Maelezo ya jumla
Kuvimba kwa wayo wa mguu ‘’plantar facitis’’ ndio sababu kubwa ya maumivu ya kisigino ‘’heal pain’’, mgonjwa anapata maumivu makali sana akikanyaga chini baada tu ya kuamka asubuhi au baada ya kukaa bila kutembea kwa muda mrefu. Tatizo hili linaweza kutokana na shughuli kama kukimbia, na unaweza kujihisi vibaya zaidi kama unakimbia peku au kama umevaa viatu vyenye soli nyembamba au iliyoharibika.
Sababu nyingine ya maumivu ya kisigino ni kuvimba kwa kano za kisigino ‘’achilles tendons’’ (Achilles tendinitis). Unaweza pia kupata maumivu ya kisigino kama umefanya mazoezi vibaya au umefanya mazoezi kupita kiasi au umefanya mazoezi ukiwa umevaa viatu vilivyoharibika. Dalili zinajumuisha maumivu ya kisigino yasioyoisha na mkazo au kukakamaa kwa kano za miguu.
Mwone daktari kama
Tafuta msaada wa kitabibu haraka sana:
- Kama umesikia ‘’snap’’ nyuma ya kifundo cha mguu wakati wa mazoezi (yawezekana kano ya kisigino imekatika ), una maumivu makali sehemu ya nyuma ya kifundo na /au huwezi kutembea vizuri
- Una maumivu ya kisigino baada ya kuumia au jeraha mguuni
Panga kumwona daktari kama una wasiwasi na hauna uhakika sababu ya maumivu ya kisigino
Unachoweza kufanya nyumbani ukiwa na maumivu ya kisigino
‘’Plantar fasciatis’’ na ‘’Achilles tendinitis’’ ni matatizo ambayo yanahitaji muda mrefu ili kupona. Fuata utaratibu ufuatao kwa wiki kadhaa ili kupunguza karaha
- Jaribu kuweka barafu (unaweza kuchukua barafu iliyowekwa kwenye kifuko, ukaitwanga na kuifunika na kitambaa chepesi, kisha ukaweka mahala penye shida). Ishikilie kwa angalau dakika 10. Rudia utaratibu huu mara 2-3 kwa masaa 48 ya mwanzo.
- Kama maumivu ya kisigino yamesababishwa na kuvimba kwa wayo wa mguu ‘’plantar facitis’’, pachue ‘’massage’’ kwa muda wakati wa asubuhi, baada ya kuoga maji ya uvuguvugu
- Tumia dawa za kupunguza maumivu kama vile ‘’ibuprofen’’ au ‘’acetaminophen’’ ili kupunguza karaha inayosababishwa na maumivu ya kisigino. Kama maumivu hayatapoa baada ya siku 4 – 5, ACHA kutumia madawa ya kupunguza maumivu umwone daktari
- Vaa viatu vinavyoshika na kutegemeza vizuri wayo wa mguu. Viatu vilivyowekewa pamba au vitu laini kwa ndani kama viatu vya michezo, vilivyofungwa vizuri vitasaidia sana. Kama umetegua kano ya kwenye kisigino ‘’achilles tendon’’ weka ‘’sponge’’ au ‘’heel pad’’ ambayo itasaidia kupunguza shinikizo kwenye kisigino na kupunguza maumivu unapotembea
- Punguza shughuli ambazo zinaongeza shinikizo kwenye kisigino, kama vile kukimbia au kucheza mpira wa ‘’tennis’’. Jaribu kuendesha baiskeli au kuogelea kama mbadala. Kama umetegua kano za kisigino, pumzika kabisa mpaka maumivu yatakapopoa na kisha anza mazoezi ya kunyoosha ndama ya mguu ‘’calf stretching exercise’’.
Kuzuia maumivu ya kisigino
Unaweza kulinda kisigino kisipate madhara unapofanya mazoezi na kukipunguzia shinikizo kwa kutumia mbinu zifuatazo
- Pasha miguu yako ‘’warm up’’ kabla ya kuanza kufanya mazoezi. Kama visigino vinaanza kuuma. ACHA; Usijaribu kufanya mazoezi ukiwa na maumivu.
- Ikiwezekana, fanya mazoezi kwenye nyasi au kimbia eneo la ndani ambalo sio gumu badala ya kukimbia kwenye lami
- Nunua viatu vya michezo ambavyo vimetengenezwa maalumu kwa ajili ya shughuli unayoifanya
- Viatu vya mazoezi vinapaswa kukutosha kabisa kuanzia mwanzo. Kama unafanya mazoezi mara kwa mara, chagua viatu vilivyoundwa kwa kusudi hilo; kwa mfano, kama unakimbia kwenye barabara ngumu. Unahitaji viatu vinavyotegemeza sehemu ya ndani ya mguu na vyenye ‘’cushion’’ kwenye kisigino.
- Unapokuwa unanunua viatu vipya, fuata hatua zifuatazo ili kuhakikisha viatu vinakutosha vizuri
- Vijaribu viatu unavyotaka kununua ukiwa umevalia ‘’socks’’ utakazovaa navyo
- Angalia kama viatu vinatoshea vizuri na kushika kisigino na vinakuachia nafasi ya kuchezesha vidole kwa uhuru. Funga kamba za viatu mwenyewe upya ili vibane vizuri na kuongeza shinikizo kwenye sehemu ya juu ya mguu
- Tembea au kimbia hatua kadhaa ili kuamua au kungalia kuwa viatu havikutii karaha yoyote
- Wakati ambao haufanyi mazoezi vaa viatu vinavyokutosha vizuri na vinavyotegemeza vizuri mguu (hasa sehemu ya uwazi iliyo kwenye uwayo ‘’arch’’), weka ‘’sole cushions’’ kupunguza shinikizo na viatu visiwe na kisino kinachozidi 5cm
- Fanya mazoezi ya kunyoosha ndama ya mguu ‘’calf stretching exercise’’ ili kulegeza misuli na kupunguza uwezekano wa kupata majeraha
- Simama umbali sawa na mikono ikiwa imekujuliwa, mguu mmoja ukiwa mbele ya mwingine na mikono ikiwa imeshika ukuta usawa wa mabega yako.
- Hakikisha miguu imekaa ‘’flat’’ kwenye ardhi, egemea kwenda mbele, kunja goti la mguu wa mbele na sukuma kisigino cha mguu wa nyuma kwenda chini ardhini. Utahisi misuli ya ndama ya mguu ilijinyoosha. Rudia zoezi hili kwenye mguu mwingine.
- Kama una uzito mkubwa, punguza uzito itasaidia kupunguza shinikiza juu ya miguu yako
Mwone daktari kama
Panga kumwona daktari kama:
- Maumivu haya japoa baada ya wiki kadhaa au kama yanazidi kuwa makali zaidi
Leave feedback about this