Last Updated on October 13, 2023 by Dr Mniko
Maelezo ya jumla
Maumivu ya meno yanaweza kuwa ya kadri unayoweza kuyavumilia au yanaweza kuwa makali sana, yanayokuwepo wakati wote, unahisi kama jino lina puta puta. Kuoza kwa meno kwa sababu ya usafi duni wa meno ndio sababu kubwa ya tatizo hili, lakini maumivu kwenye jino yanaweza pia kutokana na ugonjwa wa fizi, jino lililopasuka au kuvunjika au matatizo ya taya. Vijana walio kwenye balehe na watu wazima wanaweza kuwa na maumivu wanapokuwa wanaota meno ya mwisho (meno yanayoota baadae).
Kwa baadhi ya watu meno yao yanakuwa na ukakasi “sensitive ” na yanashindwa kuhimili vitu vya baridi au vya moto. Wanaweza pia kuhisi maumivu au kujisikia vibaya wakati wa kusugua meno kwa sababu ya kuisha kwa ganda la juu linalofunika jino ‘’enamel’’ na kwa sababu hiyo jino linalika au kupasuka kwa urahisi.
Mwone daktari haraka
Ni vizuri kumwona daktari mapema kadri iwezekanavyo kama unapata maumivu makali sana, yanayokuwepo muda wote unapouma kitu, kama una homa, mdomo wako unatoa harufu mbaya au/na kama uso wako umevimba. Kuna uwezekano una jipu kwenye jino
Unachoweza kufanya wewe mwenyewe ukiwa na maumivu ya meno
Unaweza kufanya mambo yafuatayo ili kupunguza maumivu ya jino wakati unasubiria miadi ya mtaalamu wako wa meno au kwa ajili ya kupunguza ukakasi ‘’senstivity’’ ya meno
- Epuka kula au kunywa kitu chochote ambacho ni cha moto sana au cha baridi sana kama kinafanya maumivu kuzidi. Kwa baadhi ya watu huwa inasaidia kupunguza maumivu kama watanyonya barafu au kuweka barafu kwenye jino linalouma. Acha kama unaona jino linaanza kuuma
- Sukutua mdomo wako vizuri kwa maji yenye chumvi. Kuutengeneza mchanganyiko huu ‘’mouthwash’’, changanya kijiko kimoja cha chumvi kwenye kikombe kimoja cha maji (250mls)
- Unaweza kuweka mafuata ya karafuu ‘’clove oil’’ kwenye jino linalouma. Hii ni tiba ya asili na unaweza ukapata mafuata haya ya mkarafuu kwenye maduka ya dawa, mafuta haya yanapunguza maumivu na kupooza jino linalouma. Weka matone kadhaa kwenye pamba, iweke kwenye jino linaluma kisha iume. Kuwa makini mafuata yasiufikie ulimi wako, kwa sababu yanaunguza ulimi kidogo.
- Meza madawa ya kupunguza maumivu kama vile ‘’acetaminophen’’ au ‘’ibuprofen’’. Kwa watoto unaweza pia kuwapatia ‘’acetaminohen au ibuprofen , muulize mtaalamu wa dawa akupatie dawa za maji za kunywa kwa ajili ya matumizi ya watoto
- Unawez kutumia nyuzi ya hariri ‘’floss’’ kusafisha vizuri jino linalouma, ondoa vipande vya vyakula vilivyokwama hapo taratibu kwa kupita kila upande wa jino. Uchafu unapokuwepo kwenye jino unaweza kuongeza maumivu
”Floss” - Kama meno yako yana ukakasi ‘’sensitive’’, sugua meno yako kwa kutumia mswaki taratibu kwa kutumia dawa ya mswaki iliyotengenezwa maalumu kwa ajili ya tatizo hili. Kama hauna dawa hii, nenda duka la dawa mtaalamu wa dawa atakupatia. Baada ya kusugua meno yako vizuri, chukua dawa ya meno kidogo, ipake kwenye meno yako na kisha iache hapo kwa usiku mzima
- Kuwa na mpango au utaratibu mzuri kuhusu usafi wa kinywa chako ili kuzuia meno zaidi kuoza
Jinsi ya kusafisha kinywa ukiwa na maumivu ya meno
Ukifuata hatua zifuatazo wakati wa kufanya usafi wa kinywa, itasidia kupunguza hatari ya magonjwa ya fizi na kuzuia meno kuoza. Piga mswaki angalau mara mbili kwa siku na badilisha mswaki wako kila baada ya miezi 2-3. Safisha katikati ya meno yako kwa kutumia nyuzi za Hariri ‘’floss’’.
- Piga mswaki kabla ya kwenda kulala na unapoamka asubuhi au baada ya kupata kifungua kinywa. Tumia dawa ya mswaki yenye magadi ‘’fluoride’’ na mswaki laini. Hakikisha unasafisha sura zote za meno, hasa sehemu meno yanapokutana na fizi kwa kuvuta mswaki kwenda kuu
- Unaweza kutumia nyuzi za Hariri ‘’floss’’ ili kusafisha kati kati ya meno mara moja kwa siku. Funga upande wa nyuzi kwenye kidole cha mkono mmoja na upande mwingine kwenye mkono mwingine na kisha telezesha uzi juu mpaka chini, juu mpaka chini kwenye upande wa kila jino na ukitumia kipande kipya kwa kila jino unalopita
Leave feedback about this