Magonjwa ya ndani ya mwili

MAPAFU KUJAA MAJI : Dalili, Sababu, Matibabu

mapafu kujaa maji

Last Updated on October 13, 2023 by Dr Mniko

Maelezo ya jumla

Mapafu kujaa maji (pulmonary edema) ni hali isiyo ya kawaida ya maji kujaa kwenye mapafu na kusababisha kupumua kwa shida.

Je! Nini dalili za mapafu kujaa maji?    

  • Wasiwasi   
  • Kukohoa  
  • Kupumua kwa shida
  • Kutokwa jasho sana 
  • Kuhisi uhitaji mkubwa wa hewa au mtu kujihisi kama anazama majini  (ikiwa hili litatokea ghafla mtu akiwa usingizini ataamka kutoka usingizini na kukaa kitako ili aweze kuvuta pumzi vizuri.
  • Kukoroma au sauti ya mbubujiko wa maji kifuani akipumua
  • Rangi ya ngozi iliyofifia/inayoonekana dhaifu
  • Mgonjwa hatulii, huwa na kiwewe
  • Kupumua kwa shida
  • Kupumua kwa shida kunakoongezeka mgonjwa akilala chali – Mgonjwa wa aina hii atahitaji mito kadhaa ili aweze kulala vizuri.
  • Kukorota

Dalili za ziada zinazoweza kuhusishwa na hali hii:    

  • Kukohoa damu au kutoa mapovu yenye damu mdomoni
  • Fahamu ya mgonjwa huanza kupungua na hatimaye anaweza kupoteza fahamu kabisa
  • Mgonjwa hushindwa kuzungumza na kumaliza sentensi bila kuvuta pumzi
  • Kutanuka kwa pua

Ni nini kinachosababisha mapafu kujaa maji?mapafu kujaa maji

Kushindwa kwa moyo kufanya kazi (heart failure)  ndio sababu kuu inayosababisha mapafu kujaa maji.

Moyo unaposhindwa kusukuma damu, shinikizo kwenye mishipa ya damu inayopita kwenye mapafu huongezeka. Shinikizo linapoongezeka kwenye mishipa hii ya damu, maji huchuja na kuingia kwenye aliveoli (vimfuko vya kuchujia hewa vinavyopatikana kwenye mapafu) za mapafu. Maji haya yanapojaa kwenye aliveoli, yanavuruga harakati za kawaida za mwili kuchukua okisijeni kupitia mapafu na kusababisha kupumua kwa shida.

Mapafu kujaa maji kunaweza kusababishwa na uharibifu wa moja kwa moja kwenye mapafu, kama vile

  • Uharibifu wa mapafu unaosababishwa na
    • Kuvuta gesi yenye sumu
    • Maambukizi makali,
    • Kama athari ya kutumia madawa,
    • Kama matokeo ya jeraha/kuumia kifuani
    • Kujaa kwa maji mwilini kama matokeo ya kushindwa kwa figo kufanya kazi
    • Kufanya mazoezi kwenye mwinuko, eneo lilo juu sana kutoka usawa wa bahari.
    • Mapafu kujaa maji kunaweza pia kusababishwa na shambulizi la moyo, kuharibika kwa vali za moyo  au ugonjwa wowote utakaosababisha kulegea au kukakamaa kwa misuli ya moyo.

Utambuzi wa mapafu kujaa maji

Mtoa huduma ya afya atafanya uchunguzi wa mwili na kutumia kifaa (stethoscope) kusikiliza mapafu na moyo.

Yafuatayo yanaweza kupatikana:    

Vipimo vinavyoweza kufanyika ni pamoja na:    

  • Complete blood count (CBC)– Kipimo hiki hufanyika ili kutambua upungufu wa damu na maambukizi
  • Vipimo vingine vya damu hufanyika ili kupima kazi ya figo
  • Oximetry – kipimo hiki hupima kiwango cha oksijeni kwenye damu ,kwa mgonjwa mwenye maji kwenye mapafu kiwango cha oksijeni huwa chini
  • Eksirei ya kifua inaweza kuonesha maji yaliyojaa ndani ya mapafu au moyo uliopanuka
  • Electrocardiogram (ECG) –kipimo hiki hufanyika ili kutambua mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida au kupata ushahidi wa mshtuko wa moyo.
  • Echocardiogram– Hii ni ultrasound ya moyo, hutumia mawimbi ya sauti ili kutengeneza picha ya moyo kwenye computer, kipimo hiki humsaidia daktari kuona kama kuna msuli wa moyo uliolegea, vali za moyo zilizoharibika au kama kuna maji yaliyouzunguka moyo.

Uchaguzi wa matibabu

Oksijeni hutolewa kupitia baraoa maalumu ya uso au vijibomba vidogo vya plastiki vinavyowekwa puani (nasal prongs). Mpira wa kukusaidia kupumua unaweza kuwekwa kwenye njia yako ya hewa.Wakati mwingine mashine ya kukusaidia kupumua (ventilator) inaweza kuhitajika.

Sababu ya kujaa kwa maji kwenye mapafu inapaswa itambuliwe haraka na kutibiwa mapema. Kwa mfano, kama shambulizi la moyo limesababisha hali hiyo, moyo lazima utibiwe na uimarishwe.

Daktari anaweza kukupatia vidonge vya kutoa maji kama vile furosemide (Lasix), vinaweza kutolewa ili kusaidia kuondoa maji ya ziada mwilini. Madawa ya kuimarisha misuli ya moyo, kudhibiti mapigo yake, au kupunguza mzigo wa moyo, yanaweza pia kutolewa.

Madawa ya kuepuka mapafu kujaa maji

Wagonjwa waliotambuliwa kuwa na mapafu yaliyojaa maji wanapaswa kuepuka kutumia dawa zifuatazo:    

  • Mannitol

Ikiwa umegunduliwa kuwa na mapafu yaliyojaa maji, wasiliana na daktari wako kabla ya kuanza au kuacha dawa yoyote.

Nini cha kutarajia ?

Wagonjwa wengine wanaweza kuhitaji kutumia mashine ya kuwasaidia kupumua kwa muda mrefu, na hii inaweza kusababisha uharibifu wa tishu za mapafu.

Kama mzunguko wa damu na okisijeni mwilini hautarejea mapema mwilini, inaweza kusababisha figo kushindwa kufanya kazi na uharibifu wa viungo vinginevya mwili. Ikiwa mgonjwa hatatibiwa mapema,hali hii inaweza kutishia maisha.

Matatizo yanayoweza kutokea

Wagonjwa wengine wanaweza kuhitaji kutumia mashine ya kuwasaidia kupumua kwa muda mrefu sana. Na kama hali hii haitatibiwa, hali inaweza kuwa mbaya sana.

Vyanzo

http://www.nlm.nih.gov/medlineplus/ency/article/000140.htm

    • 1 year ago (Edit)

    Thank you for your explanation, symptoms and cancels on the issue of pulmonary oedema. Nice we would be so happy next time for your assistance. Be blessed all of you..

Leave feedback about this

  • Quality
  • Price
  • Service

PROS

+
Add Field

CONS

+
Add Field
Choose Image
Choose Video
X