MAUMIVU WAKATI WA KUMEZA:Sababu,dalili,matibabu

Maelezo ya jumla

Maumivu wakati wa kumeza yanaweza kuhisiwa mdomoni, kooni, au kwenye umio. Unaweza kuhisi maumivu wakati wa kumeza unapokunywa au kula chakula. Wakati mwingine, tatizo la kushindwa kumeza linaweza kuambatana na maumivu. Lakini mara nyingi tatizo la maumivu wakati wa kumeza hutokea lenyewe.

Ni zipi dalili za maumivu wakati wa kumeza?

Maumivu wakati wa kumeza yanaweza kuhisiwa mdomoni, kooni au kwenye umio. Unaweza kuhisi maumivu wakati wa kumeza wakati wa kunywa au kula chakula. Waktai mwingine, matatizo/ ugumu kumeza huambatana na maumivu, lakini mara nyingi tatizo la maumivu wakati wa kumeza kutokea jenyewe.

Ni nini husababisha maumivu wakti wa kumeza?maumivu wakati wa kumeza

Maumivu wakati wa kumeza yanaweza kusababishwa na tatizo dogo, kama vile mafua. Katika hali kama hizi, tatizo la maumivu wakati wa kumeza huisha lenyewe baada ya muda.

Maumivu wakati wa kumeza sugu yanaweza kuambatana na tatizo jingine. Kuna matatizo kadhaa ya kitabibu yanayoweza kusababisha maumivu wakati wa kumeza. Baadhi yao ni kama yafuatayo:

 • Wakati mwingine, maumivu wakati wa kumeza ya muda mrefu ni dalili ya awali ya saratani ya umio/koo. Maumivu yanasababishwa na uvimbe unaoota kwenye umio. Saratani ya umio/koo inaweza kutokana na uvutaji wa sigara wa muda mrefu, ulevi, au kiungulia cha muda mrefu. Inaweza pia kuwa ya kurithi.
 • Maambukizi ya fangasi: aina hii ya fangasi “candida” inaweza kutokea mdomoni. Fangasi hawa wanaweza kusambaa mpaka kwenye umio na kusababisha maumivu wakati wa kumeza.
 • Ugonjwa wa kubeua/kucheua asidi ya tumbo mara kwa mara: ugonjwa huu wa gastroesophageal reflux disease (GERD) hutokea kwa sababu ukanda wa chini wa umio unaozuia chakula kisirudi kutoka tumboni kuja juu haufungi vizuri. Kwa sababu ukanda huu haufungi vizuri, asidi iliyotumboni hupanda kuja kwenye umio. Asidi hii husababisha mchomo unaopelekea maumivu wakati wa kumeza na dalili nyingine kama vile, kiungulia na maumivu ya kifua.
 • UKIMWI: Matatizo ya umio hutokea sana kwa watu wanaoishi na UKIMWI. Fangasi aina ya “candida” huwapata zaid watu wenye UKIMWI. Wakati mwingine, dawa zinazotumika kupunguza makali ya UKIMWI husababisha kubeua/kucheua asidi. Hii inasababisha maumivu wakati wa kumeza.
 • Vidonda: Vidonda mdomoni, kwenye koo, au kwenye umio, na hata vidonda vya tumbo. Vidonda vinaweza pia kusababishwa na ugonjwa wa kubeua/kucheua asidi kama hautatibiwa mapema. Matumizi ya muda mrefu ya dawa za kupunguza maumivu aina ya NSAIDS kama vile ibuprofen, huongeza hatari ya vidonda.

Maumivu wakati wa kumeza kunaweza pia kusababishwa na matibabu, kwa mfano tiba ya mionzi kwa ajili ya kansa. Baadhi ya dawa zinazoandikwa na daktari zinaweza pia kusababisha maumivu wakati wa kumeza.

Ni nani yuko kwenye hatari zaidi ya kupata maumivu wakati wa kumeza?

Zifuatazo ni sababu zinazoongeza uwezekano wa kupata maumivu wakati wa kumeza:

Umri: kwa sababu ya kuzeeka na hali ya kawaida ya kuchoka kwa umio na kuna ongezeko la hatari ya kupata baadhi ya matatizo , kama vile kiharusi au ugonjwa wa parkinon, wazee wako kwenye hatari kubwa ya kupata matatizo wakati wa kumeza.

Utambuzi wa maumivu wakati wa kumezamaumivu wakati wa kumeza

Maumivu wakati wa kumeza hutambuliwa kwa kuingiza kamera ndogo kwenye umio “endoscopy”. Kamera hii ndogo hutumiwa na daktari kuangalia sehemu ya umio inayosababisha maumivu. Anaweza pia kukuambia umeze mate wakati wa kipimo.

Daktari anaweza kuagiza vipimo ili kuchunguza chanzo chochote anachoshuku kuwa kinaweza kuwa sababu ya shida yako. Lakini ni muhimu kujua kuwa, majibu ya vipimo vya damu yanaweza kurudi yakiwa sawa kabisa – hakuna shida yoyote.

Ni wakati gani unapaswa kutafuta usaidizi wa kitabibu?

Kama daktari asipoona sababu yoyote inayosababiha maumivu wakati wa kumza , anaweza kukuruhusu urudi nyumbani na maumivu yataisha yenyewe baada ya muda. Hii ni kawaida kama una mafua au umepatwa na mzio mkali. Ongea na daktari kama unapata shida hii ya maumivu wakati wa kumeza mara kwa mara.

Uchaguzi wa matibabu

 • Dawa
  • Kulingana na sababu ya maumivu wakati wa kumeza, yanaweza kutibiwa kwa dawa. Kwa mfano, dawa zinazoandikwa na daktari za kupunguza asidi tumbo zinawea kutibu tatizo la kubeu/kucheua asidi (GERD) na kuzuia asidi isirudi kwenye umio. Na kwa sababu hii, unaweza kuona maumivu yakianza kupungua.
  • Dawa pia zinaweza kutumika kutibu sababu ya maumivu, kama vile UKIMWI na maambukizi. Fangasi aina ya “candida” yanapaswa kutibiwa kwa dwa za kudhibit fangasi “antifungal agents”.
 • Upasuaji
  • Kwa visa vya saratani ya umio/koo, daktari anaweza kupendekeza kuutoa kwa upasuaji. Aina hii ya matibabu inaweza pia kutumiwa na wagonjwa kubeua/kucheua asidi (GERD) kama dawa hazitasaidia.

Kuzuia maumivu wakati wa kumeza

Hakuna njia mahususi ya kuzuia maumivu wakati wa kumeza, isipokuwa kutibu sababu ya tatizo husaidia.

Matarajio

Kama tatizo limetambuliwa mapema na kutibiwa, sababu nyingi hupona na maumivu hupungua au kuisha kabisa. Ni muhimu kuongea na daktari unapoona kuna dalili.

Kama hautapata matibabu ya tatizo hili, maumivu wakati wa kumeza na sababu yake husababisha matatizo mengine. Unaweza kupungua uzito kama matokea ya maumivu wakati wa kumeza chakula. Unaweza kula kidogo sana kwa sababu ya maumivu. Unaweza kupata matatizo mengine ya kiafya, kama vile upungufu wa damu, upungufu wa maji mwilini, na utapiamlo. Kama unaona moja ya haya, ongea na daktari haraka sana.

Matatizo yanayoweza kutokea

Tatizo linalosababisha maumivu wakati wa kumeza linaweza kusababisha matatizo mengine. Maambukizi yanaweza kuambaa au saratani inaweza kusambaa kwenye sehemu nyingine za mwili n.k. Kama tatizo linalosababisha maumivu ya kumeza ni la kawida, basi maumivu yataisha yenyewe bila matatizo yoyote.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/003116.htm

 

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi