Magonjwa ya wanawake

KUZUIA UCHUNGU/MAUMIVU WAKATI WA KUJIFUNGUA

Kupunguza maumivu wakati wa ujauzito

Last Updated on October 12, 2023 by Dr Mniko

Uchungu/maumivu wakati wa kujifungua yatakuwa makali kiasi gani?

Hakuna njia nzuri ya kutambua maumivu yatakuwa makali kiasi gani wakati wa kujifungua. Uchungu/maumivu wakati wa kujifungua yanatofautiana kwa kila mwanamke. Baadhi ya wanawake wanahitaji dawa kidogo tu au hawahitaji kabisa kupunguza maumivu. Baadhi ya wanawake, dawa za kupunguza maumivu zinawasaidia kuweza kuhimili mchakato wa kujifungua. Wanawake ambao hutumia sana dawa za kupunguza maumivu aina ya opiods, wanaweza kupata shida kudhibiti uchungu/maumivu wakati wa kujifungua  kwa sababu mwili unakua umezizoea.

Machaguo ya kupunguza uchungu/maumivu wakati wa kujifungua ni yapi?uchunguzi/maumivu wakati wa kujifungua

Maumivu yanaweza kudhibitiwa kwa kutumia au kutotumia dawa. Mtaalamu aliyefunzwa vizuri anaweza kukusaidia kudhibiti uchungu/maumivu bila dawa kwa kukutia moyo na kukutegemeza. Baadhi ya njia nyingine za kudhibiti maumivu bila kutumia dawa ni kuloweka mwili kwenye maji (maji ya hali la joto la kawaida) au kwa kubadili mkao katika kipindi cha kwanza cha uchungu. Kusimama au kukaa kunaweza kuwa bora zaidi kuliko kulala.

Kama ukichagua kutumia dawa za kupunguza uchungu/maumivu, kuna machaguo mengi. Baadhi ya dawa za maumivu kama vile opiods, zinawekwa moja kwa moja kwenye mishipa ya damu. Kama ukichagua kuchomwa kwenye uti wa mgongo, sindano itachomwa kwenye mgongo.

Ni wakati gani napaswa kuchagua aina ya njia ya kupunguza uchungu/maumivu wakati wa kujifungua?

Kutambua machaguo uliyonayo kabla ya muda wa uchungu itasaidia mchakato wa kujifungua kwenda sawa sawa.

Madaktari na manesi wanaokusaidia wakati wa uchungu na kujifungua watakusaidia kuamua ni njia gani ya kutumia. Jipe nafasi kuchagua. Baadhi ya wanawake wanapanga kutumia dawa za kupunguza uchungu/maumivu, lakini siku inapofika wanabadilisha mawazo na kusema hawataki au wanataka. Wengine huwa hawana mpango wa kutumia dawa lakini wanabadilisha mawazo wakati wa uchungu. Haupaswi kujisikia kuwa unashinikizwa kuchagua moja au jingine.

Dawa za opioids ni nini?

Dawa za opioids ni  dawa za maumivu zinazoweza kutolea wakati wa uchungu. Kwa kawaida zinatolewa kupitia mshipa wa damu. Zinatolewa kwa kiwango kidogo na mwazoni kabisa mwa uchungu ili kupunguza madhara inayoweza kusababisha. mfano wa dawa hizi ni; meperidine, morphine, fentanyl, butorphanol, nalbuphine n.k

Je kuna tofauti ya sindano ya kuchoma kwenye uti wa mgongo(spinal) na sindano ya kwenye utando wa uti wa mgongo (epidural)

Spinal
Spinal

Sindano inayochomwa kwenye uti wa mgongo (spinal) ni sindano yenye dawa inayochomwa kwenye mgongo na sindano kutolewa mara moja baada ya dawa kuwekwa. Dawa inasababisha upate ganzi kwa muda mfupi na baadae inaisha. Mara nyingi inatumika zaidi katika taratibu ambazo daktari anajua zitachukua muda gani kuisha, kwa mfano upasuaji wa kutoa mtoto (cesarean delivery).

Sindano ya Epidural
Epidural

Sindano inayochomwa kwenye utando wa uti (epidural) wa mgongo ni mrija mdogo (mrija laini unaoweza kujikunja) unaoingizwa kwa sindano karibu na uti wa mgongo. Baada ya kuingiza, sindano inaondolewa na kubakiza mrija. Dawa inaweza kuendelea kuwekwa kupitia mrija huu kipindi chote cha uchungu. Daktari atadhibiti kiasi cha dawa kadri unavyohitaji. Epidural inapendelewa zaidi na daktari kuzuia uchungu/maumivu wakati ambapo hajui utaratibu utachukua muda gani, kwa mfano; uchungu wa uzazi.

Vipi kama nahitaji kufanyiwa upasuaji wa kutoa mtoto?

Baadhi ya wanawake wanapanga kabisa kufanyiwa upasuaji wa kutoa mtoto. Kwa kawaida, wanawake wanachomwa sindano ya kupunguza maumivu kwenye uti wa mgongo. Kama utakuwa haujapanga kufanyiwa upasuaji na ikatokea dharura, unaweza kubakia na epidural uliyonayo au daktari akaamua kukuchoma spinal. Sio kawaida kupewa sindano ya nusu kaputi (inayokusababisha ulale kabisa) kwa ajili ya upasuaji wa kutoa mtoto.

Je, sindano ya kuchomwa mgongoni (epidural na spinal) inauma?

Sehemu unayochomwa sindano unaweza kusikia maumivu kidogo. Unaweza kuhisi mgandamizo kidogo. Unaweza usijisikie vizuri, lakini kwa wanawake wengi, nafuu inayoletwa na dawa hizi inatosha kuruhusu kuumia kidogo.

Je, nitaweza kusikia tumbo likikaza na nitaweza kusukuma mtoto?

uchungu/maumivu wakati wa kujifungua

Kama ukichomwa sindano ya epidural, unaweza kujikuta unasukuma kwa muda mrefu zaidi.

Kuchomwa sindano za maumivu haziongezi hatari ya kufanyiwa upasuaji wa kutoa mtoto au mtoto kuvutwa kwa mikasi au vacuum.

Kuna madhara yoyote ya dawa hizi za kupunguza uchungu/maumivu wakati wa kujifungua?

Chini ya 1% ya wanawake wanaochomwa sindano kwenye uti wa mgongo wanapatwa na maumivu ya kichwa. Maumivu ya kichwa yanaweza kudumu kwa siku kadhaa, lakini yanatibika. Baadhi ya wanawake shinikizo la damu linashuka kwa muda mfupi baada ya kuchomwa sindano kwenye uti wa mgongo na wanaweza kuhitaji dawa nyingine ili kurudisha juu shinikizo la damu. Dawa aina ya opiods zinaweza kusababisha mtoto au mama kuhisi usingizi.

Je, nitahisi maumivu baada ya kujifungua?

Ni kawaida kujihisi maumivu baada ya kujifungua. Baadhi ya wanawake wanapata maumivu zaidi kuliko wengine. Baada ya kujifungua kwa njia ya kawaida, mwanamke anabakia na maumivu kwenye tumbo, uke na matiti. Baada ya kujifungua kwa upasuaji wa kutoa mtoto, wanawake wanaweza kuwa na maumivu karibu na mshono. Daktari atatibu maumivu kadri unavyohitaji na atajitahidi asikupatie dawa usizohitaji.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/patientinstructions/000625.htm

Leave feedback about this

  • Quality
  • Price
  • Service

PROS

+
Add Field

CONS

+
Add Field
Choose Image
Choose Video
X