MAJI YA KUNYWA: Kutakasa,kuhifadhi na kutumia

Namna sahihi ya kutakasa majikuchuja maji

  1. Kama maji yana vumbi, udongo, majani au mchanga acha yatuame na uchafu utulie kisha chuja maji kwa kutumia kitambaa kisafi.
  2. Chemsha maji ya kunywa, kupikia au kunywea dawa kwa muda mrefu mpaka yatoe mapovu makubwa. Chemsha hadi yachemke na yaendelee kuchemka kwa dakika tano. Acha yapoe.
  3. Kutibu kwa kuweka dawa ya Water Guard/klorini kidonge kimoja kwa kila dumu moja la lita 20. Tikisa ndoo au gudulia, kisha acha maji yatulie kwa dakika 30.

Namna sahihi ya kuhifadhi na kutumia maji

  1. Hifadhi maji yaliyochemshwa na kuchujwa katika chombo safi chenye mfuniko unaofunga vizuri.
  2. Chota maji kwa kutumia upawa/kikombe chenye mshikio mrefu na safi au mimina moja kwa moja kutoka katika chombo cha kutunzia maji na funika vizuri ili kuhakikisha hakuna uchafu unaoingia kupitia kushika kwa mikono au kikombe.

Vyanzo

https://www.tfnc.go.tz/publications/9

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi