MAUMIVU MDOMONI AU ULIMI:Dalili,sababu,matibabu

Maelezo ya jumla

Kuna sababu kadhaa zinazoweza kusababisha upate maumivu mdomoni au ulimi. Utando ute unaofunika mdomo na ulimi unaweza kusumbuliwa na kusababisha uvimbe kwa kula vyakula ambavyo ni vya moto, vyenye pilipili sana au vinavyowasha au hata vinywaji vya moto au kwa sababu ya matumizi yaliyopitiliza ya madawa ya kusukutua, kunywa pombe sana au kuvuta sigara.
Ulimi unaweza kuwa na maumivu, ukaonekana mwekundu na uwezo wa kuonja ukapungua au kupotea kabisa. Unaweza pia kuwa na maumivu mdomoni kama utauuma ulimi au kingo za shavu kwa bahati mbaya au kama una jino lililoharibika au kama una jino bandia ambalo halikai vizuri mdomoni. Sababu nyingine ni pamoja na vidonda mdomoni, matatizo ya fizi, na maambukizi ya kinywa kama vile fangasi. Kwa mara chache, maumivu ya mdomoni yanaweza kuwa yamesababishwa na shida kubwa zaidi.

Mwone daktari kama una maumivu mdomoni au ulimi

Panga kumwona daktari kama:

 • Kama unazo dalili za maambukizi kama vile utando mweupe mweupe kwenye kuta za mdomo
 • Kama unajihisi uchovu, hauli vizuri chakula au unaona unapungua uzito
 • Kama unaona mdomo wako na macho yanakuwa makavu muda wote

Unachoweza kufanya mwenyewe kama una maumivu mdomoni au ulimi

Unaweza kutumia njia zifuatazo ukiwa nyumbani ili kupooza mdomo na ulimi uliosumbuliwa

 • Kunywa maji angalau glass 6-8 kwa siku. Vinywaji baridi vinapunguza ukakasi. Usinywe pombe au kuvuta sigara –vyote hivi vinaweza kuutia ukakasi mdomo
 • Jaribu kutengeneza mchanganyiko wa maji na chumvi kisha sukutua. Chukua chumvi nusu kijiko na uiloweke kwenye kikombe kimoja cha (250ml), maji inabidi yawe ya uvuguvugu. Sukutua kwa kutumia maji haya mchana, hasa baada ya kumaliza kula. Sukutua kwa angalau sekunde 30 na kisha yateme.
 • Usiache kupiga mswaki meno yako, piga mswaki taratibu na polepole kwa kutumia mswaki laini
 • Kula kidogo kidogo, kula mara kwa mara milo laini kama vile viazi vilivyotwangwa, ndizi zilizoiva vizuri, yogurt. Epuka kula vyakula vyenye pilipili au vinavyowasha mdomo, epuka kula vyakula vigumu, vyenye aside au vyenye chumvi nyingi
 • Unaweza pia kutumia madawa ya kutuliza maumivu, yapo madawa ya kusukutua, ‘’spray’’ ambazo husaidia kupunguza kuvimba na kupunguza maumivu. Ongea na mtaalamu wa madawa katika duka la dawa atakupatia itakayokufaa
 • Kama unaona mdomo wako unakuwa mkavu sana, tafuna ‘’gum’’ ili kuchachawisha mate yako yatoke
 • Kama una meno ambayo yameunjika na yanakusababishia majeraha au kama una meno ya bandia ambayo hayakai vizuri mdomoni, mwone daktari wa meno akusaidie kuyaweka sawa

Mwone daktari kama una maumivu mdomoni au ulimi

Panga kumwona daktari kama

 • Ni vizuri kumwona aktari kama unaona maumivu yanazidi zaidi au kama unaona hayapungui baada ya siku kadhaa za kutumia njia zilizoelekezwa hapa

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/003059.htm
https://medlineplus.gov/ency/article/003047.htm

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi