1. Home
 2. MAUMIVU YA KIFUA
MAUMIVU YA KIFUA

MAUMIVU YA KIFUA

 • January 19, 2021
 • 0 Likes
 • 1422 Views
 • 11 Comments

Maelezo ya jumla

Maumivu ya kifua (chest pain) ni adha au maumivu unayohisi kwenye sehemu ya mbele ya mwili kati ya shingo na tumbo.

Ni nini husababisha maumivu ya kifua?

Watu wengi wanaopata maumivu kifuani hudhani kuwa ni mshtuko wa moyo. Lakini, kuna sababu nyingi sana za maumivu ya kifua. Baadhi ya sababu ni za kawaida, zinazosababisha usumbufu mdogo tu, lakini matatizo mengine yanaweza kutishia maisha.

Kiungo chochote kilicho kwenye kifua kinaweza kuwa chanzo cha maumivu, hii ni pamoja na moyo, mapafu, umio, misuli, mbavu, kano au neva.

Matatizo ya moyo yanayoweza kusababisha maumivu kifuani ni pamoja na:

 • Angina ni aina ya maumivu yanayotokana na matatizo ya moyo. Maumivu hutokea kwa sababu moyo haupati damu na oksijeni ya kutosha. Dalili kuu ya shida hii ni maumivu ya kifua yanayotokea nyuma ya mfupa wa kidari. Unaweza kuhisi kubwanwa kifuani. Maumivu yanaweza kusambaa mpaka kwenye mkono, bega, taya au mgongo.
 • Mshtuko wa moyo unaweza kusababisha maumivu makali sana kuliko ya Angina.
 • Kupasuka kwa aota kunaweza kusababisha maumivu makali ya ghafla kwenye kifua mpaka mgongoni.
 • Kuvimba au maambukizi kwenye tishu zinazouzunguka moyo, zinaweza kusababisha maumivu kwenye kifua.

Matatizo kwenye mapafu yanayoweza kusababisha maumivu kifuani:

 • Nyumonia, inasababisha maumivu kifuani, yanayoongezeka ukali unapovuta ndani pumzi.
 • Kama kuna donge la damu kwenye mapafu linaloziba mtiririko wa damu kwenda kwenye eneo dogo la mapafu au kuvimba kwa utando unaozunguka mapafu na kusababisha maumivu makali (kichomi). Maumivu huongezeka unapovuta pumzi ndani au unapokohoa.
 • Pumu pia husababisha kubwana pumzi, kukorota au kukohoa.

Sababu nyingine za maumivu kifuani:

 • Kukaza au kuvimba kwa misuli au kano(tendons) zilizo kwenye mbavu.
 • Mkanda wa jeshi (maumivu makali upande mmoja, yanayotambaa toka kifuani mpaka mgongoni)
 • Wasiwasi-Anxiety

Maumivu ya kifua yanaweza kutokana na matatizo ya tumbo:

 • Kiungulia
 • Vidonda vya tumbo
 • Matatizo ya mfuko wa nyongo (maumivu mara nyingi huwa makali zaidi baada ya kula, haswa chakula cha mafuta mengi)

Kwa watoto, maumivu mengi ya kifua hayasababishwi na matatizo ya moyo.

Wakati gani utafute matibabu?

Mwone daktari kama:

 • Unahisi maumivu makali ya ghafla yanayokaza na kubana kifua chako.
 • Maumivu yanasambaa mpaka kwenye taya, mkono wa kushoto au mabega.
 • Una kichefuchefu, kizunguzungu, unatokwa jasho, moyo wako unaenda mbio au unapata shida kupumua
 • Unajua kuwa una Angina na maumivu yako yanakuwa makali kuliko ilivyo kawaida baada ya kufanya kazi ya kawaida au kama maumivu yanadumu kwa muda mrefu zaidi.
 • Dalili za angina zinajitokeza ukiwa umepumzika
 • Una maumivu makali ya ghafla kwenye kifua yanayosababisha upate shida kupumua, hasa baada ya safari ndefu, au baada ya kupumzika kitandani kwa muda mrefu (mfano baada ya upasuaji), au baada ya kukaa sana bila kutembea-hii inapunguza mzunguko wa damu kwenye miguu na inaweza kusababisha madonge ya damu kutengenezeka.

Unapaswa kujua kuwa, hatari ya kupata mshtuko wa moyo inaongezeka zaidi kunapokuwepo na historia ya kuwepo kwa matatizo ya moyo kwenye familia, kama unavuta sigara, unatumia madawa ya kulevya, una kitambi au una kisukari.

Mwone daktari kama:

 • Una homa au kikohozi kinachotoa makohozi ya rangi ya njano au kijani.
 • Una maumivu makali ya kifua yasiyoisha
 • Unapata shida kumeza
 • Maumivu ya kifua yanayodumu kwa zaidi ya siku 3 mpaka 5.

Utambuzi wa maumivu ya kifua

Ikibidi, huduma ya dharura itafanyika. Unaweza kulazwa hospitalini kama hali ni mbaya au kama chanzo cha maumivu hakijafahamiki bayana.

Daktari atafanya uchunguzi wa mwili na kuangalia joto, mapigo ya moyo, upumuaji wako na shinikizo la damu. Uchunguzi wa mwili utalenga zaidi sehemu za kifua, mapafu na moyo. Daktari anaweza kukuuliza maswali kama yafuatayo:

 • Je, Maumivu yako wapi? katikati ya skapula? Chini ya mfupa wa kidari?
 • Je! Maumivu yanasambaa au kubadili mahala yalipo? Je! yako upande mmoja tu?
 • Je! Unaweza kuyaelezeaje maumivu yako? (Makali, ya kuchana, ya kuchoma, ya kuunguza, ya kubana, ya kukaza, ya kunyonga, yasiyo makali)
 • Je! Yanatokea kwa ghafla? Je, Maumivu hayo yanajitokeza wakati huo huo kila siku?
 • Je! Maumivu yanazidi? Je, Maumivu yanadumu kwa muda gani?
 • Je! Maumivu husambaa kutoka kwenye kifua mpaka kwenye bega, mkono, shingo, taya au mgongo?
 • Je! Maumivu yanzidi unapovuta pumzi ndani, unapokohoa, unapokula, au unapoinama?
 • Je! Maumivu yanazidi unapofanya mazoezi? Yanapoa baada ya kupumzika? Je unajihisi vizuri kabisa au yanatulia tu?
 • Je! Maumivu yanapungua unapotumia dawa kama nitroglycerin? Baada ya kunywa maziwa au kunywa antacids? Baada ya kucheua?
 • Je, kuna dalili nyingine yoyote?

Vipimo vinavyoweza kufanyika ni pamoja na:

 • Vipimo vya damu (kama LDH, LDH isoenzymes, CPK, isoenzymes za CPK, troponin, CBC)
 • ECG
 • ECG inayofanyika wakati wa mazoezi
 • Scan kya mapafu
 • Eksirei ya kifua

Vipimo vingine zaidi vinaweza kuhitajika, kulingana na ugumu wa utambuzi au sababu inayoshukiwa kuwa chanzo cha maumivu ya kifua.

Uchaguzi wa matibabu

Kama jeraha, kujikaza sana au kukohoa kumesababisha kukaza kwa misuli ya kifua, kifua kitakuwa kinauma. Hili linaweza kutibiwa nyumbani, jaribu kutumia acetaminophen au ibuprofen, barafu na kupumzika.

Kama unajua kuwa una pumu au angina tumia dawa kama ulivyoelekezwa na daktari wako.

Kuzuia maumivu ya kifua

Fanya mabadiliko ya mfumo wa maisha, unaweza kupunguza uwezekano wa kupata matatizo.

 • Jaribu kudumisha uzito wa kawaida
 • Dhibiti shinikizo la juu la damu,
 • Epuka kuvuta sigara au hewa yaenye moshi wa sigara.
 • Kula mlo bora
 • Pata angalau dakika 30 za mazoezi ya wastani kwa siku kadhaa za wiki.
 • Punguza msongo.

Vyanzo

http://www.nlm.nih.gov/medlineplus/ency/article/003079.htm

 

 • Share:

11 Comments

 •  miezi 2 ago

  Pole sana , maelezo yako hayajijitosheleza, kama unaweza tuambie ilianza lin? , una historia ya vidonda vya tumbo? umeumia? unapata kiungulia? una homa? sauti iko aje?

 •  miezi 2 ago

  Maelezo haya hayajajitosheleza, mfikishe kituo cha afya kupewa matibabu

 •  miezi 3 ago

  Kuna mtoto amebanwa ghafra analia anadai maumivu shida nn docter

 •  miezi 3 ago

  Mm Nina maumivu wakati wa kumez chakula mate apa kwenye chembe ya kitua nin tatizo

 •  miezi 3 ago

  Habari dakitari mmi nina tatzo la kifua kuuma upande wa kushoto karbu na moyo ambayo ina nipelekea shida kipumua sana. Na hali hii inatokea mara inatokea kwa mda nisaidie. Na makohozk yanatoka bila kukohoa

 •  miezi 3 ago

  habari, pole sana na asante kwa kuuandikia

  maumivu ya kifua ni dalili inayosababishwa na sababu nyingi, kwa sababu sijakufanyia uchunguzi wa kifua na kufanya vipimo stahiki, ni ngumu kukushauri moja kwa moja

  ningeshauri ufike kituo cha afya kwa ajili ya uchunguzi wa mwili na ikibidi vipimo ili kutambua sababu ni nini kwa ajili ya matibabu

  pole sana na karibu

 •  miezi 3 ago

  Hello Doctor, mimi huumwa na kifua nilianza na kukohoa kukohoa kulipoisha nmebaki na kuumwa na kifua na upande wa right kuko sensitive ni kama kumefura na ndani maybe damu haipiti vizuri na kinauma ninapolala sehemu moja kwa mda mrefu na niamkapo asubuhi je itakuwa ni nn

 •  miezi 3 ago

  Habari za asubuhi na pole sana

  Japo haujatoa maelekezo ya kujitosheleza ila nadhani una vidonda vya tumbo

  Ni vizuri ukafika kituo cha afya ili kupimwa h.pylori na kupewa matibabu sahihi

  Unawza kujifunza zaidi hapa kuhusu vidonda vya tumbo https://wikielimu.com/vidonda-vya-tumbo/

  Kama una swali zaidi, usisite kutuandikia na kama ni dharura tumia namba zilizopo hapi kutupata

  Asante na pole

 •  miezi 3 ago

  Habar daktar me nabanwa kifua na kinawaka moto na tumbo linauma sana namgongo haswa haswa wakat wa asubuhi nikipata mbweu mbili tatu tumbo linapungua Makalu yakuuma hadi linaacha kuuma ila ukila linaanza kuuma tena

 •  miezi 4 ago

  Habari za asubuhi na pole sana

  Japo haujatoa maelekezo ya kujitosheleza ila nadhani una vidonda vya tumbo

  Ni vizuri ukafika kituo cha afya ili kupimwa h.pylori na kupewa matibabu sahihi

  Unawza kujifunza zaidi hapa kuhusu vidonda vya tumbo https://wikielimu.com/vidonda-vya-tumbo/

  Kama una swali zaidi, usisite kutuandikia na kama ni dharura tumia namba zilizopo hapi kutupata

  Asante na pole

 •  miezi 4 ago

  Habar!! Docta mi napata maumivu katikati ya kifua kama msumali unanichoma hasa wakati wakuamka asbuhi. nikinywa chai hiyo hali itapoa kidgoo lakini pia na mshituko wa tumbo kma linawaka moto naomb ushauri tafadhali.

Leave Your Comment