MAPIGO YA MOYO KWENDA MBIO

MAPIGO YA MOYO KWENDA MBIO

 • February 19, 2021
 • 0 Likes
 • 97 Views
 • 0 Comments

Maelezo ya jumla

Kwa kawaida moyo unapopiga huwa hatuna ufahamu au kuhisi kuwa unapiga, lakini unapoanza kwenda mbio au kupiga isivyo kawaida unahisi unaenda kwa kasi au unapiga isivyo kawaida. Kwa wakati mwingi hali hii ni ya kawaida. Sababu za hali hii ni pamoja na mazoezi, furaha, msongo, wasiwasi na kutumia viamsha mwili kama vile kahawa yenye kafeini au sigara yenye nikotini. Katika hali ya kawaida mapigo ya moyo huenda mbio kwa sekunde au dakika kadhaa na baadae hupungua na hutokea bila kuwepo kwa dalili nyingine yoyote. Mapigo ya moyo yanapoenda mbio sio tatizo la kutia wasiwasi, lakini kama yakianza kwenda mbio bila sababu ya msingi au yakitokea sambamba na dalili nyingine au kama yataendelea kupiga kwa muda mrefu, yanaweza kuwa yanashiria kuwa kuna tatizo.

Mwone daktari kama

Tafuta usaidizi wa kitabibu haraka sana kama:

Panga kumwona daktari kama:

 • Ni vizuri kupanga kumwona daktari mapema iwezekanavyo kama unaona mapigo yanapiga haraka kwa muda mrefu sana na/au unahisi yanaruka ruka mapigo / yanasita kupiga

Unachoweza kufanya wewe mwenyewe

Kama mapigo ya moyo yanaenda mbio mara kadhaa, jaribu kufanya mambo yafuatayo ili kutambua sababu yake ili ushughulike nayo

 • Tunza kumbukumbu kwenye kitabu, andika unapoona mapigo yanaenda kasi au yanapiga isivyo kawaida na vyakula ulivyokula au kunywa, mazoezi uliyofanya, kama una msongo, au sababu nyingine ambazo unaweza kuwa nazo kwa wakati huo
 • Kama una msongo, jaribu kufanya mazoezi ya upumuaji ‘’deep breath exercise’’ na kutumia mbinu za kulegeza misuli ‘’muscle relaxation technique’’. BONYEZA HAPA KUJIFUNZA MBINU HIZO
 • Pata usingizi wa kutosha. Kuchoka kunakotokana na kukosa usingizi wa kutosha kunaweza kusababisha au kuongeza ukali wa tatizo
 • Punguza matumizi ya vinywaji vyenye kafeini. Vinywaji vyenye kafeini ni pamoja na kahawa, chai na cola. Punguza matumizi mpaka vikombe viwili au chini ya hapo kwa siku, lakini punguza taratibu, ukipunguza haraka unaweza kupata maumivu ya kichwa.
 • Kabla haujatumia madawa ya kudhibiti kikohozi au za kutibu mafua, angalia kwenye ‘’label’’ vizuri. Baadhi ya madawa ya mafua yanaweza kusababisha moyo kwenda mbio.
 • Punguza matumizi ya pombe; matumizi makubwa ya pombe yanaweza kusababisha mapigo ya moyo kwenda mbio
 • Jaribu kuacha kuvuta sigara, kwa sababu ‘’nicotine’’ inaweza kuongeza kasi ya mapigo ya moyo na kusababisha moyo kwenda mbio
 • Usitumie madawa ya kulevya kama vile ‘’amphetamines’’ au ‘’cocaine’’, kwa sababu madawa haya yanaweza kusababisha moyo kwenda mbio

Mwone daktari kama

Panga kumwona daktari kama:

 • Bado unaendelea kupata matukio ya mapigo ya moyo kwenda mbio au moyo kupiga isivyo kawaida japo umejaribu kupunguza au kuondokana na vitu vinavyoweza kusababisha
 • Unaona kuna dalili nyingine zinaambatana na tatizo hili, kama vile kupungua uzito au uchovu

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/003081.htm

 • Share:

Leave Your Comment