Magonjwa ya wanawake

MAUMIVU WAKATI WA HEDHI:Sababu,matibabu,kuzuia

Last Updated on October 13, 2023 by Dr Mniko

Maelezo ya jumla

Maumivu wakati wa hedhi ni tatizo linalowapata wanawake wengi

 • Hedhi ni hali ya kawaida kwa wanawake, wanawake hutokwa na damu ukeni kwa siku kadhaa na mara nyingi hutokea kila mwezi mara moja.
 • Hali hii huwapata wanawake walio katika umri wa kuzaa, yaani wale ambao wamekwisha vunja ungo tayari.
 • Mzunguko wa hedhi ambao ni wa kawaida ni ule ambao huanza kila baada ya siku 21-35. Kama mzunguko wako unaanza kila baada ya siku 21-35 ni wa kawaida.
 • Wanawake wengi wamekua wakipata maumivu makali sana wakati wa hedhi. Maumivu ya tumbo huwa ya kukaza au kunyonga chini ya kitovu.
 • Maumivu haya yanaweza kuwa makali mpaka kuingilia mfumo wa maisha ya mwanamke. Wanawake wa aina hii hushindwa kabisa kufanya shughuli zao za kila siku mpaka hedhi itakapoisha.

Ni nini husababisha maumivu wakati wa hedhi?

 • Wakati wa hedhi mji wa mimba hunywea kutoka kwenye umbile lake la kawaida na kuwa mdogo, hili hufanyika ili kuondoa kuta za mji wa mimba ambazo zilitengenezeka kwa ajili ya kupokea mimba, kuta hizi zinapokuwa zikipukusa ndio damu hutoka kila mwezi kama mimba haijatungika.
 • Homoni inayoitwa prostaglandin hutolewa na kusababisha maumivu, na kadiri inapotolewa kwa wingi ndivyo na maumivu huongezeka zaidi
 • Pia, kunywea kwa mji wa mimba kukizidi sana kunaweza kusababisha kugandamizwa kwa mishipa ya damu inayosambaza damu kwenye mji wa mimba na kusababisha kuziba kwa mishipa hii, baadae maumivu yanaweza kutokea.
 • Kama kuna uvimbe kwenye mji wa mimba.
 • Kama shingo ya kizazi ni nyembamba sana.
 • Maambukizi kwenye mfumo wa uzazi

Dalili za maumivu wakati wa hedhi

Nani yuko kwenye hatari zaidi ya kupata maumivu wakati wa hedhi?

 • Kama kuna historia ya tatizo hili kwenye familia
 • Wanawake walio na umri chini ya miaka 30
 • Wanawake ambao hawajabahatika kupata mtoto
 • Wanawake ambao waliwahi kuvunja ungo, yaani chini ya miaka 11
 • Wanaovuta sigara

Wanaotokwa na damu nyingi wakati wa hedhi na walio na mizunguko isiyo linganifu, yaani inayobadilika badilika.

Wakati gani umwone daktari?

Maumivu ya hedhi yanaweza kuwa ya kawaida na usihitaji kuonana na daktari, lakini pale yanapokuwa na moja ya dalili hizi ni vizuri kuonana na daktari:

 • Maumivu yanapozidi mpaka ukashindwa kufanya shughuli zako za kila siku
 • Kama una umri zaidi ya miaka 25
 • Kama una homa kali inayoambatana na maumivu.
 • Kama unapata maumivu hata baada ya kumaliza hedhi
 • Kama unatumia dawa za kutuliza maumivu na haupati nafuu

maumivu wakati wa hedhiUtambuzi

Utambuzi hufanywa na daktari na anaweza kuagiza vipimo kadhaa kadhaa:

 • Kufanya kipimo cha picha za tumbo (ultrasound) hiii husaidia kuona kisababishi cha hayo maumivu, kama ni uvimbe, au kunywea kwa mji wa mimba.
 • Kufanya hivo kunasaidia kuchagua matibabu sahihi kwa ajili ya kuondosha chanzo cha maumivu, inawezaekana kukafanyika upasuaji kwa ajili ya kuondoa uvimbe kama ndio unaosababisha maumivu.

Ufanye nini kupunguza maumivu?

Kufanya vitu vifutavyo kunaweza kusiondoshe kabisa maumivu, lakini kunaweza kupunguza ukali wa maumivu:

 • Kuoga maji ya uvuguvugu au ya moto-moto
 • Kufanya mazoezi
 • Pia, unaweza kuloweka taulo au kitambaa kwenye maji ya moto na kuweka kwenye tumbo hasa chini ya kitovu.
 • Pia, unaweza kutumia dawa za kutuliza maumivu kwa muda kama Panadol, ibuprofen,
 • Baadhi ya tafiti pia zinaonesha kuwa kutumia vitamini B1 na vitamini B6 kunaweza kupunguza maumivu kwa kiasi fulani.
 • Pia, kupunguza mawazo kunaweza kuondosha ukali wa maumivu

Angalia pia: MAMBO YA KUFANYA KUPUNGUZA MAUMIVU WAKATI WA HEDHI kujifunza zaidi

Vyanzo

https://medlineplus.gov/periodpain.html

Leave feedback about this

 • Quality
 • Price
 • Service

PROS

+
Add Field

CONS

+
Add Field
Choose Image
Choose Video
X