoka nje pia.
Moyo wenye afya ni muhimu kwa maisha ya kila mmoja.
Linda moyo wako
- Kula mlo kamili
- Dhibiti uzito wa mwili
- Fanya mazoezi, angalau dakika 150 kwa wiki
- Usivute sigara
- Punguza matumizi ya pombe
- Punguza msongo wa mawazo
Leave feedback about this